Ukinizingua Nakuzingua!

Ukinizingua Nakuzingua!

Ertugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
13,375
Reaction score
26,873
Mheshimiwa Rais wangu.

Pole na majukumu ya kazi yako ya uraisi,na pole Kwa lawama ambazo zinaelekezwa kwako hata pale ambapo makosa hayo yamefanywa na wasaidizi wako.

Mheshimiwa Rais natamani Ile kauli yako ya "ukinizingua nitakuzingua" iendelee kusikika tena na tena kwani watanzania Bila kuzinguliwa huwa hawafanyi kazi,Bila kuonyesha ukali huwa hawajitumi,Bila kufokewa wanaleta mazoea.

Mheshimiwa Rais mara baada ya kuchukua madaraka ya uraisi wasaidizi wako walikuwa bado na Ile hofu ya mtangulizi wako na Ile kauli yako kazi iendelee ikiambatana na "ukinizingua nitakuzingua" iliwafanya watendaji wako wakuogope na kuwajibika kwasababu walijua kabisa huna mswalie Mtume. Na wengine walienda mbali kabisa na kusema "mama hatabiriki" Kwa maana lolote linaweza kutokea. Hayo na mengine mengi yalifanya uonekane ni Raisi ambaye upo tayar kuchukua maamuzi magumu na hutaki kumuangalia mtu machoni,na hayo ndio mambo ambayo yanawafanya watanzania wawajibike ipasavyo.

Mheshimiwa Rais wewe umesomea Uongozi,na katika Uongozi wakati mwingine unatakiwa uwe mkali kama chui na wakati mwingine uwe mpole,lakini hayo yote yatategemeana na utashi wa wale unao waongoza,Kwa mazingira ya Tanzania kuwa mkali ndio best choice kwakuwa ndio tunavyopenda hivyo kwani Bila kushurutishwa huwa tunafanya mambo kimazoea.

Katika Uongozi pia kuna theories mbali mbali lakini moja wapo ni theory X na theory y

Theory X inazungumzia wale watu ambao wanajituma kufanya majukumu yako Bila kusimamiwa ,hawa hawahitaji kusimamiwa au kuambiwa nini cha kufanya,mara zote huwa ni wachapakazi hodari Sana,na watu hawa ukiwasimamia unashusha morali Yao ya kazi,watu hawa wanahitaji motisha kidogo na kazi inaendelea Kwa asilimia Mia mbili, lakini bahati mbaya Sana hawa watu wapo wachache sana ukilinganisha na watu wa theory y.

Watu wa theory y ni watu ambao hawajitumi,wanapenda kusimamiwa na kushurutishwa,hawa kama boss akiondoka Tu ofisini nao wanawacha kuwajibika na kutegea kufanya kazi,hawa wanahitaji uwe mkali zaidi ndio utaenda nao Sawa,hawa hawahitaji kuambiwa kauli kama " kila mtu ale na urefu WA kamba yake" kwani Kwa kufanya hivyo ndio unakuwa umewapa tiketi ya kufanya ubadhirifu na ufisadi WA kiwango cha mwendo Kasi.

Hawa si watu wa kuwaambia "alikuwepo Simba wa Yuda ambaye kila mtu alimuogopa". Hawa ni watu ambao wanatakiwa waone kauli yako na matendo yako yanasadifu malengo yako na matakwa yako ili inchi yetu isonge mbele.

Nina mengi ya kusema lakini kwa Leo naomba niishie hapa najua Una majukumu mengi ya kitaifa, panapo majaliwa nitateta na wewe tena.

Kwa heshima na taadhima naomba kuwasilisha.

Ni hayo tu.
 
Kauli iyo inafanya kazi kwa sukuma gang tu sidhani ni kwa wengine.
 
Kauli iyo inafanya kazi kwa sukuma gang tu sidhani ni kwa wengine.
Naweza kuwa ni mshamba Kwa hili, huwa nasikiaga Tu sukuma gang lkn sijui huwa akina nani haswa.

Naomba unifungulie code tafadhali.
 
Kwa hiyo utetezi hapa bado ni ule ule...anaangushwa na anaowateua na katika msingi huo lawama zielekezwe kwa anaowateua na si kwa yeye mteuzi. Na wako watu na akili zao wataunga mkono utetezi wa hovyo kama huu. Masikini Tanzania.
 
Naweza kuwa ni mshamba Kwa hili,huwa nasikiaga Tu sukuma gang lkn sijui huwa Akina Nani haswa

Naomba unifungulie code tafadhali
Inavyosemekana eti na wale waliokuwa Supportive and Loyal kwa hayati JPM (RIP) Wengi wao wa kutoka kanda ya ziwa na ndiyo walikuwa WALAMBA ASALI waqchache kwenye utawala wake tofauti na sasa kila mtu serikali ni MLAMBA ASALI , ndiyo maana Mh Rais SSH anaonekana kama anapwaya.
 
Au kwa lugha nyingine yeye mwenyewe hakuwa supportive and loyal kwa hayati JPM (RIP) Please tell this to the birds.
 
Inavyosemekana eti na wale waliokuwa Supportive and Loyal kwa hayati JPM (RIP) Wengi wao wa kutoka kanda ya ziwa na ndiyo walikuwa WALAMBA ASALI waqchache kwenye utawala wake tofauti na sasa kila mtu serikali ni MLAMBA ASALI , ndiyo maana Mh Rais SSH anaonekana kama anapwaya.
Shukrani mkuu. Nimejifunza kitu hapa.
 
Kwa hiyo utetezi hapa bado ni ule ule...anaangushwa na anaowateua na katika msingi huo lawama zielekezwe kwa anaowateua na si kwa yeye mteuzi. Na wako watu na akili zao wataunga mkono utetezi wa hovyo kama huu. Masikini Tanzania.
Tabu sana aisee !!!! Sasa nini ushauri wako tafadhali?
 
Mbona alishawaruhusu wale kwa ukubwa wa kamba zao. Alisahau kwamba mambuzi yenyewe hayana kamba kwa yanazulula shambani kula
Exactly, wanafanya alivyowashauri wafanye, they are supportive and loyal. Hawajamzingua, full stop! Swali langu ni hili, kwa nini walaumiwe hao badala ya anayewateua? If a=b and b=c, then a=c (QED)! I am out!
 
Exactly, wanafanya alivyowashauri wafanye, they are supportive and loyal. Hawajamzingua, full stop! Swali langu ni hili, kwa nini walaumiwe hao badala ya anayewateua. If a=b and b=c, then a=c (QED)! I am out!
SO YOU WANT HER OUT!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom