Wimbo
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 887
- 664
Unapokua kiongozi wa nchi, watu kukaidi seria kwa yale ambayo mmpepanga kwa maendeleo ya Nchi na ukawaacha wafanye wanavyotaka ndo utawala bora,? Mtu anaamka anaweka kibanda cha mabati kuukuu mtaa wa Samora ati anafanya ujasilia mali mahali palipokatazwa na ukamuacha ndo unajari usawa wa ninadamu? watu kuamka na kuchoma majumba ya watu usiwatie mkongoto na kuwaacha wafanye unavyotaka ndo utaonyesha unawapenda watu? Najaribu kufikiria Mwaka 1971 Nyerere aliponyanganya mabenki na viwanga vikawa vya uma watu walilaani wakawita dictator, vyombo vya habari duniani kote vikalaani, acha hiyo 1974 alipotufurusha wote kuhamia vijijini watu wakafa wengine wakaliwa na simba watu si walipiga kelele, leo si ndo tunamwita kiongozi bora, Baba wa Taifa aliyewapenda watu wake. Katika hili nimpe ushauri wa bure Mh. Kikwete ukiwachekea Nyani utavuna mabua (viminyo tu asiyetaka ahame aende atakako taka kufanya anayotaka hata Kambona alienda lakini alirudi)