Ukishafika miaka 40 STAAFU

Ukishafika miaka 40 STAAFU

stakehigh

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2019
Posts
18,933
Reaction score
14,706
Japokua umri wa kustaafu hua ni miaka 60 uliozoeleka ila kwa jinsi mwili ulivotengenezwa peak performance yake ni miaka 35 baada ya miaka hio viungo vyote ya mwili hua vimefika kikomo katika ufanisi wa kufanya kazi kwa ufasaha, mbelen ap inategemeana tu Mungu alivokubariki ama kama ulijitunza vizuri na mazoezi apa na pale unaweza kwenda kwenda ila sio sana, kwahio peak kabisa ni miaka 40

Ukishafika miaka 40, kiuhalisia umeshaishi nusu ya maisha kama utabarikiwi kufika 80+ ila kwa life expectancy iliozoeleka apo umeshaingia ukubwan 100%, Ngozi huanza kudhoofika, magonjwa kadhaa yatakuandaama, vidonda huchukua mda mrefu kupona na kwa wanamichezo ndo hali inakua mbaya zaidi ni ngumu kuweka performance ya kiushindani ndo maaana miaka 33 mpaka 35 mchezaji ashastaafu, mwili hufika kikomo

Kwa sisi ambao sio wachezaji huu ndo mda mzuri wa kula matunda yako, kukaa na familia karibu na kutoa mwongozo wa apa na pale kwa watoto sio mda wa kukomaa ofisini tena, tumia huu mda kutunza nguvu ulioikusanya katika ujana wako, na utaishi mda mrefu zaidi bila athari za magonjwa ya apa na pale

Hatusemi hautakufa ila uzee wako utakua wa kula ulichopanda badala ya kuanza kujenga urafiki na manesi
 
1760310962631.png
 
nipo kwenye 40s, tangu nianze harakakati zangu za utafutaji miaka kadhaa iliyopita, last week ndio nimebutua deal la maana lenye fedha nyingi. ningekuwa na mtizamo hasi kama huu wako, hilo deal nisingelipata. so acha kukatisha watu tamaa.
 
Hivi unajua 40 years ni miaka 15 baada ya 1st degree?

Hapo ndio imeanza kuingia kwenye Executive committee.. kama una bahati..

Ungesema labda 55 sawa, ila 40 unasema mwil umechoka?

Unadhani kila mtu ni mcheza mpira?

Age just a number, tokeni usingizini..

Hivi Trump ana Sabina ngap?
 
Mbona usemi huo haufanyi kazi huko CCM?

Mtu ana miaka 80 lakini bado anateuliwa wakati huo Vijana wanaachwa bila ajira

Miaka 40, Kibongo bongo unakuta bado hujatoboa maisha
 
Miaka 42 wengine wanasubilia kuitwa kazini ajira mpya, kweli maisha hayana formula wewe mzee wa chama hebu wafikirieni hao viumbe walau nao waonje mema ya nchi.
 
Back
Top Bottom