Ukiwa mtu maarufu halafu masikini usipende kusimanga watu, Ipo siku litakukuta jambo Watu watakupita kama nyanya mbovu

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,283
21,397
Masikini akipata, matako huria mbwata!

Mhenga aliyesema hivi hakuwa na maana ni kweli makalio yatabwata!

Alimaanisha ukipata kitu basi usiwakwaze wengine!
Kuna watu wamejipambanua kwa majina makubwa sana mtandaoni, wanatambulika kama public figure machonj pa watu!

Lakini pamoja na yote, kwa umaarufu wao wanajiona wapo tofauti sana na watu wengine!
Kwasababu ya umaarufu wao wanapongeza hata machungu ya kustahili kukemewa!

Mfano!
1. Bunge lilivyozimwa live, wananchi wengi waliumia, lakini baadhi ya watu maarufu walipongeza kwa kuona wapo tofauti,
2. Wakati wa mswada wa sheria na maudhui ya mtandao yalipokuja watu walipiga kelele, laki hao maarufu waliona haiwahusu wakapongeza etc

YANAOPOKUJA KUWAKUTA YA KUTOKEA, WANARUDI KWENYE JAMII ILEILE KUOMBA MSAADA!

Wanajipambanua machoni pa watu wanakila kitu, wanasuka nywele za 1mil, wanavaa suti za 2mil, wanajimwambafai wao kuwa ni wanawake wa shoka! Wanatetea hata upuuzi unaoumiza!

Halafu siku yanapowakuta ya kuwakuta mfano faini ya 5mil tu wanakuja kuomba msaada kwa jamii ileile!

Mi naona watu maarufu wa namna hii wanapokutwa na jambo tusiwachangie chochote! " waacheni wafu wazikane"

Tuwapite kama nyanya mbovu ili wajifunze kucheka au kuumia pamoja na jamii inapoumizwa!
 
Mm nikisikia msanii anataka achangiwe pesa ata nauli SITOI jitu linafanya vurugu ya pesa afu unampa pesa km chidbenz kipindi cha madawa ya kulevya mm siwez toa huyu jamaa alikuja shulen kwetu kuperform haaah yaan fujo tu mademu tu gar mbili utasema kuna watu wanamfuatilia wamuue akayan sitoi
 
Huenda Joyce kilia wa wanawake live kakusikia, naona huko IG anazungusha beseni kuomba mchango wa faini ya Tsaraei ,ile faini alipe mwenyewe tu asituchoshe kuchanga!
Halafu si tulikubaliana omba omba waondolewe mjini au hilo liliwahusu wale wanaotoka ukoo wa matonya tu?
 
Huenda Joyce kilia wa wanawake live kakusikia, naona huko IG anazungusha beseni kuomba mchango wa faini ya Tsaraei ,ile faini alipe mwenyewe tu asituchoshe kuchanga!
Halafu si tulikubaliana omba omba waondolewe mjini au hilo liliwahusu wale wanaotoka ukoo wa matonya tu?
Haaa haaa haaa
 
Back
Top Bottom