UKAWA yapi mmekwisha kubaliana kati ya haya?

UKAWA yapi mmekwisha kubaliana kati ya haya?

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,868
Reaction score
5,753
Habari za Jumatatu wapendwa.
Itakumbukwa kwamba Oktoba 26, 2014 , vyama vinne ; Chadema , NCCR Mageuzi , CUF NLD vilifikia makubaliano SABA ya Muungano wao ambao ni pamoja na:
1. Kuhusisha sera zao na kuchukua yote yanayofanana ili viwe na kauli Zinazolingana na kufanana kwa Watanzania.

2. Kusimamisha wagombea wa pamoja kwenye chaguzi zote kuanzia serikali za mitaa, udiwani, ubunge, uwakilishi wa urais kwa jamhuri ya Muungano na Zanzibar.

3. Kuweka utaratibu wa namna gani vyama hivyo vingeshirikiana kwenye uchaguzi wa mitaa uliofanyika Desemba 2014 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

4. Kushirikiana kuelimisha umma kupiga kura ya Hapana katika mchakato wa kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.

5. Kujenga ushirikiano wa dhati kwa mambo yote na hoja zote za msingi zenye maslahi kwa Taifa.

6. Kuulinda Muungano bila ya kuwa na migongano ya kimaslahi kama ilivyojitokeza kwenye Katiba inayopendekezwa.

7. Kuhimiza na kusimamia ushirikiano wa pmoja baina yao na asasi zingine.

Mytake: Mpaka sasa UKAWA yapi mmetekeleza kati ya hayo saba? Tumeshuhudia kwenye uchaguzi wa sm uliomalizika hivi karibuni baadhi ya vyama washirika vikiambulia patupu kabisa na kutosikika kabisa kana kwamba hawako UKAWA na maeneo mengine mfano mkoa wa pwani vyama washirika kutupiana lawama za kuhujumiana kwa maana ya kukiuka masharti ya kuachiana maeneo ya kugombea.

Kule Mtwara tumeshuhudia kiongozi wa chama kinachounda UKAWA akikiuka makubaliano kwa akimpandisha jukwaani mwanachama aliyekataliwa na chama chake. Tayari kuna vyama vimeshatangaza wawakilishi wao kwenye kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha ajenda ya kumpata mgombea mmoja wa urais kuwakilisha UKAWA ambayo ilisemekana nayo ingekuwa moja ya agenda za kikao cha kesho inaonekana kuyeyuka. Yapi mmeshatekeleza kati ya hayo Saba?
 
umesahau moja la msingi sana ambalo ni kushirikiana kupiga vita ufisadi na mafisadi pamoja na wizi wa mali ya uma ambalo hilo wanashirikiana vizuri na sisi kina gogo la shamba tunaliona hilo ndio la msingi kupita vyote
 
Ukawa mimi huwa siawaoni hata kama ni watu wa maana sana kwani sijawahi kuona kama wanahoja za msingi hata mmoja.
 
Kazi zimeonekana maana hata wewe mleta mada nidalili za kuwewesema hizo
 
Wengine lipumba na wengine slaa lipi jema katika hili.
 
TataMadiba leo hii na sidhani kama yanakuhusu, huu ni unafiki, hapo mulipo so TISS, si magamba si police munaumiza kichwa ni jinsi gani UKAWA itengane , hii ni hoja ya kitoto sana.

UKAWA ni zaidi ya uijuavyo, unayakumbuka maneno ya mzee Sabodo ktk mkutano mkuu wa NCCR?

UKAWA ni mpango wa mungu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom