Ukijiita "MNYONGE" utakuwa mnyonge mpaka kufa kwako,maneno yanaumba. Soma hapa uzinduke leo

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,491
3,998
Kwanza kabisa natangulia kusema SIIJUI KESHO YANGU lakini siwezi kuwa mnyonge kila siku.

Watanzania tumejengewa dhana potovu sana. Hivi unajua kujiita mnyonge ni kujidhalilisha?

Kama ulikua hujui usipopata changamoto katika maisha utakuwa mjinga tu,ukiishi ukiamini"mimi ni mnyonge" utakuwa mnyonge mpaka kufa,hata ukipewa dili ya milioni 100 utaona ujinga sababu tayari una dhana ya unyonge moyoni mwako.

Jitoe kwenye unyonge leo acha mawazo ya miaka 1800s, nani asiependa maisha mazuri? Nani anapenda kuwa mnyonge kila siku?

Ikiwa watanzania wengi wataendelea kuamini wao ni wanyonge wasiojiongeza badi tuna safari ndefu sana kufikia hata Kenya tu.

Unyonge unafanya mtu anatawaliwa, anadharauliwa,anateswa na kuonewa.

Dhana ya unyonge inapaswa kufa haraka sana, mama Samia naomba uhakikishe hilo ili nchi isonge mbele haraka. Kama unakubali ni mnyonge nyosha kidole juu na unipe mwisho wa unyonge ni ni lini kwako.
 
Kwa hiyo ukijiita chuma utakua chuma?
Ukijiita rais utaingia ikulu?
Ukitamka , ukaamini na ukaishi ndani ya malengo ya kukufikisha au kukufanya uwe au upate unachoamini na kukitamka kila wakati pasipo kuruhusu mawazo ya "kutokuweza" ama kukikatia tamaa unaweza ingia ikulu, unaweza kuwa na moyo kama chuma au mkakamavu kama chuma.

Maneno yana nguvu na yanaumba hivyo kujiita mnyonge huku ndani yako kujichukulia hivyo, moja kwa moja unatengeneza mazingira ya kuishi maneno hayo.
 
Hata mimi ili suala la kujiita mnyonge huwa sikubaliani nalo.Sababu mnyonge siku zote huitaji mwenye nguvu, yaani mbabe amsaidie,hapo ndipo naona pana shida.

Kwanini ukubali kuitwa mnyonge? Ki uhalisia hakuna anaetaka kuonewa na hata akionewa ni kutafuta mbinu ya kujitetea kwa kila hali na si kutafuta mtu akutetee sababu utaonekana ni dhaifu, sasa kwa nini uhalisia huu usitumike ili wote tujione tuna nguvu na sio wanyonge.

Mimi naona ni vizuri kujiita wenye nchi aka wananchi badala ya wanyonge,sababu hii itatoa changamoto kila mtu kubeba majukumu ya kulinda nchi,kulinda rasilmali za nchi,kufichua maovu,kulinda haki na usalama,pia kuchagua watu wanaowataka ili kuwaongoza. Sababu mwenye chake ukitunza.
 
Hata mimi ili suala la kujiita mnyonge huwa sikubaliani nalo.Sababu mnyonge siku zote huitaji mwenye nguvu, yaani mbabe amsaidie,hapo ndipo naona pana shida.Kwa nini ukubali kuitwa mnyonge? Ki uhalisia hakuna anaetaka kuonewa na hata akionewa ni kutafuta mbinu ya kujitetea kwa kila hali na si kutafuta mtu akutetee sababu utaonekana ni dhaifu, sasa kwa nini uhalisia huu usitumike ili wote tujione tuna nguvu na sio wanyonge. Mi naona ni vizuri kujiita wenye nchi aka wananchi badala ya wanyonge,sababu hii itatoa changamoto kila mtu kubeba majukumu ya kulinda nchi,kulinda rasilmali za nchi,kufichua maovu,kulinda haki na usalama,pia kuchagua watu wanaowataka ili kuwaongoza. Sababu mwenye chake ukitunza.
👏👏👏👏 Angalia hata wanajeshi wasipokuwa jasiri hawafai kwenda vitani...lazma ujipe moyo ili ushinde.
 
Magufuli alipachika watu dhana mbaya sana...eti sisi wanyonge!! Hizi Nyerere angekuwa mnyonge nchi ingepata uhuru kweli? Unyonge una mwisho...huwez kuwa mnyonge kila siku mwishowe utakuwa mjinga sasa
Unyonge ni uoga wa maisha
 
Uchagani ukijiita MNYONGE utatumwa mpaka uzee wako...na kila mtu anataka kujitoa kwenye unyonge.

Ili uonekane una akili ni jinsi unavyopqmbana na changamoto za maisha. Ukitesekeka sana akili itakuja kichwani tu.

Nani asiye penda kuendesha gari zuri? Kuwa na nyumba nzuri?
Tafsiri ya neno mnyonge,yan hana uwezo wowote hata ukimnyonga atakwangalia tu
 
Kwanza kabisa natangulia kusema SIIJUI KESHO YANGU lakini siwezi kuwa mnyonge kila siku.

Watanzania tumejengewa dhana potovu sana. Hivi unajua kujiita mnyonge ni kujidhalilisha?

Kama ulikua hujui usipopata changamoto katika maisha utakuwa mjinga tu,ukiishi ukiamini"mimi ni mnyonge" utakuwa mnyonge mpaka kufa,hata ukipewa dili ya milioni 100 utaona ujinga sababu tayari una dhana ya unyonge moyoni mwako.

Jitoe kwenye unyonge leo acha mawazo ya miaka 1800s, nani asiependa maisha mazuri? Nani anapenda kuwa mnyonge kila siku?

Ikiwa watanzania wengi wataendelea kuamini wao ni wanyonge wasiojiongeza badi tuna safari ndefu sana kufikia hata Kenya tu.

Unyonge unafanya mtu anatawaliwa, anadharauliwa,anateswa na kuonewa.

Dhana ya unyonge inapaswa kufa haraka sana, mama Samia naomba uhakikishe hilo ili nchi isonge mbele haraka. Kama unakubali ni mnyonge nyosha kidole juu na unipe mwisho wa unyonge ni ni lini kwako.
Watu bhana...
Maneno yanaumba, ni maneno mabaya tu yanaumba, mazuri HAYAUMBI maana kila siku kuna watu wanaongea maneno mazuri juu yao na kuomba yatokee ila wapi...
 
Back
Top Bottom