Ukiumwa na nyoka au tandu huduma ya kwanza ni nini?

CELLULAIRE

Member
Mar 16, 2016
76
97
Mlioumwa na hao wadudu wakali wanaotambaa karibuni mtupe uzoefu wenu wa kitabibu mliopata au kwenye ujuzi basi tupeni na sisi ushauri wa dawa au tiba ya kutumia.
 
Unataka tiba ipi? Ya hospitali au asili?

Kwa issue ya nyoka naona tiba asili ndo imesambaa kuliko morden one/ya hospitali. Kwa sababu wahanga ni wale wanaoishi huko porini ambako nyoka ni wengi tofauti na mijini.

Kuna dawa za kupambana na sumu ya nyoka, Antivenins au Anti Snake Venom (ASV). Kwa nchi yetu ya kimaskini zinapatinana kwenye hospitali chache mno, na huko vijijini hazipo kabisa au umbali wa kuifuata huduma hiyo ni mrefu kiasi kwamba kama nyoka ana sumu kali mtu atapoteza maisha kabla ya kufika kituoni.

Huduma ya kwanza ni muhimu, kwa kuifunga sehemu iliyoumwa kwa juu ili kuzuia sumu kusambaa. Then, kijijini niliona walichanja sehemu ile na kuweka JIWE LEUSI na nyumbani tulikuwa nalo. Then, mtu atapelekwa hospitali.

Lakini kama atawahi huduma na ikawepo atachoma sindano;
1. Antivenins
2. Ceftriaxone/powercef, kwa kuwa nyoka anahifadhi bacteria kwenye mdomo wake ni muhimu mgonjwa achome antibiotic hii.
3. Pia, atachomwa ya kuzuia Tetanus.

Kwa upande wa tiba ASILI watakuja wajuvi.

Lakini, niliumwa na Ng'e nilipokuwa high school. Maumivu yalikuwa makubwa ... Wakanichanja na wembe sehemu ile na kuniwekea Tshs 100. Ilikaa pale baada ya muda ikadondoka na uvimbe uliondoka.

Pamoja na mengine, nitapenda mtu anijuze;
1. Uhusiano wa Tshs 100 na sumu ya wadudu,
2. Hilo jiwe LEUSI la nyoka.
 
Back
Top Bottom