UKAWA wawatunishia misuli CCM

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
SERA ya ubabe inayotekelezwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) inakwaza demokarasia nchini, anaandika Happiness Lidwino.

Ukawa sasa wamesusa kushiriki chaguzi ama vikao vya wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) kutokana na CCM kukiuka taratibu za kuwachagua viongozi wa ALAT.

Uamuzi huo umetokana na kikao cha juzi kilichofanyika katika ukumbi mpya wa CCM Dodoma cha kuwachagua viongozi hao ambapo umevurugwa kutokana na taratibu kukiukwa.

Akizungumza na mtandao huu, Boniface Jacob, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam ambaye alishiriki kikao hicho amesema, msimamo huo wa kutojihusisha na ALAT ni wa Ukawa.

Amesema wamefikia hatua hiyo kwa kuwa Serikali ya CCM haitambui wala kuthamini uwepo wa Ukawa licha ya kukubalika kwa wananchi.

Jacob amesema, katika mkutano huo ambao ulifanyika juzi na kuwashirikisha wajumbe ambao ni wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri zote, mameya wa miji na majiji na mbunge mmoja kutoka kila Mkoa wa Tanzania Bara, wao hawakutendewa haki kwa kutoshirikishwa katika baadhi ya maandalizi ya mkutano huo.

“Kwa upande wetu hatukushirikishwa tarehe ya kuchukua fomu wala kurudisha fomu ambapo nafasi za kugombea zilikuwa ni nafasi ya mwenyekiti, makamu wake na wajumbe 16 wa kamati ya utendaji. Tulikua hatujui kinachoendelea, tulishangaa tulipofika ndani ya ukumbi majina ya wagombea yanatajwa,” amesema.

Amesema, katika majina ya wagombea yaliyotajwa na mgombea wetu wa uenyekiti alikuwepo bila yeye kuwa na maandalizi yoyote, huku Cleophas Manyangu, Mwanasheria wa ALAT akisema wagombea wa kutoka Ukawa hawajakidhi vigezo waliokidhi ni wa CCM tu,” amesema Jacob.

Jacob amesema, Manyangu aliwataja waliochukua na kurejesha fomu za kugombea uenyekiti ni Gulam Mukadam (Meya wa Shinyanga), Murshid Ngeze (Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Vijijini).

Wengine ni Chief Kalumuna (Meya wa Bukoba Mjini) na Isaya Charles (Meya wa Jiji la Dar es Salaam) ambapo anasema Mwita hakuwa amejiandaa kutokana na kuchelewa kupata taarifa ya uchaguzi huo.

Pia mwanasheria huyo alisema wasiotimiza vigezo ni Mwita na Kalumuna ambao walishindwa kurejesha fomu katika muda uliowekwa ambao ilikuwa saa 6.00 mchana siku moja kabla ya uchaguzi na pia hawakupata wadhamini 10 kutoka kanda tano za ALAT Taifa.

Kutokana na kauli ya mwanasheria huyo, mwenyekiti wa muda wa mkutano huo ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jaffar Mwanyemba alitangaza kuwa wagombea katika uchaguzi huo ni wawili.

Kauli hiyo ilibadilisha hali katika ukumbi, huku wajumbe wa Ukawa wakitaka wagombea wote waruhusiwe kuingia katika kinyang’anyiro hicho.

Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro aliomba wagombea hao waruhusiwe kwa kuwa maandalizi ya uchaguzi yalikiuka mwongozo, hali ambayo ilifanya baadhi yao kutokidhi vigezo akiwemo Mwita.

Amesema, taarifa ya mkutano huo ilitakiwa kuwafikia siku zisizopungua 28 kabla ya uchaguzi, lakini wengi wao walipata barua hizo chini ya muda huo.

Manyangu ameuambia mtandao huu taarifa za mkutano huo kwa mara ya kwanza zilipelekwa kwenye halmashauri Novemba 2, mwaka jana.

“Tatizo lililotokea ni baadhi ya halmashauri kuchelewa kukamilisha uchaguzi, hali iliyosababisha mkutano kuahirishwa mara mbili,” amesema.

Baada ya hoja hizo, wajumbe wote wanaotokana na Ukawa walitoka nje ya ukumbi, huku wakiahidi kufanya kazi na Serikali Kuu pekee.

Akizungumza kwa njia ya simu Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam amesema kutokana na kuchelewa kwa uchaguzi jijini humo, hakupata taarifa mapema kuhusu mkutano na uchaguzi huo hivyo hakujiandaa.

Maulid Mtulia, Mbunge wa Kinondoni (CUF) amesema, “anaunga mkono uamuzi wa Ukawa kwa kuwa uchaguzi ule haukuzingatia sheria na haki kwa hivyo ni maamuzi mazuri ili serikali ijifunze.”

Amesema, licha ya kuwa kujiondoa kwa Ukawa katika vikao vya ALAT kuna athari kubwa lakini Ukawa wametoa funzo kwa serikali ili iache kuwapuuza viongozi wake.

“Lengo letu Ukawa ni kushirikiana lakini wenzetu wanatumia ubabe katika kila hatua. Tutafanya kazi kwa kushirikiana na serikali kuu na malengo yetu kwa wananchi yatatimia lakini si kushirikiana tena na ALAT kwani haiko tayari kushirikiana nasi,” alisema Mtulia.

Licha ya Ukawa kususia uchaguzi huo na kutoka nje, CCM walijipigia kura wenyewe na kuwatangaza washindi kuwa ni Gulam aliyeshinda uenyekiti kwa kura 179 dhidi ya 97 alizopata mshindani wake huku kura tano zikiharibika kati ya kura halali 276.

Kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti alipa Steven Muhapa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa aliyepata kura 152 kati ya kura halali 276.


Chanzo:Mwanahalisi Online
 

Attachments

  • IMG-20160407-WA0096.jpg
    IMG-20160407-WA0096.jpg
    106.9 KB · Views: 65
  • IMG-20160407-WA0095.jpg
    IMG-20160407-WA0095.jpg
    93.9 KB · Views: 51
  • IMG-20160407-WA0094.jpg
    IMG-20160407-WA0094.jpg
    61.3 KB · Views: 51
  • IMG-20160407-WA0093.jpg
    IMG-20160407-WA0093.jpg
    110.2 KB · Views: 36
Hii nchi Ni ngumu sana kuwa mpinzani.....yani huwez tofautisha viongoz WA umma na viongozi WA chama, jumuia ya umma na jumuia ya CCM........so hard for opposition to grow.....democracy ya maneno ndo inatawala .
 
Pia mwanasheria huyo alisema wasiotimiza vigezo ni Mwita na Kalumuna ambao walishindwa kurejesha fomu katika muda uliowekwa ambao ilikuwa saa 6.00 mchana siku moja kabla ya uchaguzi na pia hawakupata wadhamini 10 kutoka kanda tano za ALAT Taifa.

Kimewaponza kutokujua sheria au kutozingatia sheria.UKAWA wana wanawasheria koko ambao hawawasaidii
 
ukawa wanaleta siasa kwenye issues serious za maendeleo. sio kila jambo mtufanyie siasa zenu. mnakera sana nyie ma ukawa.
 
Ifike mahali sasa wapinzani wawe kama wehu, MTU akileta ujinga anapigwa Ngumi ya pua hapo hapo! Kwa mfano huyu Manyangu aliatahili kupewa ngumi nzito ya pua!
 
Ni vizuri kuwaachia maCCM wafanye siasa za kuendesha nchi kibabe. Wakikua wataacha
 
Na Juzi jamaa kaenda kujifunza kwa Kagame jinsi ya kuwapoteza.... mmekwisha... kuwadiscourage ni njia kuu iliyobakia mkisusa ndio mnapotea vizuri mkenge huo kaingia lowassa, Maalim sasa nchi Shwali.... kilichobakia ni kuwaminya kila mtakapo kuwa mnaamka....

Ila Kumbukeni Ule Msemo waliosema Wahenga.... Mkisusa wenzio Wala....
 
Na Juzi jamaa kaenda kujifunza kwa Kagame jinsi ya kuwapoteza.... mmekwisha... kuwadiscourage ni njia kuu iliyobakia mkisusa ndio mnapotea vizuri mkenge huo kaingia lowassa, Maalim sasa nchi Shwali.... kilichobakia ni kuwaminya kila mtakapo kuwa mnaamka....

Ila Kumbukeni Ule Msemo waliosema Wahenga.... Mkisusa wenzio Wala....
Msipige kelele pia pindi mataiga ya nje yanapowapa dozi
 
Halafu rais anajinadi majukwaani yeye ni rais wa wote, akiingi kanisani anapiga goti na kufunga macho eti anamuomba Mungu aongoze vyema watanzania? Khaaa, si aseme tu yeye ni rais wa wana ccm, na Mungu amuongoze vyema kuitumikia ccm? Hajui kuwa Mungu si shemeji eee, haya wacheze tu na sharubu za simba.
 
Back
Top Bottom