Ukinyonga na unafiki wa Sitta na Mwakyembe wadhihirika

Ukinyonga na unafiki wa Sitta na Mwakyembe wadhihirika

Waombee adui zako waishi miaka mingi ili wanapobarikiwa wajionee kwa Macho,

Lowassa MTU Wa watu chaguo la watu,Tuliudhunika pamoja na Tutafirahi pamoja.
 
Tangu sitta asimamie hii katiba haramu ya chenge,nimemdharau.

Sitta ni mwanasiasa wa kuogopwa kama ukoma kwani ni mnafili, mlafi na pia fisadi!! Mpaka hivi leo bado ameng'ang'ania kukaa nyumba aliyokuwa amepangiwa kama spika wa bunge ili hali hadhi hiyo hanayo tena huku kodi zetu zikitumika kulipia pango hilo la gharama kubwa sana!!

Mkewe pia alikwisha kamatwa akitoa rushwa wakati wa kura za maoni za lakini mambo yakazimwa zimwa kienyeji huku mumewe akitumia fedha nyingi kujenga ofisi ya mbunge ya Urambo kinyume cha taratibu. Juu ya hayo yote mkitaka kujua ufisadi wa hii familia nendeni sehemu iitwayo BASI HAYA kule BOKO mkaone majumba yaliyoporomoshwa na hawa wezi wa mali za umma!!! Sitta hana moral authority ya kumyooshea kidole mtu mwingine yeyote kwani yeye ni mchafu sana.
 
Waombee adui zako waishi miaka mingi ili wanapobarikiwa wajionee kwa Macho,

Lowassa MTU Wa watu chaguo la watu,Tuliudhunika pamoja na Tutafirahi pamoja.


Wananchi wengi wanaompigia debe Lowassa kuwa Rais , wanafikiria kuwa kwa kufanya hivyo wanamshabikia Lowassa peke yake kumbe ujinga wao ndio unavyowapumbaza!!! Hawa wapambe wa Lowassa ni wafanyabiashara wengi wa kihindi na waafrika ambao wamewekeza fedha zao kwa huyu bwana kuingia Ikulu na mara akiingia Magogoni waanze kurudisha fedha walizowekeza kwa njia ile ile iliyoiumiza nchi yetu kwa miaka kumi ya utawala wa huyu mkweree!! Mfumo anaoutumia Lowassa ili kupata uongozi wa nchi ni ule ule alioutumia huyu anayemaliza muda wake hivyo usitegee mabadiliko kama Lowassa ndio atakuwa mrithi wake; wauza UNGA NA MAJANGILI wataendelea kupeta na wakina ROSTAM na wakina Serukamba ndio watakaokuwa watawala wa nchi!! Unapomshabikia Lowassa kumbuka kuwa unashabikia mfumo wa kufisadi chi!!
 
[h=2]Mwakyembe atajwa kashfa TRL.[/h]


Na Waandishi wetu



9th March 2015










Mwakyembe-09March2015.jpg

Waziri wa uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.


Kuna kila dalili kwamba uhamisho wa Waziri Dk. Harrison Mwakyembe kutoka Wizara ya Uchukuzi kwenda Afrika Mashariki, akibadilishana nafasi na Samuel Sitta, ni sehemu ya kumwepusha na kadhia ya kashfa ya mabehewa feki ambayo hadi sasa imegundulika kuwa ni kashfa nyingine inayoitafuna Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).

Uchunguzi huru umegundua kuwa hatua ambazo zilianza kuchukuliwa na Sitta katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA), nako TRL zimeanza kutikisa baada ya kubainika kwamba mabehewa ambayo yaliingizwa nchini kutoka China na kupokelewa na Dk. Mwakyembe kwa mbwembwe zote kisha kubainika hayana viwango, wakubwa wa kampuni hiyo walijua hilo, lakini wakafunika kombe kwa kuwa wakubwa walipeana zabuni kwa njia ya kujuana.

Habari zinasema kamati iliyoundwa na Sitta kuchunguza kashfa ya uingizaji mabehewa hayo kutoka India, tayari imeibua mambo mazito ambayo yanaongeza orodha ya kashfa za ulaji na ufujaji wa fedha za umma uliosimamiwa na baadhi ya viongozi wa serikali wakitumia madaraka yao vibaya.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka TRL, uingizaji wa mabehewa hayo ulifanywa na Kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ya India kwa kushirikiana na mfanyabiashara mmoja nchini ambaye kwa miaka mingi amehusika katika kadhia nyingi za kujipatia fedha kwa mikataba laghai dhidi ya serikali na mashirika yake.

Vyanzo vyetu ndani ya TRL vinasema kuwa kamati iliyoundwa kuchunguza kashfa hiyo ya ufisadi wa mabilioni ya fedha, inatarajia kukamilisha taarifa yake ya uchunguzi hivi karibuni na kuikabidhi kwa Waziri Sitta, lakini tayari imegundua madudu mengi ikiwamo wakubwa kupokea mabehewa yenye hitilafu wakati wakijua.

Waziri Sitta amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumzia jambo lolote hadi atakapokabidhiwa ripoti ya uchunguzi.

“Suala la mabehewa feki nimelikuta na kuna tume (kamati) iliundwa kuchunguza na inatarajia kukamilisha ripoti yake hivi karibini, nadhani kwa sasa tungevuta subira ila niwahakikishie wananchi sitaogopa kuchukua hatua bila kujali kashfa hiyo inamhusu mtu au kiongozi wa namna gani,” alisema. Kashfa ya uingizaji wa mabewa feki iligundulika mwishoni mwa mwaka jana, ikidaiwa kuwa kuna ufisadi mkubwa umefanyika ndani ya TRL katika utoaji wa zabuni ya ununuzi wa mabehewa mapya.

Baadhi ya mafundi wa TRL wanasema kuwa mabehewa hayo ni mabovu na hayaendani na vipimo vya reli ya kati.

Udhaifu wa mabehewa hayo uligundulika baada ya kufanyiwa majaribio, kufuatia mengi ya yale mapya 25 aliyopokea Dk. Mwakyembe kupata ajali katika mazingira ya kutatanisha, huku ikidaiwa kuwa hayana ‘stability’ yakiwa juu ya reli.

“Unajua hata yale ya mizigo mengi yalianguka sana. Sasa ikaonekana hebu na haya ya abiria yachekiwe vizuri, nakuambia matokeo yake ni balaa kama yangeachwa kusafirisha abiria. Ingekuwa ni kilio nchi nzima,” alisema mtaalam mmoja wa masuala ya reli kwa sharti la kutokutajwa jina gazetini.

Mabehewa hayo tangu yapokelewe takribani miezi tisa sasa, hayajawahi kusafirisha abiria.

Mtaalam huyo aliongeza kuwa kilichofanyika ni uongozi wa TRL wakishirikiana na wakubwa wizarani kuengua jopo la mafundi wa TRL na kuingiza mabehewa hayo kwa kuwa tayari wakubwa walikuwa na mtu wao katika tenda hiyo.

Dk. Mwakyembe alizindua mabehewa mapya 25 ya kubebea kokoto aina ya ‘Ballist Hopper Bogie’ (BHB), kutoka kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited yenye thamani ya Sh. bilioni 4.316 kwa ajili ya uimarishaji wa Reli ya Kati.

Upokeaji wa mabehewa ya mizigo ulifuatiwa na tukio jingi la kushuhudia upokeaji wa mabehewa mengine ya abiria Julai 24, mwaka jana Dk. Mwakyembe akiwa mmoja wa mashuhuda.

Alipoulizwa na NIPASHE kwa njia ya simu jana kuhusiana na kashfa ya mabehewa feki TRL, Mwakyembe alisema: "Hivi sasa niko nje ya nchi... vyombo vya habari vimesharipoti sana suala hili. Watu tayari walishachukuliwa hatua, inawezekana wewe (mwandishi) hujui, wenzako wameandika sana kuhusu suala hili, na watu walishachukuliwa hatua."

Katika hafla ya upokeaji na ushushaji wa mabehewa hayo katika Bandari ya Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alisema ununuzi wake ni sehemu ya utekelezaji wa makakati wa ‘Matokeo Makubwa Sasa’ (BRN), ambao umelenga kuhakikisha usafirishaji wa reli unaimarika kwa ajili ya kuhimili usafirishaji wa abiria na mizigo, hivyo kusaidia utunzaji wa barabara za lami zinazojengwa kila kona nchini kwa sasa.

Vyanzo vya habari kutoka TRL vinasema kuwa uhamisho wa Dk. Mwakyembe kutoka Uchukuzi, ni mkakati wa kumwepusha na kadhia yoyote ambayo inaweza kulipuka wakati wowote kutokana na zabuni hiyo ambayo inaonekana kama aina nyingine wa wizi wa wazi.

Mbali na Dk. Mwakyembe, menejimenti ya TRL nayo iko kikaangoni tangu Sitta aunde kamati ya kuchunguza kashfa hiyo.



CHANZO: NIPASHE
 
Tangu sitta asimamie hii katiba haramu ya chenge,nimemdharau.

Sita ni mwizi na Fisadi Hatari ingawa pesa Nyingi inapotelea kwenye Michepuko maana anapenda wanawake hakuna Mfano. Hivi sasa Wamiliki wa magari makubwa ya usafirishaji wa Abria na Mizigo hawana Hamu na Sita kwani kila siku anawaita Ofisini kwake mmoja baada ya mwingine kuwapiga Mizinga kisha amewahidi kama wa hataijenga Reli kwa hataka ili kuwaokoa kibiashara, Sita ni Hatari sana ana Tamaa ya pesa na hapo hapo ana Roho mbaya na wivu mkubwa.
 
Pata pesa/madaraka ili tuijue tabia yako. Huyo wa sasa ndie Sitta halisi. Aliyoyafanya kwenye mchakato wa katiba mpya kama spika hata siyasemei hapa. Ila kiukweli, mimi binafsi, cna hamu nae tena huyu mzee!!

Sita ni Balaa, hapo alipo Bado anaona kama hapamtoshi yeye kilio chake ilikuwa Wizara ya Fedha au wizara ya Nishati na Madini ambapo unapiga pesa kwa kasi kubwa kuliko wizara zingine.
 
Tangu sitta asimamie hii katiba haramu ya chenge,nimemdharau.

Sita ni mwizi na Fisadi Hatari ingawa pesa Nyingi inapotelea kwenye Michepuko maana anapenda wanawake hakuna Mfano. Hivi sasa Wamiliki wa magari makubwa ya usafirishaji wa Abria na Mizigo hawana Hamu na Sita kwani kila siku anawaita Ofisini kwake mmoja baada ya mwingine kuwapiga Mizinga kisha amewahidi kama wa hataijenga Reli kwa hataka ili kuwaokoa kibiashara, Sita ni Hatari sana ana Tamaa ya pesa na hapo hapo ana Roho mbaya na wivu mkubwa.
 
Dr.Harrison Mwakyembe atakumbukwa na taifa kama msomi aliyeshindwa kusimamia alichojifunza pale aliposhindwa kueleza maoni yake BMK kuhusiana na Serikali ya Shirikisho ambayo aliandika kitabu kuhusu na kuweza kutunikiwa udaktari. Watu wamekuwa wanafiki wa nafsi zao wenyewe, nafsi yake inajua na elimu aliyopata na kuamini inamwambia vile lakini amekubali kuenenda kama walivyoagizwa na Lukuvi, Wassira.

Samweli Sitta mnafiki na ndumila kuwili asiye na haya wala kujiuliza msimamo wake wa maisha na kisiasa. Ni kweli katika siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu lakini Sitta amekubuhu katika kuwatumia watu.
Awali aliwatumia wabunge wa upinzani na makada wa ccm wasiompenda JK akiwa spika, baadae alivyobanwa na kuhofia kuuawa sambamba na Dr.Mwakyembe.

Alipita makanisani ili aonewe huruma lakini katika BMK aliwadhalilisha maaskofu. Kimsingi watanzania tulikuwa na imani kubwa na Samwel Sitta tukiamini MZALENDO kumbe yupo kwa maslahi yake. SItta ni aina ya mtu anayeweza kupambana mkaamini mwezenu na kesho akipata fursa anatetea na kuimarisha upande aliopinga awali.

NI USHETANI
Labda ni wewe tu ulimwamini sitta! hakika nakwambia kama sitta asingekuwa mnafiki na shetani ccm wasingemchagua kuwa spika katika bunge la katiba! ushetani wake hakuanza leo, shetani ni shetani tu kwa asili hata alipokuwa malaika bado ndani ya roho yake alisha kuwa na ushetani!
 
MUNGU azidi kuyaweka yaliyofichika peupeeee uhakika Lowasa NI chaguo La Mungu kwa watanzania hivyo bac tunaona jinsi anavyompigania adui zake wanaokuja kwa Njia moja Mungu anawasambaratisha kwa Njia saba tofauti tofauti yani wapinzani wa lowasa kweli Mungu anawashuhulikia hasa.... Lowasa oyeeeeeeee

ni laana kubwa kumchanganya lowasa na Mungu,,,,,taja lingine
 
MUNGU azidi kuyaweka yaliyofichika peupeeee uhakika Lowasa NI chaguo La Mungu kwa watanzania hivyo bac tunaona jinsi anavyompigania adui zake wanaokuja kwa Njia moja Mungu anawasambaratisha kwa Njia saba tofauti tofauti yani wapinzani wa lowasa kweli Mungu anawashuhulikia hasa.... Lowasa oyeeeeeeee

Unamzungumzia Mungu yupi mkuu?! Kama ni huyu wa mbinguni hapana mungu hamteui mtu mwenye hata chembe ya doa ...
 
Back
Top Bottom