UKAWA yamuhofia Zitto

UKAWA yamuhofia Zitto

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
MUUNGANIKO vya vyama vinne vya siasa unaojulikana kwa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), umeanza kumhofia Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, baada ya kumuweka mizengwe kuruhusu chama chake kujiunga katika umoja huo, TAIFA IMARA linaripoti.

Kwa sasa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kishiriki katika UKAWA, kimelazimika kuanza ziara mikoani kujaribu kuondoa sumu iliyosambazwa na kiongozi huyo wa ACT kwenye mikoa mbalimbali.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, alilazimika kuwataka wafuasi wa chama hicho kupuuza hoja zinazotolewa na Zitto juu ya kuyumba kwa CHADEMA.

Kauli hiyo ya Lema aliyoitoa kwenye moja ya Mikutano ya hadhara iliyofanyika mjini Shinyanga hivi karibuni ni muendelezo wa matamshi ya John Mnyika aliyelazimika kuwataka wafuasi wa mageuzi kupuuza mikutano ya ACT bila mafanikio.

Pamoja na vizingiti vya kupuuzwa na viongozi waandamizi wa CHADEMA, Zitto ameandika barua ya kuomba kuunganishwa katika UKAWA. Katika kulitazama kwa kina jambo hilo, endelea na makala hii ya uchambuzi wa kisiasa juu ya nini kinachoendelea.

Wahenga walinena, "Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu," na msemo mwingine, "kidole kimoja hakiui chawa," misemo hii inahamasisha umoja katika kutenda jambo ili kuleta manufaa. Kauli kama hizi ndizo zilizosababisha vyama vya upinzani kuungana kujenga nguvu ya pamoja itakayowasaidia kupambana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichosheheni mizizi katika kila ngazi.

Cha kushangaza umoja huu unasitasita kukikubali chama kipya cha ACT- Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Zuberi Kabwe mwenye cheo cha Kiongozi Mkuu ingawa chama kina Mwenyekiti, Katibu na viongozi wengine kadha wa kadha waandamizi. Hata hivyo, muundo wa kuwa na Kiongozi Mkuu wa Chama hutumiwa na vyama vya kikomonisti.

Swali ni kwanini UKAWA (UKAWA ni kifupisho cha maneno Umoja wa Katiba ya Wananchi) wanamuogopa Zitto na chama chake cha ACT Wazalendo?

Zitto Kabwe ni miongoni mwa wanasiasa vijana machachari waliowahi kuleta ladha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mtu pekee aliyemuibua mwanasiasa huyu ni mzee wa kasi na viwango Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta katika Bunge la Tisa wakati alipokuwa Spika wa Bunge.

Sitta aliwapa wapinzani uhuru mkubwa wa kuwakilisha mawazo yao na kuwaunga mkono wapinzani wenye hoja zenye kutetea maslahi ya wananchi. Zitto alikuwa miongoni mwa wabunge wa CHADEMA walioweza kujijengea sifa na kuaminika kwa wananchi kama wawakilishi wazuri wa upande wa upinzani wanaoweza kuwashtua baadhi ya mawaziri ili wawajibike ipasavyo katika wizara zao wanazozisimamia.

Kwa upande wa UKAWA ni muunganiko wa vyama vya kambi ya upinzani ambao waliungana wakati wa mchakato wa rasimu ya Katiba kwa kigezo cha kuwawakilisha wananchi. Umoja huo unaendeleza jina hilo ukiwa na nia ya kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais kwa tiketi ya vyama vya upinzani.

CHADEMA ilimvua uanachama aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto kwa madai ya kukiuka Katiba ya chama hicho. CHADEMA ipo ndani ya UKAWA na Zitto alionekana mtu asiyefaa kwenye chama. Hizi ni baadhi ya sababu za UKAWA kumuogopa Zitto na chama chake cha ACT wazalendo.

Chanzo: TAIFA IMARA
 
Habari ya mjini hivi sasa ni fainali kati ya Juventus Vs Barcelona.

Zitto na ACT ishakuwa zilipendwa.

Au una jipya zaidi??

Kama vipi tupe japo la Nkurunzinza.

Una akili kwelikweli wewe.
 
Nadhani hiyo habari ingelikuwa imeandikwa na raia mwema bavicha wengianza kusema kuwa hilo ni gazeti la kufungia vutumbua .haitahivo inashangaza sana kwa nin hilo gazeth limeandika mazuri kuhusu zitto
 
Nadhani hiyo habari ingelikuwa imeandikwa na raia mwema bavicha wengianza kusema kuwa hilo ni gazeti la kufungia vutumbua .

Ila kwa kuwa imeandikwa na Uwazi, hili gazeti ni la serikali.
 
Habari ya mjini hivi sasa ni fainali kati ya Juventus Vs Barcelona.

Zitto na ACT ishakuwa zilipendwa.

Au una jipya zaidi??

Kama vipi tupe japo la Nkurunzinza.

Zitto aliwashika sehemu nyeti lazima wamuogope, lakini ni kwaida hata ukitongoza demu lazima alinge kidogo baadaye anachia mzigo kiulaini kabisa unajichapia unavyotaka
 
Una akili kwelikweli wewe.

Hahahahaha umejuaje? Nna akili kumzidi Erick Shigongo.

Ndo maana nataka hii hadithi aloileta huyu mkuda iwekwe front page kwenye gazeti la Ijumaa Wikienda...
 
Zitto aliwashika sehemu nyeti lazima wamuogope, lakini ni kwaida hata ukitongoza demu lazima alinge kidogo baadaye anachia mzigo kiulaini kabisa unajichapia unavyotaka

Hahahahaah ushasahau anayeshika sehemu nyeti ni demu, wakati akitaka kusikilizia utamu wa koni. Hakyamama jamaa ana akili kama Wema Sepetu.
 
Zito Angejiunga Na Ukawa Mwakani, Au Ameona Ukawa Inaenda Ikulu?, Tatzo Lake Kubwa Anataka Uongozi Wa Juu ,hivyo Hata Akija Ukawa Atataka Awe Mw/kiti Wa Ukawa. Hapo Umakini Unahtjka.
 
Kwi kwi kwi kwi lol! Kwanza UKAWA ni genge la Wasaka tonge, baadaye wakaandika barua ili wakubaliwe kujiunga na Wasaka tonge sasa UKAWA inamuogopa nanihii!!! Mtabadili sana single zenu mwaka huu bahati mbaya wanunuzi machale yamewacheza single zenu hazichezeki wala hazisikiliziki. MRIE TU! Wananihii wakubwa nyie. By the way milioni 700 ni aje cheque nasikia imekuwa NSF Hahahahaha lol!
 
Hivi Zitto ana akili kweli?
Leo Hi ajiunge na wasaka tonge?
 
Last edited by a moderator:
Hata ingekuwa wewe, mtu amekusali, labda kakuchukulia hata mkeo, anapotaka kurudisha urafiki wa hata kuja kwako usimuogope? Zito akitaka ushirika na Chadema asubiri uchaguzi upite, kisha tutaenda naye taratibu.
 
Habari ya mjini hivi sasa ni fainali kati ya Juventus Vs Barcelona.

Zitto na ACT ishakuwa zilipendwa.

Au una jipya zaidi??

Kama vipi tupe japo la Nkurunzinza.

Juventus lazima wakae
 
Habari ya mjini hivi sasa ni fainali kati ya Juventus Vs Barcelona.

Zitto na ACT ishakuwa zilipendwa.

Au una jipya zaidi??

Kama vipi tupe japo la Nkurunzinza.

afadhali umeliona hilo mzee wa "mikonooozz" - huu tunauita uandishi aina ya chanjila

Mleta hoja hana kipya zaidi ya speculations za kitoto.... Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuogopa na kuepuka. ACT ni kitu cha kuepukwa kama michepuko ya kona bar
 
Juventus lazima wakae
Hata Mungu anapenda iwe hivyo... hakyamama..

afadhali umeliona hilo mzee wa "mikonooozz" - huu tunauita uandishi aina ya chanjila

Mleta hoja hana kipya zaidi ya speculations za kitoto.... Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuogopa na kuepuka. ACT ni kitu cha kuepukwa kama michepuko ya kona bar
Kaka michepuko ya kona bar siyo ya kuepukwa bali ya kukimbia, cha kuepukwa Dar ni mvua na mafuriko yake.
 
Kaka michepuko ya kona bar siyo ya kuepukwa bali ya kukimbia, cha kuepukwa Dar ni mvua na mafuriko yake.

Swadaktaaaa... basi ndivyo hivyohivyo UKAWA wanatakiwa kukimbia kabisa ACT na makandokando yao yote
 
Leo ndo unaiona hiyo habari??

Kwali ni gazeti la kufungia maandazi, habari ya siku nyingi
 
Back
Top Bottom