Baraka cassidy
Member
- Apr 14, 2016
- 6
- 18
Kuna wakati ni ngumu kukumbatia maumivu ukitabasamu.
Kuna wakati usingizi huja baada ya machozi.
Wakati ambapo kila ladha ni Chungu na kila tendo ni vivu.
Huo wakati ambao hujielewi wewe ni nani ukihisi umepungukiwa akili ,nafsi mpaka roho.
Huo wakati unaopitia ni kila mtu anapitia kwa namna yake kwa kipindi cha maisha fulani,Yapasa ujue.
Jua la mchana likikuchoma ,usilichukie bali cheka nalo ukilitania.
Na Giza la usiku likiingia zungumza nalo kitajiri kuhusu Mwanga.
Lala na Tumaini ,usilale na majonzi.
Hivyo Basi ukilala ,utakuwa umelala kitajiri.