Ukifa leo utakwenda kwa Mungu?

Ukifa leo utakwenda kwa Mungu?

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,288
Reaction score
5,762
Hapa sina nia yoyote ya kumsema mtu ila ni kuelimishana tu

Naamini mtu akikaa mwenyewe (peke yake) akatafakari anaweza kujua mahusiano yake na Mungu yakoje namaanisha anaweza kujua kama amefaulu au kuna cha kujirekebisha

Sasa kwa kuwa nafasi bado tunayo; kwa nini tusichukue hii fursa kujirekebisha kwani hatujui muda wala saa?

Mambo matatu makuu yanayotuweka mbali na Mungu ni

1. Harakati za kutafuta mali
2. Tamaa ya kujilimbikizia mali na Ardhi
3. Wivu na husuda

  • Angalia njia yako ya kujipatia kipato kuona kama inampendeza Mungu; kwa kawaida kisicho mpendeza Mungu hakiwapendezi hawa wanadamu wanaotegemea huduma yako. Mfano: Kupunja kwenye Mizani, Kuchakachua bidhaa, wanasheria wanaopindisha sheria, Wizi nk Mungu hapendi kabisa
  • Kumiliki mali ni jambo jema sana ila angalia upatikanaji wake; kama unaona umilikaji wako mali unatokana na kunyima watu wengine haki yao ya kupata huduma; jua Mungu hapendi kabisa na siku unaondoka pengine zinaweza kusambaratika zote na bado unahoja unatakiwa ukajibu kwa Mungu
  • Watu wengine huchukia watu kwa Wivu tu na kuwafanyia figisu figisu ili wafukuzwe kazini/kwenye ndoa zao na kuharibu Maisha yao kabisa; Hii huambatana pia na Uchawi/ushirikina wa kutesa watu wengine bila sababu; Kama unafanya haya, jua Mungu anahasira na wewe; jirekebishe
  • Kuendekeza Zina ama pengine kutumia zinaa kama kigezo cha kumpatia mtu favor nk Mungu hapendi
Nakumbushia kuwa kusali/kumwomba Mungu ni jukumu la msingi la Binadamu wote hata hivyo kama mtu anasali huku akiendelea kutenda hayo machafu ni sawa na kusema anakwenda tu kujionesha kanisani/msikitini kwani sala zake hazijamsaidia kubadilika. Tuna nafasi ya Kubadilika na kuacha hayo na MUNGU wetu ni mwingi wa kusamehe

“Kumbuka Mungu hadanganyiki kwani anaona yale ya waziwazi na yale ya sirini”
Muhimu ni kukumbushana ila uamuzi ni wa kwako!
 
Kwani ndugu kwa usomaji wako wa Biblia hujangamua tu kwamba kuna watu wanye Karama ya wito wa Mbinguni na wengine wataishi dunia?

Hujui kuwa hawa wa wito wa mbinguni watakuwa wafalme au viongozi wakitawala dunia yenye watu?

Hebu tupigania kwanza nafasi ya kuja kuishi duniani kwenye Dunia Paradiso

Luka 22:28-30
28 “Hata hivyo, ninyi ndio mmeshikamana namia katika majaribu yangu;b 29 nami ninafanya agano pamoja nanyi, kama Baba yangu alivyofanya agano pamoja nami, kwa ajili ya ufalme,c 30 ili mle na kunywa mezani pangu katika Ufalme wangu,d na kuketi kwenye viti vya ufalmee ili kuyahukumu makabila 12 ya Israeli.

Ufunuo 5:10
10 na ukawafanya kuwa ufalmea na makuhani kwa Mungu wetu,b nao watatawala wakiwa wafalmec juu ya dunia.”
 
Hapa sina nia yoyote ya kumsema mtu ila ni kuelimishana tu

Naamini mtu akikaa mwenyewe (peke yake) akatafakari anaweza kujua mahusiano yake na Mungu yakoje namaanisha anaweza kujua kama amefaulu au kuna cha kujirekebisha

Sasa kwa kuwa nafasi bado tunayo; kwa nini tusichukue hii fursa kujirekebisha kwani hatujui muda wala saa?

Mambo matatu makuu yanayotuweka mbali na Mungu ni

1. Harakati za kutafuta mali
2. Tamaa ya kujilimbikizia mali na Ardhi
3. Wivu na husuda

  • Angalia njia yako ya kujipatia kipato kuona kama inampendeza Mungu; kwa kawaida kisicho mpendeza Mungu hakiwapendezi hawa wanadamu wanaotegemea huduma yako. Mfano: Kupunja kwenye Mizani, Kuchakachua bidhaa, wanasheria wanaopindisha sheria, Wizi nk Mungu hapendi kabisa
  • Kumiliki mali ni jambo jema sana ila angalia upatikanaji wake; kama unaona umilikaji wako mali unatokana na kunyima watu wengine haki yao ya kupata huduma; jua Mungu hapendi kabisa na siku unaondoka pengine zinaweza kusambaratika zote na bado unahoja unatakiwa ukajibu kwa Mungu
  • Watu wengine huchukia watu kwa Wivu tu na kuwafanyia figisu figisu ili wafukuzwe kazini/kwenye ndoa zao na kuharibu Maisha yao kabisa; Hii huambatana pia na Uchawi/ushirikina wa kutesa watu wengine bila sababu; Kama unafanya haya, jua Mungu anahasira na wewe; jirekebishe
  • Kuendekeza Zina ama pengine kutumia zinaa kama kigezo cha kumpatia mtu favor nk Mungu hapendi
Hapo nimeandika tu baadhi na utaona sija andika kusali; kwani kama unafanya hayo machafu kusali kwako hakujakusaidia chochote pengingine ni sawa na kwenda tu kujionesha kanisani/msikitini; tuna nafasi ya Kubadilika na kuacha hayo na MUNGU wetu ni mwingi wa kusamehe

“Kumbuka Mungu hadanganyiki kwani anaona yale ya waziwazi na yale ya sirini”

Mwamposa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom