Ukiona wachambuzi maandazi kwenye page zao wamenyamaza ujue Yanga wana hali ngumu

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,634
7,006
Kwa kawaida kama kuna tatizo lolote lililofanywa na yanga,hutaona kabisa kwenye uchambuzi wa suala kama hilo kwenye page zao ama vipindi vyao.
Sana sana utasikia lawama za jumla jumla tu ooh hizi timu za Simba na Yanga zinafanya ubabaishaji!Ukisikia hivyo ujue ni Yanga ndio wana matatizo hapo.

Kama Simba angekuwa hayuko sahihi kwenye sakata la Morrison, ungesikia maneno ya shobo meengi sana kutoka kwa wachambuzi hawa maandazi.Wengi wao wakiwa clouds.Hata huwa hawafikiri kwa mantiki.

Kitendo cha Senzo kwenda yanga na kushabikiwa kama vile yanga wamesajili binge la striker,ni ishara ya upungufu mkubwa wa uelewa na kuonesha kuwa hakuna mtanzania mwenye akili na uwezo wa kuleta mapinduzi katika mpira.Wanasahau kuwa Senzo ameyakuta mafanikio na hajavuka kiwango cha mafanikio aliyoyakuta.

Kwenye sakata la Morrison yanga walishindwaje kupeleka waraka wa mkataba?Hadi kikao kiahirishwe? TFF hawana huo mkataba,Yanga hana huo mkataba ndio maana hajapeleka, TFF inataka Morrison apeleke mkataba upi ambao ninyi wahusika hamna?
 
Kuna ukweli sana. media za bongo zinaibeba sana yanga na kuwaogopa GSM wanaivuruga yanga
 
Wachambuzi ni watu waliosomea kazi zao na wanafanya mambo kwa weledi siyo kwa kufuata mapenzi yao kwa hizi timu .

Hili suala la Morison kuna kamati inalishughulikia na itatoa maamuzi yake leo saa saba baada ya kuwa imepata vielelezo vyote, wewe ulitaka ihukumu tu bila kuwapa mlalamikaji na mlalamikiwa muda wa kujitetea na kuleta vielelezo vyote, hii siyo sawa.

Haya suala la wachambuzi kukaa kimya bila kuchambua linawezaje kuwa na uhusiano na Yanga na siyo Morison au hii kesi unaihusishaje na upande wa timu yako ambayo kiuhalisia haina malalamiko huko kwenye kamati.
 
Kwani TFF kuna kesi ya Yanga vs Simba? Nilidhani ni kati ya Morrison na Yanga!!
 
Yanga anaweza kubumba waraka wa Mkataba wakati mchezo umeshabumburuka? sijui leo atapeleka kitu gani na akibumba basi ajue ameikaribisha FIFA kusaidia kufumua pale Jangwani na TFF
 
Yanga anaweza kubumba waraka wa Mkataba wakati mchezo umeshabumburuka? sijui leo atapeleka kitu gani na akibumba basi ajue ameikaribisha FIFA kusaidia kufumua pale Jangwani na TFF
Unaanza kujitekenya subiri maamuzi ya kamati wewe umejuaje kama Yanga imebumba mkataba wakati maamuzi hayajatolewa acha uzandiki.
 
Pelekeni mkataba halali na mkipeleka kitu feki basi Segerea yao na kufungiwa juu
Yeyote atakaye kutwa amehusika kufanya uhalifu anastahili haki yake kwa mujibu wa sheria. Masuala ya mihemuko na shangwe zote mwisho ni saa saba mchana wa Leo.
 
Sasa hivi mtibwa wanalalamika kuhusu yanga walivyomsajili beki wao, azam pia wamelalamika kuhusu yanga kumshawishi sure boy aombe kuondoka azam sasa sijui Senzo ndio kaenda kwenye watu weledi au vp halafu huyo mwenyekiti wa kamati ni yanga lialia na aligombea uchaguzi akashindwa na huko mbeya pia ameshindwa kwenye uchaguzi pamoja na kuwa mgombea pekee anatafuta njia ya kuibeba upotolo
 
Wachambuzi ni watu waliosomea kazi zao na wanafanya mambo kwa weledi siyo kwa kufuata mapenzi yao kwa hizi timu .

Hili suala la Morison kuna kamati inalishughulikia na itatoa maamuzi yake leo saa saba baada ya kuwa imepata vielelezo vyote, wewe ulitaka ihukumu tu bila kuwapa mlalamikaji na mlalamikiwa muda wa kujitetea na kuleta vielelezo vyote, hii siyo sawa.

Haya suala la wachambuzi kukaa kimya bila kuchambua linawezaje kuwa na uhusiano na Yanga na siyo Morison au hii kesi unaihusishaje na upande wa timu yako ambayo kiuhalisia haina malalamiko huko kwenye kamati.
saa sana tayari bado wako kimya
 
Back
Top Bottom