Ukimya wake unaniumiza

Kwanza ulifanya vizuri kuuliza future ya uhusiano wenu....mwaka mmoja unatosha kabisa kwa yeye kujua kama wewe ni chaguo lake ama vipi. lakini pia, hata wewe kujua, japo kwa maelezo yako unaonekana kuwa tayari yeye kufanya proposal ya kukuoa.

Sasa ni wakati wako kufanya maamuzi magumu, otherwise utajiweka kwake na baada ya miaka mingine miwili, ukajikuta unapigwa chini na anaolewa mwingine.

Ushauri: Ni bora ukawa singo, kuliko kuwa na mtu ambaye mmeishi mwaka mmoja na ana malengo lakini katika hayo malengo wewe sio sehemu yake.....Kwani huwezi kukituliza kwa mda, jaribu kukaa singo kwa mda..!
 
Kwa jinsi navyowafahamu wanaume hapo hamna kitu...

Anza upya mamii utapata wa kwako!
Na bora umeuliza mapema
 
nyota njema huonekana asubuhi....
ishakuwa usiku hapoooo kimbia wewe!
 
Au alikuwa field kwako so muda umeisha? Lol
 
Huyo Ni Mbabe Wako Na Sio Mpz Wako.Chunguza majibu ya kukatisha tamaa anayokupa ameshagundua wewe umekufa kwake na hufurukuti so usipoangalia utakuwa mtumwa kwake na raha ya penz hutoiona.So jipe siku za kukaa kimya kusikilizia then toa maamuzi magumu.
 
msaidie kutimiza ndoto zake, nadhani hiyo ni moja ya njia kupata unacho kitaka.

toa na wewe upate
 
Mapenzi ya siku hizi ni shidaaa full stress kudadadeki
 

kimiya kimya usimtafte, kama anakupenda atakutafta.wanaume wa siku izi majanga anakufanyia vituko ili umuulize chochote apate pa kuanzia. plz usimtafte,
 

Moja ya makosa makubwa yanayofanywa na watu walioko kwenye mahusiano ni hili la kusema msubiri akutafute yeye. Mahusiano msingi wake mkubwa ni mazungumzo, kujaliana na kuthaminiana. Hivyo basi ukiona mmoja anaanza kuwa na mawazo ya kwa nini hajanitafuta au nani amuanze mwenzie hapo tayari kuna shia. Umpendae kitu cha kwanza ukiamka lazima utamani kumjulia khali (hata kama mnaishi wote). Sasa kama ninyi hamuongei kwa jambo dogo kiasi hiko inaonesha au mahusiano yenu yamegubikwa na unafki aidha kuna mmoja kati yenu anamtumia mwenzie. Ongea nae tena usisubiri akutafute, na la msingi lazima ujue kama mna ndoto za kuwa wote ni muhimu pia ukajua maswala yake ya muhimu (nikiamini na wewe ni mmoja wa hayo) pia ni vema mkaanza kushiriki katika kila mnalolifanya kwa heri.
 
Kujua muafaka ni muhimu lakini sa kamind nini, ndoto zinaweza kutimia hata baada ya miaka mia, pole mtafute tu huna haja ya kuendelea kujiumiza!!!!

Evelyn salt dada wa hekima...

Ni Moja kati ya majibu mazuri kutolewa kwenye post hii....

kuumia si kuzuri chamsingi we mtafute fanya kama hujui unajua wakati mwingine nyie dada zetu mnaona kuolewa ni kazi rahisi sana lakini mnasahau kuwa mzigo mkubwa katika maandalizi ya ndoa unakuwa upande wetu wakaka..Hivyo kama umegundua anakupenda upepee upendo wako usichoke mjali mkumbuke hata kwa msg..mchukulie kama zaidi ya rafiki fanya majukumu yale ambayo mtoto wa kike aliyempenda mvulana si kwa pesa zake, uzuri wake, umbile lake, dini au kabila lake BALI Kwa Moyo wake.

HIVYO

Mtafute tu utaona matokeo yake..yamkini ukaupdate hata mawazo yake akakushirikisha kwa nini mpaka sasa bado hajanza michakato ya kukuona pia ukahusika hata kumpa ushauri nini kifanyike..
N.B
Usiigize Upendo hayo yatokee moyoni kabisaa.



Nimeandika kwa haraka bila mpangilio lakini kwa sehemu naamini utachukua kitu na kitakusaidia.


kila la kheri!!
 
Last edited by a moderator:

mmmmhhhhhh
 
una ushauri mzuri

Asante mwaya, ukishapata matatizo ndio unajua kuyakabili, mapenzi ni kizunguzungu yakikataa yanauma mno ila inabidi usonge mbele hakuna linaloshindikana ukidhamiria.
 

Pole dear.... tatizo sie binadamu huwa tunapenda kusikia yale ambayo masikio yetu yanapenda/yanataka kusikia.

Amekujibu kwa swali ulilomuuliza. Unataka nn tena? Kumlazimisha aukuoe au?
 

Nakubaliana na ulichokiandika ......:bounce:
 
Hamna mahusiano hapo, mnapotezeana muda
 

Mbona mkuu mamaafacebook umemaliza meneno yote ...kazi kwake kufanyia kazi USHAURI ulio mpa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…