Ukialikwa kwenye kipindi cha Redio au TV unalipwa?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,284
6,712
Napenda kufahamu unapoalikwa kwenye TV, au REDIO kama ilivyo kwa kina mzee MKINGA, H.POLEPOLE, K.Mkumbo, Maprofesa, madokta na watu wa kawaida kuna malipo yoyote huwa yanatolewa?

Kwa anayefahamu kama kuna malipo ni kiasi gani?
 
Ni sehemu ya kuonesha mapenzi yako kwa unachokiamini, ukiwa mkereketwa wa ccm ni field ya kupata UDC.
 
Inategemea kuna mada nyingine inakuwa kama kipindi maalumu hivyo mwalikwa analipia udhamini....kama LHRC wanavyofanya kina sungusia,kuna mada nyingine ukiitwa unaweza ukaweka masharti kwamba unahitaji ulipwe gharama ya usafiri chakula na kutoa elimu...ila wengine wanaomba ili wapate platform ya kujitangaza.
 
Wale wazee wa malumbano ya hoja ITV kila mada wanajua washafanya ajira nasikia kila kipindi wanakula 50k ya kuwarudisha home usiku
 
Inategemea kuna mada nyingine inakuwa kama kipindi maalumu hivyo mwalikwa analipia udhamini....kama LHRC wanavyofanya kina sungusia,kuna mada nyingine ukiitwa unaweza ukaweka masharti kwamba unahitaji ulipwe gharama ya usafiri chakula na kutoa elimu...ila wengine wanaomba ili wapate platform ya kujitangaza.
Ahsante mkuu kwa kunijuza hili
 
Back
Top Bottom