UKAWA waiteka CC ya CCM

UKAWA waiteka CC ya CCM

CCM hiyo hiyo inajua kima cha chini ni shs 270,000 na bado inaamua kulipa kundi fulani posho ya 300k. Kawaida ya mawazo ya ccm ni upside down.

Kama wako tayari kuingia msituni aisee, that's good; Mungu anaweza akawageuza wakawa nyani na kutokomea hukohuko!
Ngoja tumuombe Mungu awaharakishe kukimbilia msituni!

Wakifika msituni wageuzwe tembo na Komba awe dume pekee!Kinana abaki akichunga tembo wake!
 
Kukubali serikali mbili ni kama paka kuvaa mkufu wa dagaa shingoni mwake! Haiwezekani kwa viongozi waliopo sasa.

Hahahaaaa, Stoics? Hawa viongozi wetu wa sasa ni hatari kweli, hata upige filimbi hawasikii, ngoma hawachezi, mkilia hawaombolezi, wana macho lakini hayaoni, pua lakini hazinusi, masikio lakini hayasikii, midomo lakini ...... Full drama and political gimmicks!
 
CCM mtakubali tu na mtaelewa ya kuwa hii nchi si mali yenu
 
Mhe kwa utaratibu duniani kote kwa maamuzi makubwa mfano uundwaji wa katiba inatakiwa 2/3 na nchi zingine kama marekani wamefikia 3/4, wakisema simple majority itakuwa ni muendelezo wa maajabu tanzania!!ila kwa ccm siwezi kuwashangaa walishafika ukomo wa kufikiri.

Mkuu hoja ya kubadili katiba tokea zamani,na hata kwenye katiba inayutumika sasa , ambayo iliandikwa na CCM enzi ya chama kushika hatamu, ilihalalisha 2/3 kutoka kila upande wa muungano.Hivyo kuwatukana ccm bila kufanya research ni kuwaonea.
 
Kama ccm wataenda msituni kukataa serikari Tatu basi Watakuta mwenyeji wasssira akiwa kingkong na huyu baba lulu akiwa kipara makregan. NA look v atakuwa fifi
 
Mkuu hoja ya kubadili katiba tokea zamani,na hata kwenye katiba inayutumika sasa , ambayo iliandikwa na CCM enzi ya chama kushika hatamu, ilihalalisha 2/3 kutoka kila upande wa muungano.Hivyo kuwatukana ccm bila kufanya research ni kuwaonea.
Mhe samahani kama nimetumia lugha kali,tatizo maneno mengine unapoyasikia yanakera,utafikiri hii nchi wengine ni wapangaji!!na hawana haki ya kushiriki kutoa mawazo yao,binafsi nakereka na siasa za hovyo!!fikiria mtu anasema kama serikali 2 zisipopita anaingia msituni mara jeshi litachukua nchi zikipita serikali 3,watu wanaongea maneno ya ajabu hawachukuliwi hatua hata tu wakuu kukemea!!tumekua taifa la ajabu na ndiyo maana nikasema ccm wamefika ukomo wa kufikiri!!tunacheza na viberiti petrol station wenye dhamana ya nchi ndiyo wanashangilia!!
 
Hapa watakachokuwa wamekubaliana ni kukimbilia kubadili sheria ya mabadiliko ya KATIBA.Mambo ya 2/3 yatabadishwa soon before AUGOST.
 
Mhe samahani kama nimetumia lugha kali,tatizo maneno mengine unapoyasikia yanakera,utafikiri hii nchi wengine ni wapangaji!!na hawana haki ya kushiriki kutoa mawazo yao,binafsi nakereka na siasa za hovyo!!fikiria mtu anasema kama serikali 2 zisipopita anaingia msituni mara jeshi litachukua nchi zikipita serikali 3,watu wanaongea maneno ya ajabu hawachukuliwi hatua hata tu wakuu kukemea!!tumekua taifa la ajabu na ndiyo maana nikasema ccm wamefika ukomo wa kufikiri!!tunacheza na viberiti petrol station wenye dhamana ya nchi ndiyo wanashangilia!!

Mimi nilidhani unajibu hoja yangu juu yauwepo wa 2/3s .Lakini maelezo yako yameegemea kwenye uchungu ulionao,ambao mimi katika kuchangia hoja sikusema lo lote.
 
Nimekuelewa mkuu,asante.
 
Jana,mjini Dodoma,kilifanyika kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC ya CCM) chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CCM. Mkutano huo,kwa mujibu wa mtoa taarifa aliyekuwepo ndani ya kikao hicho,ulipokea Taarifa Rasmi ya Ziara zilizofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana na timu yake katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Pia,kikao hicho kilipokea Mapendekezo ya Kamati Maalum ya Wataalamu waliopewa kazi ya kushauri cha kufanya katika hali ya sasa ya kisiasa nchini hasa katika suala la Katiba mpya. Taarifa zote mbili zliwasilishwa kikaoni na Katibu Mkuu wa CCM. Hatahivyo,kulikuwa na mambo mbalimbali mengineyo kama utendaji wa UVCCM,Umoja wa Wazazi,Umoja wa Wanawake na Idara mbalimbali za kichama na masula ya kifedha.

Katika kikao hicho kilichoisha usiku 'mnene',Umoja wa Ktiba ya Wananchi almaarufu kama UKAWA uliteka kikao hicho. " Ajenda zote zilimezwa na kujadili kuhusu UKAWA na jinsi ya kufanya mambo ya Katiba mpya yaliyokwama yasonge mbele|" alisema mmoja wa Wajumbe wa CC anayetokea Tanzania Bara. "Majadiliano yalikuwa moto sana.Mwisho wa yote, CC imetoa maagizo kwa Sekretarieti namna ya kukwamua suala la Katiba" aliongeza Mjumbe huyo bila ya kutaja maagizo yaliyotolewa.

Kuna kila dalili,CCM kuachana na msimamo wake wa Serikali mbili ili kusonga mbele kama Taifa katika kuimarisha Muungano kwa kuwa na Serikali tatu.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Are you serious?Maana nazikumbuka sentensi nyingi wakati ule tukiwa tunaangalia Ze-Comedy iliyoisha 25/April/2014.Na mwingine akasema ataingia msituni,na huyu Lukuvi naye,mh! Sijui labda wawe wamepata wakovu wakaokoka na kutubu dhambi yao ya UBAGUZI.
 
Ccm chama cha kicha machambaz hawa ni majambazi na wahun wa hii nchi kwanza lichama hili halina usajili wa kudumu,
Mtu yeyote alioko ccm hana akil na wote majambaz kwl

Aisee, umekasirika kwelikweli mpaka maneno hayatamukiki ipasavyo!!...Pole sana
 
Jana,mjini Dodoma,kilifanyika kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC ya CCM) chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CCM. Mkutano huo,kwa mujibu wa mtoa taarifa aliyekuwepo ndani ya kikao hicho,ulipokea Taarifa Rasmi ya Ziara zilizofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana na timu yake katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Pia,kikao hicho kilipokea Mapendekezo ya Kamati Maalum ya Wataalamu waliopewa kazi ya kushauri cha kufanya katika hali ya sasa ya kisiasa nchini hasa katika suala la Katiba mpya. Taarifa zote mbili zliwasilishwa kikaoni na Katibu Mkuu wa CCM. Hatahivyo,kulikuwa na mambo mbalimbali mengineyo kama utendaji wa UVCCM,Umoja wa Wazazi,Umoja wa Wanawake na Idara mbalimbali za kichama na masula ya kifedha.

Katika kikao hicho kilichoisha usiku 'mnene',Umoja wa Ktiba ya Wananchi almaarufu kama UKAWA uliteka kikao hicho. " Ajenda zote zilimezwa na kujadili kuhusu UKAWA na jinsi ya kufanya mambo ya Katiba mpya yaliyokwama yasonge mbele|" alisema mmoja wa Wajumbe wa CC anayetokea Tanzania Bara. "Majadiliano yalikuwa moto sana.Mwisho wa yote, CC imetoa maagizo kwa Sekretarieti namna ya kukwamua suala la Katiba" aliongeza Mjumbe huyo bila ya kutaja maagizo yaliyotolewa.

Kuna kila dalili,CCM kuachana na msimamo wake wa Serikali mbili ili kusonga mbele kama Taifa katika kuimarisha Muungano kwa kuwa na Serikali tatu.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Cc chama, MwanaDiwani, Nguruvi3, Mag3

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
wakuu mbona kila posta ya vuta-nikuvuta L7 hawatokei?
 
CCM hiyo hiyo inajua kima cha chini ni shs 270,000 na bado inaamua kulipa kundi fulani posho ya 300k. Kawaida ya mawazo ya ccm ni upside down.

Kima ha chini ni 240,000/- mkuu
 
Je serikali 2 zilizoboresha ni zipi? .......Mbona watanzania huku site hawaelewi serikali 2 zilizoboreshwa ni zipi?

Naomba Mwanachama wa CCM aje hapa atoe ufafanuzi, serikali 2 zilizoboreshwa zikoje? ....Muundo wake?

Kupinga serikali 3 bila kuwa na alternative ya kutatua kero za muungano ni uungwana kweli?

Katiba mpya bila kutatua kero za muungano ni kuwaingiza watanganyika matatani...
 
Haiwezekani makonda, lukuvi na komba wameze maneno Yao. Labda wabadilike jinsia
 
Back
Top Bottom