Ukila na kipofu usimshike mkono akashituka.

Ukila na kipofu usimshike mkono akashituka.

Shida na raha

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
3,773
Reaction score
3,474
Habari za mihangaiko ya kazi ndugu zanguni.

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kuna mdada mmoja tulifahamiana kwenye fb kama rafiki, urafiki wetu uliendelea kukua yapata miezi miwili sasa lakini hatujawahi kuonana ana kwa ana.
Tuliendelea kuchat usiku kucha mchana kucha yaani haipiti dakika ni mwendo wa kutafutana tu.
Lengo la hivyo kuna mzigo nilimuomba anichukulie kuwa niliona mkoa aliopo ndo mzigo wangu ulipo.

Siku zilienda hatimae tukajikuta sote wawili kila mmoja ameanza kumtamani mwenzake kwa picha tu.
Sikatai mwanamke ambae tayari tumeanza kutamaniana kuniomba japo hela ya vocha. Ila atumie akili kuomba asifanye kwamba ameshafika kwangu wakati hata busu sijawahi kupata.
Siku ya kwanza alitaka kunipiga mzinga nikajinasua kiaina lakini sikujua mzinga huo ulikua wa kiasi gani. Naweka maneno aliyoanza kunambia:

Yeye: baby, mme wangu kuna kitu naomba nikwambie.
Mimi: kitu gani?
Yeye: kwanza nijibu nikwambie???
Mimi: baby kuna ishu ya pesa naifuatilia kuna jambo langu limekwama maana kwenye account hamna tena hata mia.
Yeye: baby mimi nilikua nataka nikuombe hiyo hiyo pesa.
Mimi: basi ndo hivyo baby ndo umecherewa kidogo tusubiri nikipata mshahara mwezi unaofata.
Yeye: sawa mme wangu.

Sasa tuliendelea kuchat hakunipa raha kila wakati alitaka niwe "online." Niliendelea na ile hali mpaka nikaizowea.
Ila nilimsifu kitu kimoja, mwanzo hakuwa na shida hata ya vocha kumbe alikua ananipimia tu.
Sikuwa na wasi wasi juu yake maana niliona tayari nilishapata mtu ambae hapendi mizinga kama wengine maana alikua kwenye duka la mama yake vocha kila kitu alikua anachua humo.

Juzi moja alipote online kama siku mbili, baada ya kumuuliza alinijibu sim yake ipo kwa fundi na imedondoka kwenye maji, lakini haina shida sana.
Akawa ana sim nyingine anatumia kwa mujibu wa maelezo yake. Sasa juzi ya kuamkia jana akanitumia sms za kutaka ajibiwe haraka haraka maana alisema sim kaazima, maana yake sim yake imeyaribika.
Akanambia nimuongeze elfu 70 aongeze na laki moja ya kwake akanunue japo tecno W4.

Sasa mimi nikaanza kutafakari, sim ya kwanza ipo kwa fundi ya pili imeharibika, kwanini asichukuwe hiyo hiyo laki moja ya kwake akaenda kuzigomboa zote kwa pamoja?
Kama amepungukiwa japo kidogo ndo nimuongezee?
Kwanini aache kila sim kwa fundi?
Au ananidanganya?
Nilijiuliza na moyo wangu.

Hapo hapo nikapata jibu la haraka haraka, "Ukiacha mwana kulia, utalia wewe." Nikachukuwa uamuzi wa kiume.
Niliamua kusema si wa kwanza huyu kwanza hatujawahi kufanya chochote na istoshe nipo mbali nae na sijui ni siku gani ambayo ntakutana nae.

Nikaamua kum block fb na wasp. Nilijisemea mwenyewe leo kaanza hapa kwa yeye anaona ndogo nikimchekea kesho atanambia nimpe laki 2 wakati kuna watu wanaitafuta mia tano tu hawaipati.
Wenzake walikua wanatumia akili angalau wanaomba elfu 15 au 10 yeye kaanza pakubwa.

Wanaume wenzangu, vyuma vimekaza usichezee pesa kwa mtu anaejifanya anakuita baby za ulaghai. Ni bora wewe ni mwanaume mwenzangu tunaetafuta kwa jasho ukibanwa ntakusaidia kuliko mtu ambae ana miradi mingi na ana uwezo wa kuitumia kila sehemu.
 
Waga naanza kufikiria faida ya huo mzinga nikifanya cha maana
Au somtyms napata wazo2 la hyo hella kumpa ndugu au mafuta
Ninaemuhonga kaniingia sana akilin
 
Mmh. Ila mnazidi kuwa wachungu jamaani khaaa. Hivyo hapo umeshapiga mahesabu utaombwa kikubwa zaidi ya hicho. Daaah.

Pia inaelekea hakukufaa hivyo ulikuwa unatafuta sababu ya kumuacha sio bure sababu kwani ungemwambia huna kingeharibika nini.

Na upande mwingine sie wanawake tujuage kujiongeza basi ili tuepuke vitu kama hivi sababu mwisho wa siku unaweza sema mbona sidumu kwenye mahusiano kumbe vizinga visivyo na macho ndio sumu.
 
Mmh. Ila mnazidi kuwa wachungu jamaani khaaa. Hivyo hapo umeshapiga mahesabu utaombwa kikubwa zaidi ya hicho. Daaah.

Pia inaelekea hakukufaa hivyo ulikuwa unatafuta sababu ya kumuacha sio bure sababu kwani ungemwambia huna kingeharibika nini.

Ila na sie wanawake tujuage kujiongeza basi ili tuepuke vitu kama hivi sababu mwisho wa siku unaweza sema mbona sidumu kwenye mahusiano kumbe vizinga ndio sumu.
Umeanza vibaya umemaliza vizuri, asante kwa kujirekebisha.
 
Mmh. Ila mnazidi kuwa wachungu jamaani khaaa. Hivyo hapo umeshapiga mahesabu utaombwa kikubwa zaidi ya hicho. Daaah.

Pia inaelekea hakukufaa hivyo ulikuwa unatafuta sababu ya kumuacha sio bure sababu kwani ungemwambia huna kingeharibika nini.

Na upandw mwingine sie wanawake tujuage kujiongeza basi ili tuepuke vitu kama hivi sababu mwisho wa siku unaweza sema mbona sidumu kwenye mahusiano kumbe vizinga ndio sumu.
Vyuma vinapozidi kukaza na ndio tunazidi kuwa wabunifu kukwepa mizinga
 
Sema huna ela umepigwa kizinga pabukwa you can't afford. Usikimbilie vyuma vimekaza hapa
Ndugu ya kuhonga kweli sina na naiwazia sana, ila ukiwa na shida kwa elfu 20 sema ntakusaidia ila iwe ya kweli.
 
Hongera kwa kujitambua..

Angekua zuzu angepigwa mchana kweupe!!!!
 
Hutaki mizinga huku unataka apendeze[emoji23][emoji23]jamaani muwage na huruma eti.
 
Back
Top Bottom