Ukitaka kutoa ubunge wa 2025

Ukitaka kutoa ubunge wa 2025

Bosi Kalewa

Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
7
Reaction score
4
Unayetaka jimbo 2025, acha kulala lala jiandae kuanzia sasa. Shiriki shughuli za kijamii hasa mambo kama ya misiba.

Ukiweza weka harambee kwa ajili ya mfuko wa maendeleo. Tembelea wafanyabiashara wadogo na wakubwa masokoni.

Ongea sana na vijana wenye shughuli za kila siku kama bodaboda. Zingatia katika maongezi onesha utofauti wako wa kiakili na wao.

Jenga ukaribu na heshima kwa viongozi wa kiroho wa dini zote.
Shiriki kwenye vikao ambavyo vinahusu jamii inayokuzunguka.

Kote huko toa mawazo chanya ambayo yatatatua changomoto zao. Uwe mtu ambaye uwepo wako unaleta nafuu kwao bila hata kutoa pesa.

Heshimu watu wote, badili nyendo zako kama uzinzi na ulevi. Bila kuishi namna hii majimbo ya 2025 utayasikia mitandaoni tu.
 
Back
Top Bottom