Ukimwi majeshini kujadiliwa Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukimwi majeshini kujadiliwa Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Apr 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete leo atafungua Kongamano la Kimataifa kuhusu Tatizo la Ukimwi katika Majeshi, litakalofanyika kwa muda wa siku nne katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

  Kongamano hilo linatarajia kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 260 kutoka nchi 70.

  Hadi sasa nchi 60 zimethibitisha kushiriki katika kongamano hili la kwanza kufanyika Tanzania upande wa majeshi ya ulinzi na usalama.

  Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Kapambala Mgawe, amesema kongamano hilo litahudhuriwa na makamanda kutoka nchi za Bara la Afrika, Asia, Amerika, Caribbean, Ulaya, Peru na Marekani.

  Luteni Kanali Mgawe amesema mbali na makamanda wa majeshi hayo, pia kongamano hilo litahudhuriwa na taasisi za kimataifa zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi katika nchi hizo.

  Pia litahudhuriwa na wataalamu wa afya katika majeshi ya ulinzi na usalama na taasisi za kitaifa zinazojihusisha na Ukimwi.

  “Kongamano hili ni la Kwanza kuendeshwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Marekani kuhusu masuala ya Ukimwi baada ya kubainika kupotea kwa idadi kubwa ya nguvu kazi katika majeshi,” amesisitiza Luteni Kanali Mgawe.

  Kupotea kwa nguvukazi hiyo, kumechangia kudhoofisha uwezo wa majeshi hususani katika nchi zinazoendelea zikiwemo za Bara la Afrika.
  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=6608
   
Loading...