UKAWA Watuombe radhi Watanzani

Jun 11, 2015
5
2
Wanajukwaa, nimeshuhudia sarakasi za ukawa bungeni kwenye uteuzi wa kamati. Haiingii akilini kwa mtu kwenye akili timamu aliyeichagua UKAWA Leo anaambiwa mbunge wa Ukawa hana kiwango cha kuwa kwenye kamati ya PAC na LAAC. Ukawa watuombe radhi wapigakura kwa kutuletea wagombea wasio na viwango na kutuaminisha ktk mabadiliko hewa!
 
TBS sijui ilivamiwa na akina nani mkuu. Maana sielewi kabisa. Kipindi kile tuliaminishwa ni "majembe" leo tunaambiwa hawana kiwango! Anyway 2020 si mbali!!
 
Ukawa wanafiki sana aisee.

Kuna baadhi ya wabunge wanajiona wao bora sana kuliko wenzake hasa yule Mwenye elimu ya hapa na pale, kigeugeu na safisha mafisadi.
 
Ni matunda ya watu ndani ya ukawa kujiona kuwa wao ndiyo kila kitu. Iweje waseme mbunge nwenzao hawa uzoefu au kiwango?

Akina Tundu Lissu walianzia wapi hadi wakaaminika? Kwa nini hao wengine wasiweze? La msingi wawape ushirikiano wenzao ili kupanua uwezo wa wabunge wa upinzani
 
Hii kitu imenisikitisha sana, na imenikumbusha animal farm, pale nguruwe walipojiona wana akili na ni werevu kuliko wanyama wote. mwisho wa siku wakapindua sheria zote hata ile sheria mama: ALL ANIMALS ARE EQUAL, BUT SOME ARE MORE EQUAL THAN OTHERS
Mi nafikiri watambue kuwa kwanza wote ni wabunge, na hakuna mbunge bora kuliko mwingine
Pili, kamati zote ni kamati za bunge, sioni haja ya mchora ramani kumdharau mpaka rangi; au mwashi kumdis reseramala wakati wote wanajenga jengo hilihilo
 
Mwandishi wa mada hii kaonyesha ni kwa kiasi gani alivyo na weledi "finyu". Vyama vya siasa huwakilisha orodha ya Wagombea wake tume ya uchaguzi kwa ajili ya kuona kama wana vigezo. Tume ikikupitisha basi una vigezo.

Pengine kwa tafsiri yako wewe mtu kuwa JEMBE lazima awe na Vyeti vya PhD au awe profesa. Lakini tambua tuna "formal" education na "infomal" education,hivyo vigezo walivyokosa ni vipi? Maana hujavieleza bayana zaidi ya kujitambulisha kama mtu "mwenye kuripoti udaku".
 
Wanajukwaa, nimeshuhudia sarakasi za ukawa bungeni kwenye uteuzi wa kamati. Haiingii akilini kwa mtu kwenye akili timamu aliyeichagua UKAWA Leo anaambiwa mbunge wa Ukawa hana kiwango cha kuwa kwenye kamati ya PAC na LAAC. Ukawa watuombe radhi wapigakura kwa kutuletea wagombea wasio na viwango na kutuaminisha ktk mabadiliko hewa!
ungekuwa na akili timamu ungemtaka alie tuita malofa na mbumbumbu watanzania atuombe radhi kwanza,hapo unaonyesha kwamba wewe ni mjinga kati ya wajinga
 
Mkapa hapaswi kuomba radhi bali anastahili kupongezwa maana maamuzi yalikuwa ya kipumbavu na yaliamriwa na nyumbu.Akili timamu haziwezi kwa miaka kumi kujua nani atakuwa mgombea wao. Je CCM wangempisha mliyempokea mngefanyaje. Ni nyumbu tu wanaofuata aliyetangulia hata kama kazama. Hoja iliyomezani mnawakataaje wabunge wenu wenyewe.
 
Mwandishi wa mada hii kaonyesha ni kwa kiasi gani alivyo na weledi "finyu". Vyama vya siasa huwakilisha orodha ya Wagombea wake tume ya uchaguzi kwa ajili ya kuona kama wana vigezo. Tume ikikupitisha basi una vigezo.

Pengine kwa tafsiri yako wewe mtu kuwa JEMBE lazima awe na Vyeti vya PhD au awe profesa. Lakini tambua tuna "formal" education na "infomal" education,hivyo vigezo walivyokosa ni vipi? Maana hujavieleza bayana zaidi ya kujitambulisha kama mtu "mwenye kuripoti udaku".

Sasa haya maelezo yote njoo uje kuwauliza UKAWA, kwa nini wanakataa baadhi ya wabunge wao eti hawana uwezo? Ni dhaifu sana hawafai kuwemo katika kamati ya PAC au LAAC
 
Anza kutoa boriti kwanza kwa jicho lako mpuuzi wewe, tuombeni radhi kwa kuwabagua Machotara, tutakeni radhi kwa kuwabagua wa kaskazini, tutakeni radhi kwa kuifanya nchii hii kuwa Mali yenu, tutakeni radhi kwa kutubagua kwa rangi zetu, kabila zetu Na dini zenu, tumbili wewe
 
Watu wanatofautiana katika namna ya kufuatilia na kupenda mambo,unapotafuta utendaji wa uhakika katika kamati bila kuingiza siasa uchwara inapasa kuzingatia ubobezi na historia ya mhusika katika kufatilia swala husika.
ndomana mkuu aliwateuwa watu mahiri akawapa ubunge na Kisha uwaziri kwa kuzingatia umahiri wao. Kwanini hakuteuwa mbunge yeyote kuwa waziri wa fedha ama elimu? Ni welewa mdogo kudhani aliwadharau wabunge wooote wa chama chake hadi kuteuwa mtu toka nje.
kwakweli hii hoja ya kazi tuu tutachelewa,kunawatu majungu,fitna na mipasho iko damuni.
 
Wanajukwaa, nimeshuhudia sarakasi za ukawa bungeni kwenye uteuzi wa kamati. Haiingii akilini kwa mtu kwenye akili timamu aliyeichagua UKAWA Leo anaambiwa mbunge wa Ukawa hana kiwango cha kuwa kwenye kamati ya PAC na LAAC. Ukawa watuombe radhi wapigakura kwa kutuletea wagombea wasio na viwango na kutuaminisha ktk mabadiliko hewa!
Mhhhh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom