Ukiusikiliza mjadala wa TBC juu ya Chanjo ya Corona, utaihurumia Afrika

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,162
Ukifuatilia mjadala unaoendelea TBC juu ya chanjo ya COVID-19 na maswala ya uzalendo utangundua kuwa bado tuko na matatizo makubwa Africa.

Ukiutizama mjadala umejikita juu ya kuuponda ukoloni ambapo ni jambo jema ingawa ni mada ya kizamani. Ukiwasikiliza wasomi wanaochangia hizo mada, wamejikita kuwaponda wazungu badala ya kuwaambia Watanzania kuwa wao wamefanya nini.

Unamsikiliza Prof Mgaya akieleza huchukua takribani miaka 7 hadi 10 kupata chanjo rasmi, anasema hii chanjo inayotolewa iko katika majaribio, kwamba ufanisi wake ni kwa asilimia kidogo, je hizi dawa za miti shamba tunazoambiwa zinatibu Corona, Covidol, NIMRCRAF na ile iliyofuatwa kwa ndege ya umma Madagascar ilifanyiwa majaribio miaka mingapi? . Hapa unajiuliza, kama kwa siku nchi inaweza kupoteza maelfu ya watu, je inabidi usubiri miaka 10 ndipo uzuie vifo? Lakini je ni kweli kwa technolojia ya sasa karne ya 21 ni lazima usubiri miaka 7 au 10 ndipo ujue chanjo inafanya kazi au la? Haya ni maswali ya kujiuliza.

Jambo la mwisho, wasomi hawa wanaoendesha mjadala, hawasemi kabisa kuwa serikali imefanya nini hadi sasa kuwekeza kwenye uvumbuzi wa chanjo yetu binafsi ya Corona, inakuwaje wewe hata kujaribu hufanyi halafu unainua mdomo wako kuponda chanjo zinazotoka nje ya nchi?. Je kwanini Tanzania hatuandai chanjo zetu? kama tunaweza kutumia mabilioni ya pesa kujenga miundombinu ambayo haina manufaa kwa wananchi, inakuwaje tushindwe kutumia mabilioni kuwekeza kwenye chanjo zetu badala ya kulalama na habari ya chanjo ya tunaowaita mabeberu?
 
Moja ya mambo makubwa ambayo utawala wa awamu ya tano umefanikiwa, ni kuonesha namna watanzania wengi tusivyo na Akili, kwa hiyo ndugu yangu mtoa mada Wala usipate shida, huo uprof wao Wala usikupe shida, kuwa Prof na kuwa na Akili ni vitu viwili tofauti
 
Ninauangalia mdahalo huu. Mkuu:

1. Prof. Mgaya ni mtalaamu wa chemistry. Mwalimu wa jiwe. Yuko NIMRI kwa hisani ya huo ukweli. Anaongelea mambo ya dawa za binadamu. Utegemee nini?

2. Floor imejaa uvccm - kina johnthebaptist Unategemea nini hapo?

3. Kuna time saver moja (advocate Sibanda) limesafirishwa kuja Tanzania lina lala na kulishwa na Tanzania eti ni admirer wa namna tunavyo pambana na Corona.

Utegemee nini kwenye hili jopo la wasaka teuzi na wale wasiojulikana?
 
Ma Profesa na Ma doctors wetu wanajitoaga ufahamu, sijajua sababu hua roho inauma saaana, mwingine majuzi anazingua machine ya kujifukiza!!!!

Nilitegemea angewaita Wana kemia wabobezi nchini wakaingia maabara,lakini anazingua mashine iliyotoka SIDO!!!!

SIDO wamefeli hata kutengeneaa ventilator, wamefeli hata machine ya kukamua mawese, alizeti hata ya kupukuchua mahindi.

Bora mie kapuku la Saba B.
 
Yaani wabongo bana mara utawasikia ooh mimi siangaliagi TBC , cha ajabu kumbe ndio wako sit ya mbele.
All in all lecture imetolewa na hao african patriots
Sikia hayo madini acheni negativity na roho zenu za ndoano.
IMG-20201230-WA0004.jpg
 
Prof Mgaya ameteuliwa na Rais.Msimamo wa Rais katika janga hili unajulikana,no lockdown,herd immunity,promote herbal medicine.Je yeye afanyeje?
Kama mngejiuliza chanjo ni nini, nadhani msingekuwa mnapingana na msimamo wa wizara ya afya na serikari.
 
Nimelisoma bandiko lako. Kwa kiasi fulani lina hoja. Mfano mpaka sasa tumefikia wapi kupata chanjo ya ugonjwa wa uviko-19. Hilo ni suala na swali la msingi.

Lakini kuja kwenye chanjo ambayo sasa inatawanywa. Haina tofauti yoyote na ile nyungu inayotumiwa na akina msukuma wa ushetu. Chanjo hizo zilipitishwa kwa emergency approval na wanavyosema dharura ni kwamba iliruka baadhi ya hatua ili kukidhi matakwa ya chanjo halisi. Na kama umefuatilia watoa chanjo hawana uhakika na ufanisi wake. Ndiyo maana hata ukipata chanjo. Unasisitiziwa kuendelea kujikinga na kuchukua tahadhari kama mtu ambaye hajapewa a jab. Unapaswa kuchukua tahadhari kama vile ulivyokuwa ukichukua tahadhari hizo kabla ya kupata chanjo.

Ukifuatilia chanjo zote zilizowahi kutolewa duniani, watu waliopewa chanjo hawakuambiwa wachukue tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kupata chanjo.

Lingine ni kuwa chanjo hizi hazitegemewi kwamba zitaweza kumdhibiti huyu kirusi kigeu geu. Maana ukimtengenezea chanjo A kesho anageuka kuwa B.

Lingine kwa ufupi ni muda wa hiyo kinga kukaa mwilini, bado hijajulikana. Baada ya kupata chanjo, ni miaka mingapi utakuwa imara bila kushambuliwa na virusi hivyo.

Mwisho nasema, tunaweza kushangilia chanjo hii aghali, kumbe tunapewa placebos.
Naomba kuwasilisha.
 
Kama mngejiuliza chanjo ni Nini,nadhani msingekuwa mnapingana na msimamo wa wizara ya afya na serikari.
Hawa wakiona mzungu wanachanganyikiwa ndio maana waepewa ubarozi wa kutetea mashoga
 
Umekimbilia kutoa thread ya iliyoegemea upande moja ili wengine wakitoa thread zao objective zisiruhusiwe!

Eti mdahalo umejaa kuponda ukoloni! Nina wasiwasi Kama unajua maana ya ukoloni, vinginevyo usingesema hivyo. Hata hivyo walichofanya ni ku present facts, ugonjwa ulianzaje, kitaalam chanjo mpaka ithibitishwe kutumika inapitia hatua zipi? Na je chanjo hizi zimepitia hatua hizo?

Hoja ya Prof Mgaya na siyo hoja yake bali ukweli wa kisayansi chanjo hizi za korona bado ziko kwenye majaribio (experimental stage). Tafsiri yake ni kwamba si uthibitisho wa kwamba zinazuia ugonjwa huu, na vilevile inawezekana zikawa na madhara na inawezekana vilevile baadhi zikaondolewa zikionekana na madhara.

Lawama eti serikali na taasisi zake wamekaa tu. Mgaya kaeleza nchini kuna dawa 7 ziko kwenye majaribio
 
Hawa wakiona mzungu wanachanganyikiwa ndio maana waepewa ubarozi wa kutetea mashoga

Bwana Soviet Union umerejea kwa nguvu mpya, kasi mpya na ari mpya.

Kulikoni ulikuwa unapigisha nyungu mitaa ya wapi mkuu?
 
Back
Top Bottom