UKAWA yameguka Handeni, Wanachama 115 wahamia CCM

UKAWA yameguka Handeni, Wanachama 115 wahamia CCM

Kansigo

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
2,670
Reaction score
2,156
Wanachama 115 wa CHADEMA na CUF wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, wamejiunga na CCM kwa madai kuwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umeshindwa kuelewana hadi kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Wakirudisha kadi na bendera juzi mbele ya Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tanga, Mathew Mganga walisema walikuwa na nia ya kweli ya kuunga mkono UKAWA unaoundwa na vyama vyao lakini kutokana na kutokuwa na msimamo wameamua kuhama.

Katibu wa CHADEMA Kata ya Kwenjugo, Rajabu Vuli, alisema alifanya hamasa kuhakikisha chama chao kinapata ushindi lakini viongozi wa wilaya hawakuonyesha ushirikiano na watu wa chini.

Mwingine aliyehama ni Katibu wa Vijana wa CHADEMA wa kata hiyo, Ramadhani Dawa.

Dawa alisema ahadi zisizotimia za viongozi ikiwamo kuwadharau viongozi wa kata ndiyo sababu kubwa iliyosababisha kuhamia CCM.

Alisema kama wasingedharauliwa na mawazo yao kufanyiwa kazi wangebaki CHADEMA na kukiendeleza chama hicho ambacho amedai kimekuwa na mvuto mkubwa na Watanzania ambao walitaka kuleta mabadiliko ya kweli.
 
hadi 2017 sioni kama kutakuwa na kitu kinachoitwa ukawa, wamepotana kabisa
 
Ukawa hawajui hata ni kitu gani wanafanya ...wapo wapo tu.
 
kama ni hao ukawa a.k.a ukiwa waende tu. tunahitaji upinzani imara na sio huo upinzani wa wapiga dili. upuuzi kabisa
 
Oooooh ahsante kumbe anajua kina mvuto mkubwa bas ajue hatutkshik aliondika slaaaa sebuse hao kupe
 
2017 urudi hapa kuyashuhudia haya unayoyasema


wakati wa kampeni mlisema ccm tutakimbia humu ndani kwa bahati mbaya ni nyie mliokimbia kwa wingi humu ndani watu kama wakina nifah wanakuja kwa kuchungulia na kukimbia
 
wakati wa kampeni mlisema ccm tutakimbia humu ndani kwa bahati mbaya ni nyie mliokimbia kwa wingi humu ndani watu kama wakina nifah wanakuja kwa kuchungulia na kukimbia

UKAWA tumekomaa kisiasa tunajua kutenga nyakati, nyakati za kampeni na uchaguzi zimeisha sasa tunasonga mbele kujenga nchi. Tunawashangaa nyie mnahisi bado tuko kwenye kampeni kila siku chokochoko na mipasho kama mstaafu
 
Back
Top Bottom