Wadau, kwa hali ilivyo hivi sasa ndani ya CHADEMA ni kwamba jumuiya zao ambazo zilikuwa nyenzo muhimu ya kueneza chama za BAVICHA na BAWACHA kwa sasa ni kama zimeshakufa kifo cha mende. Na hii ni kutokana na jumuiya hizo kukosa maarifa ndani ya muungano wa UKAWA. Harakati alizoanza nazo Mwenyekiti wa BAWACHA, HALIMA MDEE kwa sasa hazipo tena. Mwenyekiti wa BAVICHA, PATROBAS naye anaonekana kushindwa kabisa kimbinu na kimkakati na hivyo kutotimiza vema majukumu yake.
Sababu kubwa ya mabaraza haya kushindwa kazi inaelezwa kuwa ni kutokana na mikakati mingi kufanywa na UKAWA hivyo viongozi hawa kujikuta wakielea hewani. Aidha, baadhi ya wachambuzi wanaeleza sababu za kushuka umaarufu kwa mabaraza hayo inatokana na viongozi waliochaguliwa hivi karibuni kwa shinikizo la Mwenyekiti kukosa weledi na maarifa ya kuendeleza jumuiya zao. Kwa sasa wamebaki kuwa bendera fuata upepo.