Pole sana ndugu yangu yangu kwa hilo,ila mimi nina mambo kadhaa ya kuksema:
Kwanza sio kila unapofanya mapenzi na mtu mwenye VVU utaambukizwa. Kumbuka tumekuwa tunafanya mambo haya mara kadhaa na watu wenye VVU bila kujua na hakuna shida yoyote tunayopata;ni bahati nzuri tu kwamba nyie mlienda kupima soon after hilo tendo..huo ni ujasiri wa hali ya juu na unastahili kupongezwa.
Pili,huna haja ya kukosa amani kiasi hicho.Hilo limeishatokea,limetokea,unachotakiwa ni kufocus mbele na kuendelea na maisha yako kama awali.Najua hii ni chungu kumeza,lakini je ikiwa umeambukizwa,what next?! Hakuna haja ya kuhangaika mahospitalini kutafuta kipimo,unaweza kukipata kwa gharama ya juu sana,maana inaonekana uko radhi kutoa kiasi chochote cha pesa mradi tu ujue afya yako.Swali,sasa ukishajua umeambukizwa,nini kinafuata?! Na je ukiambiwa hujaambukizwa,unadhani itakuwa kinga ya kuzuia kuambukizwa tena?! Nachotaka kusema hapa ni kwamba wewe endelea na maisha yako kama kawaida huku ukisubiri hiyo miezi 3 ipite ukapime tena ili kujiridhisha..
Inavyooneka wewe ni kijana na yumkini upo chuoni,unachotakiwa kujua ni kwamba bado unayo safari ndefu ya kuishi.Utakumbana na mengi tena mazito kuliko hili,jaribu kuwa mstahimilivu.Hili limetokea hivi leo,hujui mwaka kesho utakuja hapa na lipi,so kwa muda huu wewe concetrate with what you're doing.Usije ukapoteza hata unachokifanya,halafu mwisho wa siku unapima unakutwa uko salama..