Ukimya wa serikali na hatima ya watoto wetu shuleni

mtotowatatu

Senior Member
Jul 31, 2016
103
58
Wasalaamu wakubwa!!
Binafsi nmekuwa muathirika wa Moja kwa Moja na hiki kinachoitwa "Elimu Burr". Nimuathirika kwa kuwa Ndugu zangu wengi wapo katika shule za Kata.

Wasiwasi wangu upo katika masomo ya sayansi maana muda unaenda na hatujui nini hatima ya wanafunzi wetu.
Katika shule nyingi za kata kwa sasa hakuna walimu wa kutosha wa masomo ya sayansi na baadhi ya shule hawapo kabsa.
Serikali iko kimya na muda unaenda nini hatima ya hawa watoto.
Kabla ya elimu bure walimu wa kujitolea walikuwa wakilipwa na wazazi sasa hakuna maana yake waliopo hawatoshi .
Tusaidiane great thinkers nini future ya hawa maskini katika nchi hii ya viwanda??.
Nawasilisha .
 
utapewa jibu rahisi kabisa kwamba hizo ni changamoto za kawaida.
 
Hakuna Elimu ya bure nowadays, hizo Ni siasa, Elimu ni gharama, w anasema Elimu bure halafu watoto wao wanasoma Nje ya nchi na wewe unashangilia Elimu bure, umesahau msemo wa wahenga ukitaka uzuri sharti uzurike
 
Kuna mbunge mmoja aliwahi sema, "children of richmen, MPs, ministers, DCs and RCs wako nje ya nchi wanasoma; hatuwezi peleka watoto wetu kwenye shule za kata"
Lakini mh mwingine anasema shule za kata ni nzuri sana hadi zimefikia kushika namba moja kitaifa akitolea mfano shule moja iliyokuwa ya kwanza kitaifa mwaka huu. Sasa hapo mimi naona mfuko ndo utaamua hatima ya mtoto/ndugu/rafiki yako katika kupata elimu nzuri hususani sayansi na lugha ikizingatiwa shule za kata ndo zimetuletea uandishi wa mwendokasi, idadi ya wasomi wasiojua tofauti ya R&L, H&I, E&I, Y&W ikiobgezeka, wasiojua tensi za kiswahili ndo usiseme.
 
Back
Top Bottom