Ukipatwa na msiba nyumbani kwenu usianze kupiga kelele au kutoa taarifa kabla ya kufanya yafuatayo

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
3,967
12,951
Kwanza msitiri marehemu, Hii ni kwa wale waliofia nyumbani, muweke katika hali ya usafi (maana wengine roho inapotoka inatoka na takamwili) hivyo marehemu kujichafua. Hakikisha marehemu umemsafisha na umemuweka sawa.

Pili, anza kusafisha mazingira ya pale home.
Wabongo wengi huwa tufanya usafi sehemu za machoni Ila sio zile nyeti ambazo hazionekani kwa watu.

Baada ya kufanya hayo mambo makubwa mawili sasa ndio unaweza kuanza kukola ngolo na kutoa taarifa.
 
Kuhusu kutokutoa taarifa hadi marehemu awekwe vizuri ni jambo la maana sana. Sema Sio rahisi sana kwa wenye hisia kali kutokupiga kelele za kilio labda kwa wenye ukomavu sana.
Kikubwa jaman tujifunzeni kusafisha nyumba zetu mda wote tusisubiri hadi matatizo yafike.
Mfano kila week mara moja unaweza kuwa unasogeza vitu kama viti na vitanda ili kudeki sehemu ambazo hazifikiki kwa urahisi...
Pia utaratibu wa kulima majani yanayozunguka nyumba pamoja na kufyeka mapori.
Ukiwa na utamaduni huu siku ya matatizo watu hawawezi kukukuta na aibu ndogo ndogo kama hizi.
 
Kweli nakumbuka mzee wangu alipovuta maza alisafisha chumbani kwake takataka na nguo kuukuu alikusanya na kuchoma zote, godoro alilokojolea mzee lilionekana baada ya matanga, pia vitu fulani fulani alifungia chumba kimoja kwa usalama zaidi maana msibani wezi na wadokozi wapo pia, kama chumba hakina kufuli kuwe ba mtu maalumu kwa ajili ya kusimamia usalama wa ndani.
 
Hiyo ya kuandaa mazingira umenikumbusha miaka ya nyuma bush niliwahi kuishi na granny yangu mmoja alikuwa anauguza mjomba wangu.

Huyo mjomba alikuwa anaumwa sana na alikuwa anauguzwa na huyo kikongwe.

Siku mgonjwa anafariki yule bibi akabana mlango na kufuli akaenda chaka kichimba udongo wa kusiliba ndani ili kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya watu wataokuja kulia msiba.

Majirani ambao walikuwa wanajua kuna mgonjwa pale walikuwa wanakawaida ya kuja kumuona kila siku.

Sasa siku hiyo wanashangaa wamefika home wanakuta mlango umepigwa kufuli.

Wakawa wanajiuliza kwa namna ambavyo walimuacha jana mgonjwa alikuwa ni mtu wa kumuangalia kila muda sa imekuwaje leo pafungwe au kapelekwa hospitali na kumbuka muuguzi ni bibi kizee ambaye asingeweza kumtoa kumpeleka hospitali bila assist ya majirani

Majirani wakaondoka, walivyorudi baadaye wakamkuta kikongwe ana malizia kusiliba sakafu. Wakaingia moja kwa moja ndanj kumuona mgonjwa lakini walivyomcheki wakagundua alikuwa amekufa kitambo sana maana mwili ulikuwa ushapoa kabisa.

Bibi alijikausha na kuanza kulia as if ni taarifa ngeni iliyo msuprise, hicho kilio kiliwaita na majirani wengine ukawa msiba rasmi.

Mwisho nakumbuka waombolezaji wa msiba walikaa kwenye sakafu ambayo ina ubichi bichi kutokana na udongo aliokuwa anasiliba haukukauka vizuri.
 
Kuhusu kutokutoa taarifa hadi marehemu awekwe vizuri ni jambo la maana sana. Sema Sio rahisi sana kwa wenye hisia kali kutokupiga kelele za kilio labda kwa wenye ukomavu sana.
Kikubwa jaman tujifunzeni kusafisha nyumba zetu mda wote tusisubiri hadi matatizo yafike.
Mfano kila week mara moja unaweza kuwa unasogeza vitu kama viti na vitanda ili kudeki sehemu ambazo hazifikiki kwa urahisi...
Pia utaratibu wa kulima majani yanayozunguka nyumba pamoja na kufyeka mapori.
Ukiwa na utamaduni huu siku ya matatizo watu hawawezi kukukuta na aibu ndogo ndogo kama hizi.

Ni kweli kabisa usafi wa nyumba zetu uwe Mara kwa Mara ili kuondoa aibu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom