Ukiongezea haya Valentine yako itanawiri sana

CPU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
3,863
687
Ndugu zangu wa JF, sina shaka mtakuwa wazima wa afya njema na mipango inaendelea vyema.

Kabla sijaanza topic hii, napenda kuwapongeza wale wote walioweza kudumisha mahusiano yao mpaka wakati huu. Pia napenda kuwasihi walio ktk mifarakano wajaribu kukaa chini kuongea pamoja kujadili na kutatua matatizo yaliyowasibu, kwani mtu yeyote mwerevu mwenye upeo mzuri wa kufikiri atakubali ya kwamba hajui kila kitu.

Na kwa wale walioanza mahusiano basi nawasihi washikamane na wawe wamoja, wajifunze kuvumiliana ktk shida na wafurahi pamoja ktk raha


aacouplevalentinesday.jpg

Kwa kuanza tu ni kwamba kimsingi hakuna kitu kipya katika Sikukuu ya Wapendanao, watu karibu wote watazungumzia juu ya mavazi, zawadi, ‘outing’ na mengine, lakini hapa kuna kitu cha zaidi cha kujifunza na mengine mengi mnaweza kuongezea.
Tujionee...


Vipi kuhusu zawadi?

(i) Kwa wanawake

Zipo zawadi nyingi sana ambazo wanawake wanapenda kupewa katika siku hii lakini zilizo bora zaidi ninazopendekeza ni pamoja na mkufu, maua, nguo za ndani, hereni au kitu chochote ambacho kinahusiana na kazi zake.

Mathalani anafanya kazi inayotumia sana kalamu, basi unaweza kumnunulia kalamu nzuri ya thamani ambayo itakuwa ya kipekee sana kwake.

Wanawake wanapenda rangi tulivu sana, nunua maua yenye rangi ya pinki, damu ya mzee, limau, hudhurungi, nyeupe na nyingine zinazofanana na hizo.

Wanaume wengi wanapenda kuwanunulia wapenzi wao zawadi zenye rangi nyekundu lakini utafiti unaonesha kwamba asilimia 70 ya wanawake wanaotumiwa rangi hiyo hawazifurahii badala yake wanapenda rangi zilizopoa.


(ii) Kwa wanaume

Hawa rangi yao ni nyekundu au maziwa, ukimnunulia mwanaume mkanda, saa, nguo za ndani, shati, tai, vifungo maalum vya shati na soksi utakuwa umempatia sana! Kwa nini? Kwa sababu ni kati ya vitu muhimu ambayo huvitumia mara nyingi zaidi katika siku yake.

Asipovaa mkanda uliomnunulia, basi atavaa tai, saa, vifungo au soksi. Kwa bahati nzuri, vitu hivi huviona kila wakati hivyo huzidisha mapenzi yake kwako kila anapoona zawadi zako.

Wanaume wanapenda sana kadi, manukato na maua lakini kama nilivyosema hapo juu, nakshi kubwa zaidi ni rangi nyekundu.

Kama umeamua kumnunulia mwanaume wako kadi, basi hakikisha maneno yaliyoandikwa ni ya kumsifia zaidi kwa jinsi anavyokufanya uwe mwanamke bora. Msifie kwamba, yeye anaweza kukufanya ukajiona mwanamke hasa hata unapokuwa barabarani.

Kwamba yeye ni mwanamke bora maana yupo na mwanaume wa shoka!
Teh teh teh . .
Mmenipata?


ONESHA TOFAUTI

Siyo lazima mtoke ‘out’, hata kama mkiamua kutoka, itakuwa vizuri zaidi mkienda katika maonesho tulivu (ya kistaarabu zaidi), nikimaanisha kuanzia wanamuziki wenyewe au hata aina ya mtindo wanaotumia.

Ufukweni si mahali pazuri sana, maana mara nyingi katika siku kama hizi, wengi hupenda kwenda huko hivyo hamtapata utulivu ambao mnaoutarajia.

Kumbuka siku yenyewe imeangukia Jumatatu, kwa maana hiyo wengi watakuwa kazini hadi jioni, hivyo kutoka makazini na uchovu halafu kwenda tena kwenye kelele hakutakuweka sawa kihisia. Ingekuwa siku ya kipekee zaidi kwako, kama mtaamua kujifungia chumbani mkipanga mambo ya mapenzi yenu.

Chumba kiwe na nakshi za kimahaba, puliza manukato ya kuvutia, tandika mashuka ya rangi za kimapenzi na mwanga uwe hafifu. Itakuwa nzuri zaidi kama mtatumia mwanga wa mshumaa pekee. Muziki laini utawale chumbani na muitumie siku hiyo kuzungumza namna ya kuboresha zaidi penzi lenu.


Mambo muhimu ya kuzingatia...


1. Hutakiwi kukasirika kwa sababu hata kama amekukosea au amechelewa ‘appointment’, usizungumzie kabisa suala hilo, kwani linaweza kuharibu siku yenu.

2. Msifie mara nyingi uwezavyo, mwambie kwamba yeye ni bora kwako na hujutii kuwa naye.

3. Tengeneza picha nzuri ambayo anaipenda aliyokupatia au mliyopiga pamoja katika ‘frem’ halafu buni maneno matamu ambayo yatasomeka pembeni mwa picha hiyo, kisha umpe. Maneno hayo yawe matamu yenye kumsifia.

Mathalani unaweza kuandika; Najivunia kuwa nawe, Nina bahati sana kukupata, Mtanashati wangu, Mrembo wangu, Malkia wangu, Mwanamke wa maisha yangu n.k.

Maneno haya unaweza kuyatafsiri na kuyaandika kwa lugha ya Kiingereza au Kifaransa (kama anaelewa na kupenda lugha hizo).

4. Mfanyie ‘massage’ ya kimahaba mkiwa chumbani, hapa siwezi kueleza zaidi lakini kama hufahamu namna massage inavyofanyika na unataka kujua, wasiliana na mimi nitakuelekeza zaidi.

5. Tengeneza uchokozi wa hapa na pale, kuhakikisha anakuwa mwenye tabasamu muda wote utakaokuwa naye.


MFANYIE ‘SURPRISE’
Kama ulikuwa na jambo ulilotaka kumfanyia mpenzi wako kwa muda mrefu, ingekuwa vizuri zaidi kama ungemfanyia katika siku hii ya wapendanao kwa kumshtukiza!

Inawezekana ulikuwa na mpango wa kumvalisha pete, kwenda kujitambulisha kwao au kupeleka barua ya posa!

Kama ukifanya hayo katika siku hii ya wapendanao, utalifanya penzi lenu kuwa la kihistoria kwani kila inapofika siku kama hiyo, mtakuwa mna kitu kikubwa cha kukumbuka katika penzi lenu.


ZAWADI YANGU KWENU!


Marafiki zangu JF nawapenda sana, hapa nimeamua kuwapa zawadi ya Valentine, unajua nini? Ni ‘Love Messages’ bomba ambazo utazitumia kwa ajili ya kumpa raha mpenzi wako siku hiyo.

(i) Natafakari zawadi nyingine ya kukupa mpenzi wangu lakini sijapata zaidi ya kukuambia mimi ni mali yako milele!

(ii) Joto lako ndiyo tiba yangu ya kweli, napenda sana kuwa karibu nawe laazizi...fanya kazi lakini jioni usinitoroke dear...Happy Valentine’s Day!

(iii) Siogopi kusalitiwa mpenzi wangu lakini naogopa kusalitiwa na wewe kwa kuwa unaishi ndani ya nafsi yangu siku zote!

(iv) Kukupenda ni wimbo ambao nimeuimba siku zote lakini leo nakupa chorus yake...sitakuacha milele...Happy Valentine’s Day!

(v) Zawadi zote nilizokupa, ipo moja muhimu ambayo bado sijakupa, nikuambie kitu darling...leo ni siku ambayo utaifurahia zaidi katika siku zote ulizowahi kuwa na mimi kimapenzi. Mwaaa....

Kwa sasa niishie hapa, ila tunaweza kuongezea mengine mengi mazuri

 
Nieleze basii zaidi juu ya hili chini

Mfanyie ‘massage' ya kimahaba mkiwa chumbani, hapa siwezi kueleza zaidi lakini kama hufahamu namna massage inavyofanyika na unataka kujua, wasiliana na mimi nitakuelekeza zaidi.
 
Nieleze basii zaidi juu ya hili chini

Mfanyie ‘massage' ya kimahaba mkiwa chumbani, hapa siwezi kueleza zaidi lakini kama hufahamu namna massage inavyofanyika na unataka kujua, wasiliana na mimi nitakuelekeza zaidi.

Mkuu una mpenzi au umeoa???
 
Shukran sana kwa msaada wa nguvu. Je na wale walio single lakini wana wapenzi waume za watu wengine utawasaidije?
 
Shukran sana kwa msaada wa nguvu. Je na wale walio single lakini wana wapenzi waume za watu wengine utawasaidije?

Mkuu njanjamimi, hao watu msaada wangu kwao ni ONYO
Waache kabisa kujimilikisha mali za watu, watafute wenzao walio singo watengeneze penzi lao HALALI
 
Safi sana kwa kutuongezea maujuzi maana wengine tunasherehe mbili siku hiyo. Birthday na Valentine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom