Ukistaajabu ya Samatta Utayaona ya Mkwasa

Mwanagandila

Senior Member
Oct 9, 2011
182
100
Ukistaajabu ya Samatta utayaona ya Mkwasa

Ni takribani wiki moja sasa tangu mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta ashinde tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani(Best Player based in Africa).

Tangu Samatta kushinda tuzo hiyo na kurejea nyumbani, mambo mengi yamejitokeza ikiwemo kosoa kosoa nyingi kutoka kwa kila anayeujua mpira wa miguu.

Mwezi mmoja kabla Samatta hajashinda tuzo hiyo hakuna aliyekua akimuongelea, kuanzia serikali mpaka mwananchi wa kawaida, lakini baada ya usiku wa tarehe 7 Januari 2015 mambo yamebadilika.

Wajanja wa mjini wakatumia fursa kupitia mgongo wa serikali, wakamsainisha mkataba kabla hajasafiri kuelekea Nigeria, na sass ndio wanaomuongoza mchezaji huyo kwa kila jambo.

Kabla ya kutwaa tuzo hiyo, serikali na hao wajanja hawakuwahi kujua Samatta amekua vipi, amepitia Changamoto zipi mpaka kufikia hapo alipo, wanapoona raha kumuandalia events za kumpongeza usiku kana kwamba yeye ni mssanii wa muziki.

Ajabu Mbwana alitembezwa Dar katika wilaya mbili, bila matembezi hayo kugusa mtaani kwake alikozaliwa na kuanza kucheza mpira Mbagala, ila matembezi yakaishia Ufukweni kwa ajili ya manufaa ya wajanja.

TFF imewekewa mipaka ya kuonana na mchezaji huyo na wajanja wanaommiliki, kwa kisingizio serikali imesema, Waziri kasema, ilihali TFF ndo walezi wa Samatta kimichezo ndani na nje ya nchi.

Samatta amepitia changamoto nyingi sana mpaka kufikia mafanikio hayo, serikali ilipaswa kuwekeza na kuwasaidia vijana wengi wenye vipaji ili kuweza kuzalisha wachezaji wengine kama Samatta.

Watoto hawana viwanja vya kuchezea, maeneo ya wazi yameuzwa, walimu wa kufundisha mpira hakuna, serikali inatazama tu na mwisho wa siku timu ya taifa ikifanya vibaya hakuna anayetezama tulipojikwaa.

Serikali na wajanja wa mjini wamemuandaliwa events hizo zote Samatta kwa kua amefanya vizuri, walikua wapi kabla ya kijana huyo hajashinda tuzo? InakuajeTFF leo hii inawekewa mipaka ya kuonana na Samatta ikiwa haikuwahi kuwa hivyo kabla ya kushinda tuzo hiyo?

Leo hii chimbuko la vipaji vya michezo na timu kufanya vizuri ni makocha, serikali na hao mameneja wa dakika za nyongeza za mchezo wamefanya nini kuhakikisha wanazilishwa kina Samatta wengine?

Mkwasa tangu ateuliwe kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars ni zaidi ya miezi mitano, serikali imekataa kumlipa mishahara yake, nyumba ya masaki wameichukua, halafu akishinda kombe la CHAN/AFCON mtampongeza Mkwasa na kumuandalia sherehe kama za Samatta pamoja na mameneja wa dakika ya 93??

Hii inatokea Tanzania pekee ambapo ambao hawakushiriki kumkuza, kumlea mchezaji wanapata ujasiri wa kujitanua kifua mbele kama wamepigwa ngumi za mgongo, ikiwa wakati wa njaa hawakuonekana na sasa wamejitokeza wakati wa mavuno.

Namalizia kwa kusema, Ukistaajabu ya Samatta utayaona ya Mkwasa.
 
waliompa mkataba Mkwasa ni TFF wao ndio walipaswa kuhakikisha vitu hivyo badala ya kulialia kwa serikali pia Mkwasa alipaswa ajue hayo kabla ya kuvunja mkataba na Yanga zaid sioni haja ya kumapatia hayo yote kocha aliyetupatia kipigo cha aibu kwa algeria tungefungwa angalau 4 lakini saba ni aibu
 
wampe timu ya taifa yule kocha aliyetimuliwa simba kwa jinsi nilivyomchunguza ni bonge la kocha...
 
Ukistaajabu ya Samatta utayaona ya Mkwasa

Ni takribani wiki moja sasa tangu mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta ashinde tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani(Best Player based in Africa).

Tangu Samatta kushinda tuzo hiyo na kurejea nyumbani, mambo mengi yamejitokeza ikiwemo kosoa kosoa nyingi kutoka kwa kila anayeujua mpira wa miguu.

Mwezi mmoja kabla Samatta hajashinda tuzo hiyo hakuna aliyekua akimuongelea, kuanzia serikali mpaka mwananchi wa kawaida, lakini baada ya usiku wa tarehe 7 Januari 2015 mambo yamebadilika.

Wajanja wa mjini wakatumia fursa kupitia mgongo wa serikali, wakamsainisha mkataba kabla hajasafiri kuelekea Nigeria, na sass ndio wanaomuongoza mchezaji huyo kwa kila jambo.

Kabla ya kutwaa tuzo hiyo, serikali na hao wajanja hawakuwahi kujua Samatta amekua vipi, amepitia Changamoto zipi mpaka kufikia hapo alipo, wanapoona raha kumuandalia events za kumpongeza usiku kana kwamba yeye ni mssanii wa muziki.

Ajabu Mbwana alitembezwa Dar katika wilaya mbili, bila matembezi hayo kugusa mtaani kwake alikozaliwa na kuanza kucheza mpira Mbagala, ila matembezi yakaishia Ufukweni kwa ajili ya manufaa ya wajanja.

TFF imewekewa mipaka ya kuonana na mchezaji huyo na wajanja wanaommiliki, kwa kisingizio serikali imesema, Waziri kasema, ilihali TFF ndo walezi wa Samatta kimichezo ndani na nje ya nchi.

Samatta amepitia changamoto nyingi sana mpaka kufikia mafanikio hayo, serikali ilipaswa kuwekeza na kuwasaidia vijana wengi wenye vipaji ili kuweza kuzalisha wachezaji wengine kama Samatta.

Watoto hawana viwanja vya kuchezea, maeneo ya wazi yameuzwa, walimu wa kufundisha mpira hakuna, serikali inatazama tu na mwisho wa siku timu ya taifa ikifanya vibaya hakuna anayetezama tulipojikwaa.

Serikali na wajanja wa mjini wamemuandaliwa events hizo zote Samatta kwa kua amefanya vizuri, walikua wapi kabla ya kijana huyo hajashinda tuzo? InakuajeTFF leo hii inawekewa mipaka ya kuonana na Samatta ikiwa haikuwahi kuwa hivyo kabla ya kushinda tuzo hiyo?

Leo hii chimbuko la vipaji vya michezo na timu kufanya vizuri ni makocha, serikali na hao mameneja wa dakika za nyongeza za mchezo wamefanya nini kuhakikisha wanazilishwa kina Samatta wengine?

Mkwasa tangu ateuliwe kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars ni zaidi ya miezi mitano, serikali imekataa kumlipa mishahara yake, nyumba ya masaki wameichukua, halafu akishinda kombe la CHAN/AFCON mtampongeza Mkwasa na kumuandalia sherehe kama za Samatta pamoja na mameneja wa dakika ya 93??

Hii inatokea Tanzania pekee ambapo ambao hawakushiriki kumkuza, kumlea mchezaji wanapata ujasiri wa kujitanua kifua mbele kama wamepigwa ngumi za mgongo, ikiwa wakati wa njaa hawakuonekana na sasa wamejitokeza wakati wa mavuno.

Namalizia kwa kusema, Ukistaajabu ya Samatta utayaona ya Mkwasa.
Mkuu, mie bwana Mkwasa kumpa timu ya Taifa siridhii asilan na hii inajidhihirisha kwa uwezo wa Samata na Tomas. Wachezaji hawa wanaupeo mkubwa mno kumzidi Mkwasa.
 
Back
Top Bottom