Ukiacha tofauti zetu za kisiasa; haya yatuunganishe kama Taifa

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
37,141
46,411
Ukiachana na tofauti zetu za kisiasa ambazo ni haki ya kila mmoja kikatiba, lakini bado mambo haya ni muhimu sana kutuunganisha kama Taifa!

1. AMANI.

Tuhakikishe kwamba chembe chembe zote zinazopelekea amani kuvunjika tunaziepuka.

Tuhakikishe kwamba tofauti zetu hazivuki mipaka na kuharibu a man I yetu, kwani amani ikipotea hakuna atakayebaki salama.

2. UCHUMI.

Uchumi ndio maisha!

Uchumi ukivurigika basi maendeleo na maisha yetu yanakua mashakani.

Tuhakikishe tunakuza pato la Taifa kwa kufanya kazi halali na kulipa kodi ipasavyo!

Harakati zozote za kuvuruga uchumi wa nchi ni za kupiga vita!

Tukihakikisha hayo yote mawili tunaungana pamoja Taifa litaendelea bila kujali tofauti zetu za kisiasa!
 
Mkuu stroke;
Tatizo lenu maccm ni kuwa mnajua kweli siasa za majukwaani. Ahadi hata milioni moja kwenu kuzitoa si shida ila kuzitekeleza ni ndoto.
Amani mnayo ihubiri mbona ndo kwanza mnatafuta kila njia ya kuivuruga bila hata sababu?? Uchumi mnao uhubiri, mbona tena kila kitu mnafanya hata nje ya bajeti au bila hata bajeti??
Stroke, mna mawazo mazuri yaan baas tena. Lakini, Hayatekelezekiiiiii. Yapo kwenye vitabu vyenu
 
Haya yote ni muhimu lakini yatawezekana iwapo tutafuata katiba,sheria na taratibu tulizojiwekea kama nchi kuanzia kwa viongozi hadi wananchi wa kawaida
 
Amani ni Tunda la Haki.
Bila Haki patakuwa na Amani ya kinafiki tu.
Tujitahidi kutenda haki ndio amani ya kweli itapatikana.
CC.Maalim Seif vs Jecha.
 
Ukiachana na tofauti zetu za kisiasa ambazo ni haki ya kila mmoja kikatiba, lakini bado mambo haya ni muhimu sana kutuunganisha kama Taifa!

1. AMANI.

Tuhakikishe kwamba chembe chembe zote zinazopelekea amani kuvunjika tunaziepuka.

Tuhakikishe kwamba tofauti zetu hazivuki mipaka na kuharibu a man I yetu, kwani amani ikipotea hakuna atakayebaki salama.

2. UCHUMI.

Uchumi ndio maisha!

Uchumi ukivurigika basi maendeleo na maisha yetu yanakua mashakani.

Tuhakikishe tunakuza pato la Taifa kwa kufanya kazi halali na kulipa kodi ipasavyo!

Harakati zozote za kuvuruga uchumi wa nchi ni za kupiga vita!

Tukihakikisha hayo yote mawili tunaungana pamoja Taifa litaendelea bila kujali tofauti zetu za kisiasa!
Hakuna amani bila haki.Vita yeyote inaletwa na Vyama tawala kubana haki za RAIA nankuvunja katiba,ubaguzi usiokuwa na lazima.Cha nsinginmwambie mwenyekiti wako aache Ubaguzi.
 
Ukiachana na tofauti zetu za kisiasa ambazo ni haki ya kila mmoja kikatiba, lakini bado mambo haya ni muhimu sana kutuunganisha kama Taifa!

1. AMANI.

Tuhakikishe kwamba chembe chembe zote zinazopelekea amani kuvunjika tunaziepuka.

Tuhakikishe kwamba tofauti zetu hazivuki mipaka na kuharibu a man I yetu, kwani amani ikipotea hakuna atakayebaki salama.

2. UCHUMI.

Uchumi ndio maisha!

Uchumi ukivurigika basi maendeleo na maisha yetu yanakua mashakani.

Tuhakikishe tunakuza pato la Taifa kwa kufanya kazi halali na kulipa kodi ipasavyo!

Harakati zozote za kuvuruga uchumi wa nchi ni za kupiga vita!

Tukihakikisha hayo yote mawili tunaungana pamoja Taifa litaendelea bila kujali tofauti zetu za kisiasa!

Mkuu stroke hapo namba mbili ndio kuna utata.

Amani huwa ni kitu kisichohitaji unafiki.

Fanya PROPAGANDA kwenye kila kitu, ila sio kwenye AMANI.

Amani ni tunda la haki, yaani, Amani haiwezi kuwepo kama haki haipo hii ndio formula yake.

Tunachokiona sasa serikalini ni uminywaji wa haki, Za RAIA, WAFANYABIASHARA, WAFANYAKAZI, WANASIASA, bila kusahau VYAMA VYA SIASA..etc

Kama Taifa tukitaka kuongea Lugha moja kuhusu AMANI! Basi HAKI itangulizwe kwenye kila jambo!

Mwanamuziki PETER TOSH, aliwahi kuimba kuwa, "Everybody is crying out for peace, none is crying out for justice!"

Again, AMANI ni tunda la HAKI, kumbuka hilo!
 
Swala linakuja hapa! Unaitafsiri vipi A man I! Au haki?

Kama ukiangalia tafsiri za hayo yote kwa jicho la unazi basi ni vigumu kufikia lengo la utaifa!

Tofauti za kisiasa zinatakiwa kuwa changamoto za maendeleo na sio kikwazo!

Kama kila MTU atataka like anachotaka yeye itakua vigumu sana kufikia muafaka!

Ndio maana nasema! Maswala haya yawezaidi ya tofauti zetu za kisiasa!
 
Bila haki hamna amani. So blah blah huwa ni maneno ya ccm tu kuhadaa watu wasidai haki zao.
Swala la Utaifa limetokea Rusia, China, Uingereza na sasa Marekani!

Kila nchi inataka kurudisha hadhi yake!

Umoja wa kitaifa ndiyo Sera ya kidunia kwa sasa!

Trump katika hotuba yake Leo kasema " buy american and hire american"

Uzalendo umeshika hatamu!

Sisi tuko wapi?
 
Yaani wewe ukiwa mwanaccm hata kwenye msiba wangu usihudhurie, kamwe sitashirikiana na mwanaccm hata awe ndugu yangu!Nawezaje kushirikiana na watoto wa ibilisi/lucifer/shetani????
 
Swala linakuja hapa! Unaitafsiri vipi A man I! Au haki?

Kama ukiangalia tafsiri za hayo yote kwa jicho la unazi basi ni vigumu kufikia lengo la utaifa!

Tofauti za kisiasa zinatakiwa kuwa changamoto za maendeleo na sio kikwazo!

Kama kila MTU atataka like anachotaka yeye itakua vigumu sana kufikia muafaka!

Ndio maana nasema! Maswala haya yawezaidi ya tofauti zetu za kisiasa!
Nyie ndio hamjitambui ya kwamba haya yana umuhimu kuliko u~ccm wenu,mnakuwa radhi hata kuua na kusingizia watu ugaidi kwa tamaa yenu ya madaraka.***(acha unafiki).
 
Back
Top Bottom