Ukimya wa Mwigulu na haya yanayoendelea, aachie ngazi

mackie

Senior Member
Jan 26, 2017
141
197
Haiwezekani matukio makubwa ya mauaji pamoja na haya ya utekaji yanazidi kushika kasi dhidi ya raia wema na polisi kwa ujumla yanashika kasi lakini upo kimya na hakuna juhudu thabiti unazofanya..

Unapruvu failure braza ,wizara imekushinda kweli..kuwa muwazi kwa hili,ni juzi juzi tu bunge limekataa kuongelea habari za utekaji lakini usiku wa kuamkia leo tumesikia huko KIBITI yametokea mauaji ya askari 8 wa jeshi la polisi..

Why this please....!!!??

whats wrong with you braza...??

Kama huwezi kazi achia hiyo nafasi...
jitumbue mwenyewe ...
na tunashangaaa sana hata MKULU naye yupo kimya juu ya haya matukio ya mauaji.TISS mko wapi au ndo nyie mnaohusika au ni akina nani..??
Ni ushauri wa bure braza achia ngazi...wizara hii imekushinda ..
 
Mwigulu ni sawa yupo kundi moja na watu Kama
-le mutuz
-mwakyembe
-mrisho mpoto
-Steve nyerere
-kibonde
-jenista mhagama

Hawa watu kwa kweli ni WANAFIKI SANA yaani + KUCHUMIA TUMBO
Wako radhi kutetea UONGO na wakijua ni Ukweli,Lakini kwasababu ya unafiki na kujipendekeza wanaamua bora iwe tu,,kulinda Matumbo yao+Familia zao
 
Mwigulu ni sawa yupo kundi moja na watu Kama
-le mutuz
-mwakyembe
-mrisho mpoto
-Steve nyerere
-kibonde
-jenista mhagama

Hawa watu kwa kweli ni WANAFIKI SANA yaani + KUCHUMIA TUMBO
Wako radhi kutetea UONGO na wakijua ni Ukweli,Lakini kwasababu ya unafiki na kujipendekeza wanaamua bora iwe tu,,kulinda Matumbo yao+Familia zao
hapo hiyo le mutuz anawazidi wote hapo, tangu mamaye apewe ubunge vitu anavyopost vinavuka mpaka aamekuwa kama amepagawa
 
Namwamini Mwugulu

Kazi ya uwaziri wa mambo ya ndani ni tofauti na uwaziri wa michezo na burudani

Wizara ya Mwigulu ni nyeti haihitaji kutangaza mambo yake hadhalani bali kufanya kazi kwa isiri wa hali ya juu ili kufanikisha mikakati yake

Wizara hii inafanana na wizara ya Ulinzi na Usalama.
Kazi zake nyingi zinafanywa kwa siri

Ninavyo mjua Mwigulu si mtu wa mchezomchezo siku sio nyingi wahalifu hawa watatiwa mbaroni na ndivyo tunavyotaka wizara hii ifanye kazi zake

Angalieni tu mafanikio ya muda mfupi wa wizara hii, jinsi

trafiki yaani askari wa usalama barabarani wanavyofanya kazi zao kwa ufanisi,
wizi wa mabenki umepungua, mataikuni wa madawa ya kulevya wanavyopelekwa Marekani kwa hukumu zaidi, wizi kwenye taasisi kama Bandarini ulivyopungua,

Ajali za barabarani zimepungua
Ulevi ulivyodhibitiwa, unywaji pombe baa unaanzia saa Kumi (10) jioni hadi saa (6) sita usiku

Sasa hivi utafiti unaonyesha hata ndoa zimeimarika, madada poa wenyewe wanajiuzuru kazi kwa hiari yao na kuanza biashara ndogondogo

Ulinzi wa sungusungu umeimarika
Vikundi vihalifu kama vya panyarodi vimetoweka kabisa

Kwa ujumla Wizara ya Mwigulu inaendelea kufanikiwa katika kutimiza malengo yake, tofauti na huko nyuma.

Mwigulu hii siyo wizara ya sanaa, chapa kazi kimyakimya watakuja humuhumu kusema, kama kuhusu matukio wasemaji wapo kutegemea na aina, mahali, muda, sehemu ya tukio husika.

Tunataka usalama wa raia na mali zake siyo kauli za kubahatisha.

Asante Mwigulu.
 
Anajiuzuru Kwa Kosa Gani Mh Mwigulu ?
Ikumbukwe Hakuna Huo Utamaduni Hapa Tanzania Wa Kuachia Ngazi.


Inauma Sana Na Kuumiza Kupoteza Watu Kila Siku Tena Hao Ndiyo Wenye Taaluma Ila Nao Wanapotezwa

Nchi Hii Tanzania Ina Vyombo Vingi Professional Kwa Masuala Ya Uchunguzi Ninahakika Wakivitumia Tunapata Majibu Haraka Sana Na Mazuri

Chukua Wataalam JW
Chukua Wataalam PCCB
Chukua Wataalam TISS (Wale Wasioteka)
Halafu Police Wasihusishwe Kwenye Huu Uchunguzi Naamini Ikiwa Hao Hapo Wote Watakuwa Wazalendo Kutuletea Report Nzuri Isioogopa Kusema Ukweli Ninahakika
Ufumbuzi Nzuri Sana Tutaupata
 
Haiwezekani matukio makubwa ya mauaji pamoja na haya ya utekaji yanazidi kushika kasi dhidi ya raia wema na polisi kwa ujumla yanashika kasi lakini upo kimya na hakuna juhudu thabiti unazofanya..

Unapruvu failure braza ,wizara imekushinda kweli..kuwa muwazi kwa hili,ni juzi juzi tu bunge limekataa kuongelea habari za utekaji lakini usiku wa kuamkia leo tumesikia huko KIBITI yametokea mauaji ya askari 8 wa jeshi la polisi..

Why this please....!!!??

whats wrong with you braza...??

Kama huwezi kazi achia hiyo nafasi...
jitumbue mwenyewe ...
na tunashangaaa sana hata MKULU naye yupo kimya juu ya haya matukio ya mauaji.TISS mko wapi au ndo nyie mnaohusika au ni akina nani..??
Ni ushauri wa bure braza achia ngazi...wizara hii imekushinda ..
Unataka Waziri Mwigulu afanye nini,avae naye green jangle combat uniform aende na yeye front au??

Bungeni ameongea na kutoa ufafanuzi wa kila kitu kuhusu kinachoendelea nchini na usalama wa RAIA

Kuhusu kuuwawa kwa Polisi huko Pwani ameeleza na kinachoendelea kuhusu Haya mauaji.

Kama ndiyo maisha mlioamua kuishi watanzania mnataka aingie vinchwani mwenu nyie mmeamua kuua Polisi na yeye anahangaika kuhakikisha Polisi hawauwawi na watu wako salama.

Hawezi muda wote yuko kwenye press conference kama unavyotaka.

Lazima kama Wizara wakae intelenjia ya juu kabisa kuangalia nini kilo field na nini kifanyike maana kwanza Silaha zimechukuliwa na risasi zake INA maana hata RAIA hawako salama mahali Fulani.

Hebu tuwaache hawa Serikali wafanye kazi zao kikamilifu .

Na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ujumla mnatakiwa kukaa kutatua hili jambo kwa kushirikiana sio la Polisi peke yao.
 
Matukio mengi na makubwa yameendelea kutokea hapa nchini na yote yakiigusa wizara ya mambo ya ndani,Lakini kuna ukimya usio wa kawaida wa waziri mwenye dhamana,hakuna tamko,kamati za uchunguzi ama chochote kile kinachofanywa na Waziri huyu matukio kuanzia uvamuzi wa Clouds,kutekwa na kupotea kwa watu wengi tu akiwemo Ben Saa nane,kuokotwa miili ta watu waliouawa na kutupwa huko mkoani mara,Kilimanjaro yule,maiti mto ruvu,kutekwa kwa mwanamuziki Roma mkatoliki Waziri yupo kimya

Leo Askari 8 wameuawa huko kibiti mkoani pwani,Waziri unasubiri nini kujiuzulu upishe wengine wafanye kazi.Wengi tunajua unaishi maisha ya unafiki ya kutomuudhi bosi wako na mwenyekiti wa chama chako ukidhani utakua Rais ajaye baada ya yeye kuondoka unajidanganya,subiri utaopatwa na mshangao
 
Muda mwingine tunaweza kulaumu kumbe na yeye anatulaumu kwa nini hatuoni kitanzi chake

Nadhani tangu kipindi kile mitandao imemsuta alipofika kwenye tukio akiwa na gwanda na akiwa kiongozi wa kwanza ndipo siku aliacha kufuatilia mambo ya hii nchi
 
Back
Top Bottom