ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,692
Vita ni maandalizi na watalaamu wa vita wanasema wakati mzuri wa kujiandaa na vita ni wakati wa amani. Huwezi kushinda kama unategemea wakati wa mapambano ndio uandae silaha. Sasa ni wakati wa kufanya maandalizi ya kutafuta mtu sahihi atakayepeperusha bendera ya ukawa. Ni mtu mjinga anayefikiria muungano wa Ukawa unaweza kuvunjika lakinj ukawa hauwezi kuvunjika kwa sababu vyama vikubwa vyote cuf na chadema wamenufaika mno na umoja huo . Nccr wanaonekana kupoteza kwa sababu ya mazingira yaliyopo kwamba walijiimarisha zaidi mkoa mmoja wa kigoma na ACT nao walikuwa na njama ya kuona nccr inakufa mkoani humo lakini mbili ccm walishaonyesha kwa namna yoyote ile lazima majimbo yote ya kigoma yarudi ccm . Kwa hiyo hata hivyo kama si ukawa hata hilo jimbo moja wasingelipata. Naimani cuf na chadema hawawezi kuuwa umoja wao .
Kwa upande wangu Lowasa alikuwa bado ni asset kubwa ndani ya ukawa tatizo ni umri tu hadi 2020 atakuwa na miaka 67, lakini vinginevyo bado angefaa . Intelligensia ya ukawa waanze kutafiti kimya kimya watu sahihi wanao weza kuvaa viatu 2020. huyu mtu awe ambaye amewahi kushika Nyadhifa za juu serikalini na alikuwa mwadilifu, atoke maeneo ambayo yana wapiga kura wengi kama kanda ya ziwa au kaskazini hii itasaidia sana .