Zimebaki siku chache za kampeni. Mgombea wa‪ CCM, ‎Dr Magufuli ameonyesha uimara wake kila siku tofauti na mgombea wa UKAWA - ambaye anaonekana amechoka, yuko hoi balaa.
CCM kupitia Magufuli imekamilisha kampeni zake zaidi ya- Mikoa 21 na Wilaya 120, ukiachia mbali stop-overs za kumwaga huko njiani. Magufuli amekuwa akitoa hotuba zenye kuleta matumaini mapya ya‪ Tanzania tuitakayo tofauti na Lowasa ambaye amehahaa tu na hata majimbo yote anakopita- hamalizi kutokana na afya yake.
Kwenye kampeni hakuna kitu cha maana zaidi ya wapiga kura kujihisi wanakusikia wewe mwenyewe ukiwapa ahadi za kuboresha hali zao za maisha. Personal connection is very important kwenye kampeni. Ukifanya mikutano michache, ama usipofanya, kwa kiasi kikubwa unajipunguzia kura zako mwenyewe tu.
UKAWA hawafanyi kampeni, kazi yao kutoa vitisho na kutia wananchi shaka ya kuwa wataibiwa kura, hivi nani atahangaika kuwaibia kura ambazo hawana tofauti na kulalamika kila kukicha?
Hivi kweli chama kina wagombea ubunge 138, kina migogoro na wagombea wa CUF kwenye majimbo zaidi ya 50, kitashindaje sasa? Wabunge wote mashuhuri wa vyama vyao hawana muda na kumuuza mgombea Urais, wanakomaa na kampeni zao majimboni japo pia wameshikwa vibaya na wagombea mahili wa CCM, hali si shwari kabisa.
Lowassa anahaha mtaani na-‪ makapi-toka CCM. Makapi yenyewe hayana mvuto wowote kwa jamii basi tu ilimradi wanamtia moyo kamanda wao anayetoa hotuba za dakika 5 tu.
Sasa watashindaje? Hawa kwa hakika wamejihakikishia kushindwa tu, hakuna namna nyingine!