mozes
Senior Member
- Jan 11, 2012
- 115
- 21
Umoja wa Katiba ya wananchi ni vuguvugu jipya kuwahi kutokea Tanzania, kitendo cha vyama vikuu vya upinzani kuwa pamoja ni tendo jema lenye mwelekeo wenye nguvu kuiondoa CCM madarakani lakini wasiwasi wangu ni juu umoja wa kundi hili. Je, ni kweli kuwa wataweza kumsimamisha mgombea urais mmoja? Tanzania tumekua na viongozi waliovaa joho la uzalendo lakini wengi wao sio wazalendo sasa UKAWA wanaweza kuwa wazalendo kama wanavyojitanabaisha? Ili tuwe na ukombozi wa kweli katika TZ lazima ukawa wabebe agenda mbili muhimu 1. Katiba na tume huru ya uchaguzi 2. Daftari la wapiga kura liboreshwe. Hapo ukombozi ni wazi la sivyo ni jeramba mlimani