Ukawa ruksa kufanya mikutano nchi nzima

Ukawa ruksa kufanya mikutano nchi nzima

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,930
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa ruksa kwa wanachama wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufanya mikutano yao nchi nzima.

Pinda alizungumza jana wakati akifunga maonyesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, alisema yaliyotokea bungeni yanaweza kumalizika kwa kukaa meza moja ya majadiliano.

“Yale mambo ya bungeni yanaweza kumalizika na tukaendelea kama ambavyo ilikuwa katika majadiliano ya kutengeneza kanuni. Tulikuwa tukishindana kwa kukaa meza moja na kumalizana, kisha tunaendelea sasa hili tumeshindwa nini?” alihoji Pinda

Alisema: “Walitoka bungeni na kusema watazunguka nchi nzima, nasema wazunguke tu kuwaeleza wananchi na sisi hatutashindwa kuzunguka kwani hoja tunazo.”

Waziri Mkuu Pinda alitumia nafasi hiyo kuelezea kauli aliyoitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kwenye Kanisa la Methodist kwamba hoja ya serikali tatu ikipita inaweza kulifanya jeshi kuchukua madaraka.

Alisema nilimpigia simu nikamweleza: “Rudi mara moja ueleze kilichotokea huko na nafikiri mlimsikia alichokisema.”

Lukuvi akitoa ufafanuzi bungeni bila ya kuwapo kwa Ukawa alisema: “Nayasema yote haya kwa kuwa naamini huo ndio msimamo wangu na utakuwa msimamo ambao wakati wote utaendelea kuwa hivyo na ninawataka ndugu zangu kuacha unafiki.”

Kutokana na kauli hizo, Ukawa inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, DP na NCCR-Mageuzi na wajumbe 25 kutoka kundi la 201 walitoka bungeni Jumatano wiki hii na kuahidi kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kuwaleza wananchi kilichotokea.

Hivi haya mamlaka makubwa wanayojipatia haya WATAWALA kama Pinda wanayotoa wapi? au ndiyo kulewa madaraka. Pinda anapata wapi mamlaka ya KUZUIA na KURUHUSU mikutano ya vyama vya SAISA? Naomba anieleze ibara ya katiba inayompatia mamlaka hayo. Hii sio mara ya kwanza Pinda amewahi kufanya hivyo. Hata kule Mtwara alipiga marufuku ya mikutano ya vyama vya siasa. Ninanong'enezwa kwamba bado hiyo Marufuku inafanya kazi huko Mtwara.
 
Kwahiyo yale maneno ya Lukuvi alitumwa na Pinda kwenda kuyaongelea kanisani?
 
Sio vibaya ngoja wote / yeyote anayeweza kutoa elimu atoe kwa nafasi yake bila kubanwa.., so long as havunji sheria wala kutangaza chuki au kuleta propaganda za kuchafuana / kutishiana
 
Dingswayo said:
...........“Walitoka bungeni na kusema watazunguka nchi nzima, nasema wazunguke tu kuwaeleza wananchi na sisi hatutashindwa kuzunguka kwani hoja"........

Kauli hii ndiyo inanichefua. Kama si kauli ya kiongozi mkubwa kama waziri Mkuu! Hivi kweli haelewi gharama ya ujinga huo? Mke awe wake au wa mume mwingine akiaamua kugawa nje ya ndoa suluhisho lake ni yeye au mume mwingine naye aamue kuchapa nje kwasababu tu mke ameamua kugawa nje ya ndoa? Kweli huu ni ujinga wa zama hizi (Kabudi, 2014).
 
Zinaitwa kauli za kubwa jinga
 
Pinda hajaruhusu,nasikia polisi wa zenj wananoa virungu kwa ajili ya matumizi ya jumatano.
 
Zinaitwa kauli za kubwa jinga

Hujakosea! Nchi yetu tumefika tulipo (uchumi umekuwa lakini percent kubwa ya watanzania huishi chini ya dola moja kwa siku! masikini) kwasababu viongozi wetu wanakosa maarifa. Sehemu kubwa ya utumishi wao wanafikiri ni vipi ccm itatawala milele kama si ni vipi watoto wao watachukua nchi baada ya wao kustaafu! Hovyo sana!
 
Pinda hajaruhusu,nasikia polisi wa zenj wananoa virungu kwa ajili ya matumizi ya jumatano.

Wazanzibari wanaeleweka si wajinga wala waoga kama huku kwetu. Kwao kuishi uhamishoni kwasababu ya kutetea haki yao si kitu kigeni. Polisi wakitumika vibaya, tutasikia Mapinduzi mengine.
 
waje kwa mpangilio ili tuwapime - wale wa serikali 2 na wale wa 3 - halafu tupige kura. kama walivyofanya wa Kenya - chungwa na ndizi. huo ndo utakata mzizi wa fitina
 
Wazanzibari wanaeleweka si wajinga wala waoga kama huku kwetu. Kwao kuishi uhamishoni kwasababu ya kutetea haki yao si kitu kigeni. Polisi wakitumika vibaya, tutasikia Mapinduzi mengine.

Mauwaji na sio Mapinduzi ndani ya Muungano. Ndani ya Muungano Mapinduzi ni ya Daima - CUF wanalijua hilo
 
Wazanzibari wanaeleweka si wajinga wala waoga kama huku kwetu. Kwao kuishi uhamishoni kwasababu ya kutetea haki yao si kitu kigeni. Polisi wakitumika vibaya, tutasikia Mapinduzi mengine.

Hapo umesema neno na kuna weng wametoka somali walikuwa kule kama miaka 10 wanajifundisha vita. Kwa zanzibar ndio mwanzo wa ukombozi

Nimekubali watanganyika ni waog sana migambo 2 wanawaondosha na kusafisha mji mzima. B
 
Kauli hii ndiyo inanichefua. Kama si kauli ya kiongozi mkubwa kama waziri Mkuu! Hivi kweli haelewi gharama ya ujinga huo? Mke awe wake au wa mume mwingine akiaamua kugawa nje ya ndoa suluhisho lake ni yeye au mume mwingine naye aamue kuchapa nje kwasababu tu mke ameamua kugawa nje ya ndoa? Kweli huu ni ujinga wa zama hizi (Kabudi, 2014).

Umemsahau alisema bungeni liwalo na liwe likamkuta Ulimboka,
 
Back
Top Bottom