Ukinzani ndani mwako

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,704
Ni muhimu sana ujitambue ili uondoe ukinzani ndani mwako. Uache kutamani hiki, lakini nje una-manifest kingine. Siyo unatamani kazi, lakini nje unazizuia zisije. Au unavuta usizozitaka, na hata zikija unazozitaka hazidumu (unafanya self sabotage)...

Harmony within... inatokea pale ambapo maisha yako yako totally aligned with the "WILL OF THY SELF"... Hiki ndicho tunachohitaji. (Mapenzi yake yatimizwe hapa duniani kama ilivyo mbinguni) Swali ni je utajuaje roho yako inachotaka? Rohol yako inataka ku-experience nini? Utaisikiaje sauti yako ya ndani kama muda wote unachosikiliza ni kelele za akili yako pekee?

Ni muhimu kutambua kila ukinzani... however small!.. Kuona mawazo, hisia, na kawaida /matendo.. Je kuna mahali zinapingana? Tazama kama zinapingana na unachokitaka deep inside yourself...

Ninaposema "however small"... ninamaanisha very very subtle kiasi kwamba siyo rahisi kujua.. Mfano:

1: Je wewe unapenda sana vitu vya bei rahisi, kiasi kwamba unawekeza nguvu nyingi kulia bei mpaka ishuke sana... lakini binafsi unatamani au unapanga kufanya biashara na kupata faida?

Je wewe unatamani au tayari unafanya biashara lakini tabia zao kwenye biashara za watu wengine ni za kuua biashara? Yani siyo za kusaidia bishara ya mtu mwingine ipate faida? Mfano unakwepa kulipa nauli, ukizidishiwa change hurudishi? Au unazunguka kutafuta mwenye shida alielazimika kuuza bidhaa yake kwa bei ndogo kupita kiasi... yani umlalie? Je wewe unapenda vitu pirated online? Mfano movies, vitabu, muziki n.k vilivyoibiwa na kuuzwa kinyume na matakwa ya hati miliki..? Yani upo tayari mhusika akose mapato?... Je unapenda kununua vitu vilivyoibiwa na kisha kuuzwa kwa bei ndogo?

Je wewe ni muajiriwa usiyefanya kazi kwa bidii ili muajiri wako afanikiwe? Je unadokoa vitu vya muajiri? Mfano kutumia muda wa kazi vibaya, kuiba vifaa vya kazini na kuvipeleka nyumbani, kutumia gari na mafuta vibaya, kutoa risiti za uongo n.k?... Halafu unatamani kuwa na biashara kubwa itakayoajiri wafanyakazi waaminifu?

2: Je unatabia ya kukashifu au kuhukumu vitu fulani hadharani lakini deep inside unavipenda au unavifanya kwa kificho?

N.k
Concept nzima ya kuacha dhambi, kuambiwa tusihukumu, na kuwafanyia wengie yale tu tunayotaka tufanyiwe... kunalenga kutuepusha na contradictions za ndani zitakazokuondolea harmony... na siyo kwaajili ya kutuepusha na jehanamu..

Fahamu mawazo, maneno na matendo yako, ili yasipingane na mkataba wa nafsi yako.

3: Je kwenye mawazo na matendo yako unatafuta pesa au unatafuta kile ambacho pesa inahitajika ili kifanyike? (Naomba mlifikirie hili vizuri)... Unapopanga mipango yako ya maisha... unakuwa unatafuta nini hasa?? unatafuta pesa? Gari, nyumba, ada, chakula?... Au unatafuta uwezo wa kusafiri kwa urahisi, makazi, elimu ya watoto na lishe??.. Hivi ni vitu tofauti kabisa. Unaiomba nini universe? Je unataka mkate wa kila siku, au pesa za kununulia chakula?..
 
Umeuliza maswali meeeengi, je ni kwamba wewe ni muhanga ndio unataka majibu au?
Bado hujaeleweka
 
Back
Top Bottom