Ukinyimwa bonus kazini unaichukuliaje hali hiyo?

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Ukinyimwa bonus au ukipewa bonus kidogo kazini kwenu (kama umeajiriwa), au kama iliwahi kukutokea uliichukuliaje hali hiyo? La pili, siku nilipolipa kodi ya pango pale Kibangu Dsm ya mwaka mzima ndio siku niliyokwenda kutafuta kiwanja ili nijenge kibanda. Ilikuwa hivi, nilimpa baba mwenye nyumba kodi ile halafu nikasema asante kwa kupokea malipo yangu kwake. Nikaingia ktk chumba kile nikakiangalia na kufikiri sana. Dawa ikawa ni kutafuta kiwanja na kujenga room moja nihamie kiugumu.

Nipeni uzoefu wenu ktk haya mambo mawili kama yamewahi kukutokea, na nini ulijifunza kwa matukio hayo kama mjasiriamali?
 
mimi nilianza kufikiria kuacha kazi pale nilipopewa bonasi kidogo! na naamini kwa hatua nilizoanza kuchukua Mungu atanisaidia nitaachana na hizi shughuli za kukadiriwa nipewe ngapi bila hata ya kutumia formula ambayo ipo based on performance of somebody.
 
Inamaana mnaopewa bonus hao wanaowapa huwa hakuna target zozote? Na bonus zinatolewa bila evaluation? Huwa hamuambiwi umefanyaje kipindi cha mwaka mzima? Halafu ukisema ndogo unamaanisha na nini? Maana kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kulalamika yeye anapewa mshahara mdogo lakini anafanya kazi kuliko Mkurugenzi. Pia nafasi zenu kazini zikoje? Yaani vyeo?
 
Back
Top Bottom