Ukimya huu wa maaskofu wetu je, ni uoga?

PastorA

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
361
275
Wapendwa habari zenu, tumeshuhudia na kusikia kwa ushahidi wote kuhusu uvamizi wa kituo cha matangazo cha Clouds Media,

Na baada ya tukio hili tumeona vyombo vya habari vingi na redio pinzani na Clouds wamelaani tukio hili, lakn hii imekuwa tofauti kwa hawa Maaskofu wetu maana wameshuhudia kabisa video ya kutengenezwa mwenzao kuchafuliwa, na hatujasikia hata askofu yyte hata askofu wangu akiongea chchte, hivi huu umoja wa maaskofu walimtenga Gwajima?.. Au wanaogopa nini kulaani kitendo hicho?

Nawaza kama tukio hili angefanyiwa Shekhe na sidhani kama Mashekhe na taasisi zao wangekaa kimya.

Jambo hili lina tia aibu.. Kwenu nimeshangaa hata Askofu wangu yupo kimya.. Hii nguvu ya Bashite sio mchezo.

UKIMYA HUU WA MAASKOFU WETU JE NI UOGA?
 
Si Askofu wenu Gwajima ameshaongea sana?
 
Watanzania wengi ni wanafiki pamoja na viongozi wetu wa dini wanaishi kiunafiki tukio hili la clouds lingetokea awamu iliyopita basi wale watu wa pale kurasini ungesikia wanatoa waraka wa kulaani ila awamu hii mengi yanafanyika ya hovyo hovyo wamekaa kimya tatizo wanafahamu matatizo yao wakijifanya kukosoa wataumbuliwa kwa makandokando yao ndiyo maana siku hizi sitoi sadaka yangu naona hakuna umuhimu. Hili LA kumtenga gwajima lipo wazi toka kipindi cha mchakato wa katiba kama unakumbuka ugomvi uliotokea kwahiyo wamemuweka mbali sana. Sidhani kwenye hii vita ya madawa kama wangemtaja pengo hali ingekuwa hivi! Kwa sasa acha tuishi kufuata mkono wa sheria muda ukifika tutaangalia tunabadili vipi mfumo 2020 siyo mbali
 
Wao wanachoweza ni kumsurubisha Yesu tu, hawana ubavu wa kuwachallenge watawala.
 
Back
Top Bottom