Huyo achana naye kabisa. Hata kama unampenda vipi, tulia, utampata mwingine atakayekufaa zaidi. Halafu usikubali mimba, make unajua wenye pesa hawalei mimba watamtolea nje fasta. Atakuja kwako akishatemwa na kujifanya ametulia kama kondoo. Kitakachofuata: 'mpenzi nikwambie kitu? Nina mimba yako'. Usikubali mpaka kipimo cha DNA kithibitishe. Halafu 'title' yako inaoyesha umekatazwa kuoa lakini habari inaonyesha 'umeshauriwa' kuachana na huyo malaya na unaweza kuoa mwingine.
sikulaumu hata kidogo. Labda binti anajua mambo ndo maana hukutaka kumusiliza mama yako mdogo. Penzi la kicheche lilikuchanganya.
Kubali mimba ndo garama za uzembe wako.
Pole sana mkuu! Ila hata mimi sikushauri uwe na huyo kicheche kwani kama ameshindikana sasa hivi usitegemee aje kubadilika ndani ya ndoa. Mbwage fasta, hakufai huyo hata kama anayajua vizuri kunako 6x6!!!
Usisahau kwenda kupima kama hajakuachia AIDS mana ake!!!
Wanawake wazuri wapo wengi sana, kaa chini chunguze yule ambaye unamuona anafaa pia usimsahau kumuomba Mungu wako!
Nakutakia kila la kheri mkuu!
Kuna rafiki yangu alikatazwa kuoa mwanamke mwenye tabia kama hiyo, jamaa alipenda kufa ikabidi ajibebe mzima mzima na akaoa kwa nguvu. Mwaka mmoja wakapata mtoto, baada ya siku chache akagundua kuwa kuna jamaa mwingine naye anadai huyo mtoto ni wake. Jamaa akavumilia. Siku nyingi hazikupita demu katembea na rafiki wa mumewe na hata mume alipogundua huyo demu hakuacha na tayari wana ndoa ya kanisani, HADI KIFO! It's true and not a joke, na hadi leo wanaishi wote lakini ndoa imekuwa ndoano hivi sasa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.