Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,466
Bunge la katiba tayari limegeuka kuwa bunge la katiba ya CCM. Ukawa warudi au wasirudi maoni yao hayataweza kusikilizwa wala kuingizwa kwenye katiba mama. CCM kwa wingi walionao BMK wanaweza kubadili kanuni na vipengere kadhaa ili wafanikiwe wanachokitaka.
Ukawa wanatakiwa wajue haswa wanataka nini? Ili waweze kufanikiwa na haja yao ya kupatikana kwa katiba ya wananchi lazima wakubali ku take high risk. Moja kutokurudi kabisa kwenye bunge la katiba ili katiba iwe ya CCM sio Taifa tena. Pili muungano wao uwe wa kweli, dhati, na wakubali kushirikiana kwenye uchaguzi mkuu ujao kuanzia serikali za mitaa kwa kufanya kuanzia primaries pamoja ili kupata mgombea anayekubalika na pande zote ama
Tatu kila chama kiwekeze nguvu zake katika kuhakikisha wanachukua wabunge wengi 2015 na kushinda viti vya uraisi. Wakiwa wengi bungeni kutatokea kusikilizana kwani inaonyesha pamoja na uchache wao wanaweza kutikisa, wakiongeza wabunge wapya mi kwa pamoja hali itakuwa nzuri.
Nne kuhakikisha wanawaingiza bungeni watu makini, wasomi wa kada zote, wachumi, wanasheria nguli, wanasayansi, na wenye elimu za biashara ili kutokuwa kama Ma CCM.
Vigezo vya kugombea viongezwe ili kupata watu makini na kutengeneza bunge lenye tija.