Ukimfadhili binadamu usitegemee malipo hapa duniani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Jeniffer alifiwa na mume baada ya miaka saba ya ndoa, aliachwa na watoto wawili wa kike. Jeniffer ana kazi yake na walifanikiwa kujenga nyumba na mume wake. Mume alimuachia Jeniffer pesa na mali za kutosha kulea na kusomesha watoto.
Katika mihangaiki ya maisha Jeniffer anakutana na Lucas. Lucas alioa na kupata watoto wa tatu na mkewe. Mke aliondoka na kumwachia Lucas ulezi wa watoto wadogo. Lucas aliwapeleka watoto kijijini kwa mama yake. Yeye alianza kuwa mlevi.

Jeniffer alianza uhusiano na Lucas aliweka wazi kuwa watoto wake wanakuja kwanza kabla ya mapenzi. Lucas alipenda malezi ya Jeniffer kwa watoto wake. Na yeye alianza kuwaleta watoto wake kutoka kijijini.

Watoto wa kijijini wamefika mjini masikini hata ice cream hawajui. Jenifer aliwapekeka mdogomdogo hivyo hivyo. Watoto wamemaliza shule ya msingi. Secondary walikwenda boda . Watoto wa Jeniffer walikuwa wakubwa kidogo wakubwa na walisoma boarding school Botswana. Graduations zao zote uncle Luca alikuwepo.

Shopping za kuendea shule za watoto wa Lucas Jenifer alizifanya na kuna wakati Lucas akiwa hana hela kabisa baada ya kulipa ada. Leo mtoto wa Lucas ana graduate darasa la 12, amemwambia Baba yake hataki Jeniffer awepo, kwani si mama yake.
 
Hii itakuwa huko ughaibuni, kwa Tanganyika hakuna mtoto asiyekuwa na adabu kama huyo, hivyo Dakitari nakushauri umaluzie tu hii story yako ili tujue tunaongelea masuala ya nchi gani.
 
Sky ulipashwa kuwa Director wa Bongo movies maanake story ya kutengeneza movie moja wao wanatoa movie tatu. Anyway hongera zako ukimaliza kazi zako kwenye Sekta ya Afya. Si vibaya ukaja huku kwenye tasnia ya filamu uweke mkono wako. Kila la kheri.
 
Lucas hakuwa mkweli kwa watoto wake..alibeba utukufu na sifa yeye pke yake akuwaambia watoto wake mchango wa Jennifer.Lucas abadirike aache tabia mbaya
 
Labda ungeweka neno "Ceteris Paribus" vinginevyo sio kweli, watu wanalipwa hapa hapa duniani.
We mwenyewe nikikutoa out, nikakuacha na laki 5, kesho nikakupeleka shopping Dubei, Keshokutwa Nikakujengea flyover, nitasubiri unilipe ahera?
 
Mkuu account yko imedukuliwa lazima, sio bure khaaa ( jokes[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…