UKAWA ni adui mwingine Tanzania

UKAWA ni adui mwingine Tanzania

Yani Ukawa hata aibu hawana jamaniii... Alafu wao ndio wanakusanya kodi lakini wanaishia kuziiba na nyingine kuzipeleka kwenye matumizi ya anasa badala ya kuzitumia kwenye shughuli za maendeleo ya taifa kama kununua madawati, alafu hapo hapo wanakuja tena mitaani kwa wananchi maskini kuwachangisha kwa nguvu hela ya madawati, khaaaaaaa

Hivi hii michango ya kinguvu ya madawati sio kinyume cha haki za binadamu kweli?
 
Yani Ukawa hata aibu hawana jamaniii... Alafu wao ndio wanakusanya kodi lakini wanaishia kuziiba na nyingine kuzipeleka kwenye matumizi ya anasa badala ya kuzitumia kwenye shughuli za maendeleo ya taifa kama kununua madawati, alafu hapo hapo wanakuja tena mitaani kwa wananchi maskini kuwachangisha kwa nguvu hela ya madawati, khaaaaaaa

Hivi hii michango ya kinguvu ya madawati sio kinyume cha haki za binadamu kweli?
Yani wamekuwa kero sana hawa ukawa ..wanakusanya kod...ila zinapo pelekwa hatujui wanakuja kutaomba michango ya madawati
 
Hawa 'UKAWA' ni laana kwa kizazi hiki na kizazi kijacho...!
 
Wanajavi,

Leo mimi nimekuja hapa kuleta kero zangu kuhusu hawa jamaa wa UKAWA na mawakala waoyani ACT wazalendo nampongeza sana mzee wangu ,Lytonga Mrema kwa kuwapasha ukweli hawa UKAWA. Mzee wangu Mrema ukiwa hapo Kilaracha pole sana na majukumu umekuwa sio mtu wa kujipendekeza kwa watawala kwa sasa umejiajiri.Nikupongeze pia kwa kura ulizopata kwenye uchaguzi wa mwaka jana kura 6,000 sio ndogo watu walitambua utumishi wako ulio tukuka japo, kibaraka uchwara wa UKAWA Mbatia alitangazwa mshindi kwa kura 60,000 na zaidi. Mzee wangu hawa vibaraka uchwara wamenisababisha nije leo hapa kunena ya fuatayo juu yao:

Tangia uhuru mpaka miaka ya hivi karibuni TANZANIA imekuwa inapigana na madui wake ambao ni ujinga, maradhi na rushwa, ila hivi karibuni karibuni baada ya mtukufu mpendwa wetu rais Dr. John Pombe Magufuli kuingia madarakani kumeibuka adui mwingine huyu UKAWA, huyu adui amekuwa mbaya zidi wa wale maadui wengine waliopita adui huyu ubaya wake ni huu:
  • UKAWA,wameingiza taifa kwenye dimbwi la umaskini kwa kuingiza kwenye mikataba mibovu mafano ile ya madini.Leo hii wanachi wanaozungwa na migodi ni maskini sana na sababu kubwa ni hawa UKAWA, kwa miaka mingi wamekuwa wanaingia mikataba ambayo sio rafiki na sisi wanachi.
  • UKAWA wamekuwa wanatukwamisha kimaendeleo huku mtaani kila kitu wame hodhi viwanja tulivyojenga wote wakati nchi ilikuwa, chini ya chama kimoja wanamiliki wao na wameshindwa kuviendeleza mpaka leo, japo wanapata mapato makubwa kupitia viwanja hivyo. Hata vile viwanja vya mitaani kwetu maeneo ya wazi wameuza na kula hela wao.
  • UKAWA, wamekuwa wanapitisha bajeti zisizo tekelezeka kwa kiasi kikubwa kila mwaka utekelezaji wa bajeti unakuwa chini ya 25% hasa kwenye miradi ya maendeleo. Tumewachoka huku mtani sikuhizi tukiwaona wanapita tunafumba macho japo ni wakali sana ukirusha neon tu kwao la kudhi unaweza hukumiwa miaka mitatu jela au faini ya milioni saba. Hivyo tunawangalia kwa jicho la kengeza na kuwaacha wapite.
  • UKAWA, bajeti ya 2016/17 wameipitisha kwa kishindo mpaka huku mtaani wengine tumehamki bajeti ya trillion 29 fedha za kitanzania, ambayo wengi tuliona haitekelezekei na mkanganyiko umeanzia pale kwenye VAT wengi wao hawa UKAWA sijui hawaelewi maana ya maneno kodi ya ongeeko la samani ( VAT).Wametufahamisha kuwa taasisi za fedha ndizo zitakazolipa ila nashangaa tumekuja kulipa sis walalji wa mwisho, kweli hawana huruma kwetu.Sasa tena line za simu tumeanza kuzilipia ya ni kodi kodi kodi. Nadhani wao haiwaumi kwasababu wao hawalipi hizo kodi na hatakama wanalipa mara nyingine wanauwezo wa kuzikwepa nawazatu nasikia ukivaa yale Magwanda yao ukienda kwenye ofisi zao kila kitu bure na mimi nipo njian kwenda kwenye ofisi zao pale buguruni au mtaa wa ufipa nipate hiyo tax exception.
  • UKAWA hawafai kabisa kwenye bunge la bajeti liloisha,japo nilikuwa silioni live kwasababu yule waziri wao anayejisifu kwa ushupavu wa kushawishi alishawishi UKAWA tusilione bunge live. Binafsi nlibahatika kuona vipande vya video vikionyesha wabunge hao wa UKAWA wakiwa wamepandwa na hasira kutetea posho zao na mafao yao yasikatwe kodi, nilishangaa sanaa ila hawakuwa na hasira kuona kodi ya bodaboda inaandishwa ,nashukuru wenzao wa CCM walikubali kukatwa kodi na wakaweka bayana ikibidi hata posho za vikao ziondolewe wabaki na mishahara tu, nawa shukuru wabunge hawa waccm kwa kuawa wazalendo.
  • UKAWA wamekuwa mizigo eti hawataki wenzao wafanye siasa mara zote wanataka wao ndio waongee tu, tuwasifie wao tu. Maana ya kutaka wasinongee wenzao ni hii wanataka wanachi wawasikilize wao tu na hawataki hoja mdala na maswali magumu wakuwajibu hayupo. Nadhani pia hawa jamaa wanaogopa wenzao wakiongea watavua mfalme nguo zake atabaki uchi.
  • UKAWA, wamekuwa janga kwa taifa na wafananisha na ile nchi ya vichaa inayo ongozwa na Mfalme **** wanapenda sifa wao tu…
Nimalize kwahili lililonichekesha kwa kitikio`` hakuna mikutano ya siasa mpaka 2020``...kila mtu anaitikia mpaka mabalozi wao…ukiona hivyo ujue wameishiwa UKAWA wakujibu hoja zetu hawana lazima wafunge midomo…ili kilamtu awe kimyaa...wafanye yao waendelee kutuibia kama kawaida yao. Nina mengi ila tuige busara ya mzee mrema ya kutopenda vyeo.
Haya bana kwa usanifu wako,.. ila hapa kazi tu ndio iko mujini siku hizi.
 
someni mumuelewe mtoa mada
Umeona ee! Kuna shida kidogo hapa JF ya uelewa. Mtoa mada ametumia tafsida katika andishi lake na wapo wanaompinga bila kumuelewa na wanaounga mkono pia bila kumuelewa.
Mie niongezee tuu kuwa UKAWA sio wazalendo kabisa, sisi tunataka sanamu ya Diamond iwekwe pale city center na wao wanapinga
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Umeona ee! Kuna shida kidogo hapa JF ya uelewa. Mtoa mada ametumia tafsida katika andishi lake na wapo wanaompinga bila kumuelewa na wanaounga mkono pia bila kumuelewa.
Mie niongezee tuu kuwa UKAWA sio wazalendo kabisa, sisi tunataka sanamu ya Diamond iwekwe pale city center na wao wanapinga
kuna tatizo la watu kutokusoma
 
Kabla ya ujio wa Lowassa niliiunga mkono CHADEMA na UKAWA 100%
UKAWA ya sasa haina tofauti yoyote na CCM.
Hii nchi viongozi wazuri wanapatikana kwa kudra za Mungu tu na sio umakini wa vyama.
Kama Mungu asingeingilia kati Lowassa leo ungekuwa rais.
 
Ukweli hata ukapinduliwa, ukawekwa in a sarcastic way... bado utakua ukweli.

Tatizo la nne la hii 'nji' hii ni ukawa wa leo. Tunasubiri ukawa ya 2020 tuipime tena.
hujaeleweka mkuu...hoja yako ni nini hasa?
 
Ukawa ni wapinga maendeleo.

Hawajachangia hata mia kwenye madawati ya watoto lkn hela ya maandamano nchi nzima wanayo!!!
Sanasana wamechangia mvinja sharia. Hivi kweli kiuna mtu anathubutu kuwa sambamba na UKAWA.Wametupotezea muda wetu na bado wanalipwa kodi zetu kwa kwenda kuuza sura Dodoma kwa kweli haikubaliki na mchakato wa katiba uanze upya mengi tuyaongeze! Haw UKAWA wanaweza kweli kuwahimiza mfano watoto waende shule kweli??? Endapo wenyewe wakubwa wa zima wanaowezakujitetea eti wanagoma kisa hawampendi Fulani. KWeli Watanzania tu wapole!
 
Asante umetumia fasihi vzuri
CCM walifikiri hoja inahusu ukawa kumbe n wao
Adui wa usalama wa taifa n CCM
Tusaidiane kumuondoa kwa hali yyt
Sasa nathibitisha kuwa ni lazima uwe mpuuzi ndio unaweza kuona ukwa ni wa maana na mleta uzi ni mmoja wao
 
Back
Top Bottom