Ukimwonyesha unampenda sana lazima atakutenda

Jay_the_analyst

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
206
Reaction score
151
Binadamu ndivyo walivyo, pale unaposema nampenda sana mwenzangu na ukamwonyesha mapenzi mazito mazito ndipo atakapokutenda bila kujali maumivu utakayoyapata. Hali hii inaweza kumtokea mtu bila mwenyewe kujijua endapo atakuwa mtu wa kushindwa kutumua akili kufanya kumbukumbu za maisha.

WANAWAKE WANAONGOZA
Tabia hii ipo kwa pande zote mbili, mwanamke na mwanaume lakini kwa undani zaidi wanawake ndiyo wanaoongoza kwa kumtenda mwanaume aliyeonyesha mapenzi mazito kwake.Wengi walioongea na safu hii kwa jinsi zote wanawake ndiyo walizidiwa na skendo hii ya kutenda wapenzi wao.
Muddy Sukari wa Dar es Salaam yeye anasema aliwahi kumpenda mwanamke kupita maelezo. Ikafika mahali akaamua kumsomesha hadi chuo kikuu kwa lengo la kumwongezea elimu ili maisha yawe bora, lakini baada ya kuyapata hayo maisha bora alimtenda.

MWANAMKE AKIJUA ANAPENDWA HUFANYA HAYA
Kwa mwaname, upembuzi unaonyesha kwamba akishajua mwanaume anampenda sana, huanza maringo, kutotii na kushika njia yake katika mahusiano akiamini hawezi kuachwa kwa sababu anapendwa sana.
Hili linataka kuonyeshwa kwamba, kama mwanaume atampenda sana mwanamke iwe sehemu ya siri ya moyo wake badala ya kumwambia au kumuonesha kwa vitendo.

MWENYE HEKIMA HUFANYA HIVI
Mwanamke mwenye hekima atakapobaini kupendwa sana na mwenza wake ataongeza upendo kwa nafasi yake ili mapenzi yao yazidi kuwa motomoto.
Kila thamani ya ongezeko la penzi kwake kutoka kwa mwenza wake ni deni la kutafuta namna ya kurudisha upendo huo ili kuwe na uwiano.

MWANAMKE ANAYELIPA UPENDO KWA KUMTENDA MWENZA YUKO HIVI.
Siku zote mwanamke anayependwa sana lakini yeye akarudisha dharau na kutotii kwa kuamini hawezi kuachwa anatoa majibu kwamba hajampenda huyo mwenza wake ila kuna kitu anachokipata ndiyo maana yuko nae, au kuleta dharau kwa anaye mpenda, ikiwemo majibu machafu na hata usaliti wa wazi wazi.

NINI CHA KUFANYA KWA WOTE?
Kwa pande zote ni vizuri sana upendo ukalingana katika mizani moja, mwenzio akionyesha anakupenda sana na wewe kazana kuwa mbunifu kutafuta namna ya kujibu upendo wake badala ya kuutumia kumtenda.
Historia inaonyesha kwamba wengi wanaowatenda wenza wao mwisho wao lazima na wenyewe watendwe na kilio chao huwa kikubwa kuliko kilio cha yule aliyemtenda.Hapo pana kitu cha kujifunza kwamba siku zote mtenda hutendewa na usimfanyie mwenzako jambo ambalo ukifanyiwa wewe huwezi kulipenda hata siku moja.
 
Hata hawa jamaa zetu ukiwaonesha upendo huanza kukufitinisha na ndugu wengine.
 
Raha ya mapenzi ni kupendana. atakae kupenda kweli na utakae mpenda kweli.

Wengine wanajua kuharibu tu basi
 
duh sijui shida ni nini lakini mwanamke wangu ananiringia sana siku hizii...Ameshajua nampenda mno
 
Unajua maana ya RED FLAGS??? we endelea kung'aa sharubu mda si mrefu utaleta uzi hapa jukwaani!
 
Mwanaume ili uwe salama kwenye mapenzi na hata ndoa, usiruhusu mwenza wako akujue, yaani awe anakuona ona tu! akikujua tu, mengi yatafuata.
 
Mmmh ishantokea nilimuonesha binti flani kuwa nampenda Sana but ndo Kama niliongeza gap btn yeye na Mim, Afu kuna binti mwingine alinipenda Sana but nikawa namu ignore, ila somo ukipendwa shikilia, from Now one siwezi kukuonye hisia zang hata iweje utaona picha picha tu
 
Mwanaume ili uwe salama kwenye mapenzi na hata ndoa, usiruhusu mwenza wako akujue, yaani awe anakuona ona tu! akikujua tu, mengi yatafuata.
True... ni kweli kabisa. Ukiwalegezea wanakudharau. So ubandidu kias.. na msimamo
 
Hapo ndipo huwa nachoka na haya mapenzi. Hivi kama mtu unampenda kwa nini usimuonyeshe?
Kwa wenzetu wa nchi zilioendelea.. ukimuonyesha mtu love... na yeye anakupa love.. no secrets.. no lies. Lakini, hapa bongo mashauzi kibao... dharau.. sasa sijui ni ili waonekane kuwa wanammiliki fulani na kumuendesha.. ? Wanadhani ni sifa.. kumbe ndio wanaharibu
 
Back
Top Bottom