UKAWA wakishindwa nani ataweza?

UKAWA wakishindwa nani ataweza?

kensh

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2012
Posts
527
Reaction score
113
Siasa za mwaka huu ni kali, tena sana. Utamu na ukali wake umenogeshwa na mambo matatu hasa.moja ni jambo ambalo watanzania walikua wakisema sana kuwa vyama vya upinzani vikiungana ndipo vitaweza kuitoa ccm ikuli,hilo limetokea mwaka huu. Pili ni ile hali ambayo haikuzoeleka ya wana ccm wakubwa kama lowasa,sumaye na wengineo kuhama ccm na kuenda upinzani,hilo limetokea na kunogesha siasa za mwaka huu. Tatu ni jinsi wagombea wa urais toka ccm na yule wa ukawa walivyo na nguvu ktk jamii,woote wanakubalika na ni vigumu kusema nani ni zaidi ya mwingine,hapo ndipo utamu unakolea zaidi na zaidi.

Najiuliza tu, je, ukawa wakishindwa kuitoa ccm madarakani mwaka huu,nani au chama gani kitakuja kufanikiwa? Au hilo litamaanisha hakuna upinzani mioyoni mwa watanzania na hivyo upinzani utaparaganyika?
 
Ukweli ni kuwa CCM haiwezi kushinda Uchaguzi huu! Swali la Msingi ni kuwa CCM wakibaka Uchaguzi watahimili vishindo vya nguvu ya Umma kwa muda gani?
 
Walishasema Ushindi ni lazima, hii inaamisha kuwa maamuzi ya wananchi hayatakuwa na nafasi...
 
ccm wana akili ya kujiongeza ndio maana awashindwi kizembe
 
Siasa za mwaka huu ni kali, tena sana. Utamu na ukali wake umenogeshwa na mambo matatu hasa.moja ni jambo ambalo watanzania walikua wakisema sana kuwa vyama vya upinzani vikiungana ndipo vitaweza kuitoa ccm ikuli,hilo limetokea mwaka huu. Pili ni ile hali ambayo haikuzoeleka ya wana ccm wakubwa kama lowasa,sumaye na wengineo kuhama ccm na kuenda upinzani,hilo limetokea na kunogesha siasa za mwaka huu. Tatu ni jinsi wagombea wa urais toka ccm na yule wa ukawa walivyo na nguvu ktk jamii,woote wanakubalika na ni vigumu kusema nani ni zaidi ya mwingine,hapo ndipo utamu unakolea zaidi na zaidi.

Najiuliza tu, je, ukawa wakishindwa kuitoa ccm madarakani mwaka huu,nani au chama gani kitakuja kufanikiwa? Au hilo litamaanisha hakuna upinzani mioyoni mwa watanzania na hivyo upinzani utaparaganyika?

Type picha ya UKAWA wakishinda.
 
swali ni je ukawa wakishindwa kuitoa ccm ,nani mwingine ataweza kuula mfupa huo ?
 
CCM itapungukiwa na kura ukilinganisha na Chaguzi zilizopita, Kama tunapaswa kuchagua Chama basi Chadema inafaa, kama tunapaswa kuchagua Mtu basi Magufuli anafaa
 
Ukweli ni kuwa CCM haiwezi kushinda Uchaguzi huu! Swali la Msingi ni kuwa CCM wakibaka Uchaguzi watahimili vishindo vya nguvu ya Umma kwa muda gani?

Eti nguvu ya umma Tz kuna nguvu ya umma hahahaaa
 
Back
Top Bottom