- Thread starter
- #21
Naomba nikuulize mleta mada, hivi tatizo la maji liko Monduli tu au liko kona zote za Tanzania kuanzia vijijini hadi mijini? Je Lowassa amewahi kuwa Raisi wa Taifa hili? Ni lini alichaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Tanzania? Ndio maana anaomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania aweze kuleta mabadiliko tunayoyahitaji. Ngoja nikupe ushahidi wa ninachokisema;
Reuters, naomba nikutembeze sehemu tofauti hapa Tanzania, mijini na vijijini uone mwenyewe shida ambayo wananchi wa taifa hili wamekuwa nalo kwa muda wa miaka zaidi ya hamsini ya CCM. Hizi picha zimechukuliwa kwa wakati tofauti na katika mazingira tofauti zikionesha hali ilivyo Lindi hadi Mara, Dar es Salaam hadi Kigoma na hapa sijaweka picha za mkoa wa pwani anakotoka Raisi wetu wa sasa Jakaya Kikwete. Haya twende;
View attachment 294305 View attachment 294306View attachment 294320 View attachment 294307 View attachment 294308 View attachment 294309 View attachment 294310 View attachment 294311 View attachment 294313 View attachment 294315 View attachment 294312 View attachment 294314View attachment 294316 View attachment 294318Picha ya kwanza kabisa ni ya Dar es Salaam na picha ya mwisho kabisa ni ya Songea, hayo ndiyo maendeleo chini ya CCM na sasa wanatuomba tena Watanzania tuwape tena miaka mitano...ni uenda wazimu!
View attachment 294317 View attachment 294319
Vizuri sana Kwa kuonyesha picha ila nikuambie kitu kimoja huyo anayegombea ukawa alikua Waziri Mkuu na Huyo kampeni meneja wake Sumaye amekaa miaka 10 hakuweza kulitatua hilo miaka yote hyo tena wakiwa watendaji wakubwa tu Leo hii wanaitaka nchi wakafanye nini Ikulu?