Ukawa siasa za "ujanjaujanja" hazidumu;Wakazi wa mabondeni waondolewe!

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
16,003
Habari zenu wana JF!

Leo ni mara ya pili kuwapa wito hasa Meya wa Jiji na wabunge wa Ukawa ambao kwa pamoja waliweka zuio mahakamani ili kuwawezesha wananchi kuishi maeneo hatarishi.

Kwa wananchi ambao walibomolewa bonde la mkwajuni kwa sasa wanafurahia maisha kwani kutokana na mvua hizi familia zao zipo salama.Ni wakati sasa kuheshimu maamuzi ya mahakama ambapo wiki iliyopita iliamuru wakazi wa mabondeni wahame bila fidia.Ikumbukwe miaka ya 90 kipindi cha Elnino Mkuu wa Mkoa DSM aliwahamishia wakazi wa bonde la mto msimbazi maeneo ya Segerea,Mbunge wa Ilala Iddi Simba akaleta siasa ati wapiga kura wake hawawezi kuishi porini na fisi.Waathirika wa mafuriko ubungo walihamishiwa wazo hill na mbweni,wengi waliuza maeneo waliyopewa.
Kwa waliobaki wengi hawaishi kwa kuhofia mafuriko hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Tusijenge kumbukumbu mbaya ya kufidia wavunja sheria kwa kigezo cha umasikini.

Wabunge na madiwani wa CCM walilea huu ujinga wakifikiri wanalinda "wapiga kura" wa...lakini cha moto wamekiona...sasa kwa kasi wabunge na madiwani Ukawa mmeuvaa huu ujinga,utawaumiza waambieni wananchi ukweli ili mmalizane nao mapema.Wapo leo wanazidi kuamia mabondeni sababu wanategemea siku moja kulipwa fidia.

Suluhisho;
Kwa kuwa ukawa mnaongoza halmashauri ya ilala na kinondoni,hakikisheni mnapitisha azimio la kuwafidia wananchi hao...la sivyo hao "wapiga kura" ndio watakuwa angamizo lenu,muwalipe mliyowaahidi ili jiji liwe na mpangilio.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom