Ukijifanya mbabe tegemea pia anguko,Magufuli hapa umefeli.

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Watanzania walifurahia pale Rais wetu wa JMT ndugu John Pombe alipochaguliwa,walifurahia wengi japokuwa kuna ambao walichukia,waliofurahia ni wale waliotaka Rais mwenye element za udikiteta(dictator). Hii ilikuja baada ya nchi kugeuka kuwa shamba la bibi na kuwa sehemu ya kufuja pesa sambamba na ukosefu wa maadili kwa watumishi wa umma.
Tuligemea Rais huyu atakuwa mkombozi wa wanyonge,ni dhahiri sasa kuwa kila mtanzania mwenye akili timamu kagundua kuwa Rais wetu hana dhamira ya kumkomboa mnyonge,awamu ya tano imedhamiria kuwafilisi matajiri,kuwanyonya masikini ikiwemo kuwanyima ajira vijana masikini waliosoma kwa gharama kubwa kwa hisani ya bodi ya mikopo na wengine kujilipia. Pia serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuwakomoa wapinzani na kuweka mazingira ya kuua upinzani,serikali ya awamu ya tano imekosa vipaumbele ambavyo vinagusa Moja kwa Moja mahitaji ya mwananchi wa kipato cha chini ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama,umeme wa bei nafuu,MADAWA na vifaa tiba katika hospitali za umma.

Ukweli wananchi wamechoshwa na awamu ya tano.

Katika miaka yote ya awamu zilizopita,nadhani awamu ya tano inaweza kuwa awamu mbovu mbovu kupita zote katika nchi yetu. Mawaziri wamaekuwa wa hovyo hovyo, ukiachilia mbali waziri wa Ardhi mhe.William Lukuvi ambaye kwangu Mimi namuona kama presidential material,mawaziri wengine hawaba mchango tena na matokeoa yake wameahindwa kutimiza wajibu wao kama mawizi.

Wananchi wamefikia hatua ya kuchukia serikali na kutamani itokee hata vurumai ili tuheshimiane. Serikali gani hii?.

Nasema hivi hii serikali ya awamu ya tano ni serikali ya hovyo kuwahi kutokea.

Kila MTU ajiombee,mambo ya kusema tuombeane ili hali hamuoneshi la maana ni bora tuendelee kuombea marehemu.
Naomba mnipe kura 2020 niwe rais wenu kwa maisha bora kwa kila mtanzania.
Usirudie kosa 2020
Ni Mimi Rais anayesubiriwa kuapishwa 2020.
Mwafaaaaa
Ngoja niende kolomije kutafuta matokeo ya Mr. F(DAB).
 
Hata kuchangia inakua ngumu sasa maana ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,badala ya kucheza yeye anaendelea kula majani tu.

Anyway, naona bado mkuu yupo busy na teuzi za kulipizana fadhila so tusubiri akimaliza atawakumbuka na wengine like vijana wasokua na ajira.

Kiukweli anayoyafanya mkuu mazuri ni machache kulikoni maovu. Issue ya ajira kwa wahitimu, watoto wa maskini kukosa mikopo na kuukandamiza upinzani ni moja ya mambo ya ovyo kabisa anayoyafanya baba huyu.

Wampe na Mrs John Komba ubunge wa viti maalumu Japo aweze kuilea familia..
 
Naogopa kuitwa mchochezi mkuu
Kuwa huru mkuu. Hapa uchochezi uko wapi?.
c05e4826b375d5b5d5e50557a451b666.jpg
.
Speak ili mradi tu hujamtukana MTU.
 
Kama ingekuwa inawezekana basi tungemuomba Kikwete arudi ikulu angalau kwa mwaks mmoja amuelekeze kazi huyu jamaa maana hajui cha kufanya kwasaasa amebaki Mara katerero, Mara hakuna njaa,Mara visasi, kusumbua polisi wakati watu wana ngoja maendelea yeye hana hata moja anatetea madivision Zero
 
Back
Top Bottom