Eti huu nao ni uchambuzi......afadhali tu ulivyoweka wazi kuwa u kada wa CCM, hucho ndicho nilichokiona ila si uchambuzi, hembu tuongelee kufuata mkumbo na uoga......Magufuli kafuta safari za nje kwa sababu zinalitia Taifa hasara, misukule munapiga makofi, wakati kina Mbowe na wenzake wanasema hizi safari zinatia hasara Taifa na mulikuwa munawatukana na kusema zina Tija kwa Taifa,CDM wamesema ndani ya musimu yote ya bunge kuwa sheria za manunuzi hazifuatwi na zinatoa mwanya wa rushwa, hakuna aliyewasikiza zaidi ya kuwaita waongo....leo kasema Magufuli, fuata upepo wote munashangili......nakumbuka Mbowe alishahoji siku moja khs ujenzi wa jengo la VIP pale airport, gharama zake mukataka kumtoa roho.....leo Magufuli anasema bic inanunuliwa kwa elfu 10, makofi na vifijo......meno ya tembo, imesemwa mara nyingi kuna wahusika huko serikalini wanashirikiana na majangili, mpk ikasemwa ndege ya Rais wa China ilisafirisha shehena, bungeni mukaja juu hatari.....juzi kasema Magufuli.....mukalipuka na makofi ya hatari.....sijataka kuongelea ya zanzibar kwa sasa, nimeamua tu kukuonyesha ni nani nyumbu na mwenye nidhamu ya woga kati ya CCM na CDM, hembu pima uone, mifano ni mingi ila tafakari hayo machache kwanza.