Peter Dafi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 389
- 272
Ni Hivi majuzi tumewasikia vijana wa BAVICHA wakitangaza eti watakwenda Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM na kwa hakika niliwaonea huruma.
Lakini Imekuwa Kila Siku wanaibuka Kila Mkoa nakuropoka tu kuwa Wataenda Kukwamisha Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma.
Nashangaaa....!
Hivi ndio kusema ubunifu wa vijana wa UKAWA umefikia mwisho kabisa hapa nchini Tanzania?
Kweli vijana ambao walikuwa wakijipambanua kuwa wao ni mahiri na wazungumza hoja kumbe hizi ndio Hoja za kuzuia Mkutano wa Ndani wa CCM?
Kijana Sosopi, Patrobas nawengineo mmefilisika kwa Mwendo kasi mpaka leo mmefikia hatua hii! Hizi ndo siasa za sasa kweli naanza kuamini maneno ya Prof Kitila Mkumbo aliposema "Upinzania Tanzania utajimaliza wenyewe kwa kutegemea udhaifu wa serikali"
Wako wapi vijana wa Chadema waliokuwa na hoja za kufikirisha hadi sasa zinaibuka hoja za kufilisika?
Nimeandika haya leo, kimsingi ni kuwatakia kila la kheri katika azma yao hiyo!
Lakini kwa kuwa vijana hawa wanasema kisha ndipo wanafikiri, basi wakiwa wanaelekea Dodoma kukipata wanachokitaka, nawakumbusha tu haya;
1.Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa mikutano ya ndani ya vyama haiingiliwi hata na polisi na ndio maana hata mikutano ya viongozi wa juu wa Ukawa wenyewe wanaokutana mara kwa mara haijaingiliwa na chombo chochote;
2.Hakuna zuio la mikutano ya ndani katika nchi hii ndio maana kule Dodoma kila siku wabunge wa Ukawa walikuwa ama wakikutana katika mikutano yao ya kimkakati au waliachwa wajinafasi kwa kufanya mikutano na vyombo vya habari kila walipotaka na kuropoka walivyotaka;
Nilidhani vijana hawa wangetumia akili na nguvu walizopewa walau kwenda kusaidia shughuli za maendeleo japo katika majimbo ya Ukawa kama vile kusaidia utengenezaji wa madawati,kusaidia ujenzi wa miradi ya maji,kwenda kukaa na kuwafundisha ujasiriamali vijana wasio na elimu n.k lakini kumbe sivyo.
Kwa kuwa akili zao zimeshikwa mahali na wakilala,wakiamka wanawaza siasa tu, nawakaribisha sana Dodoma maana mimi nitashiriki katika majukumu yangu ya kikazi na watakipata tena kiurahisi sana wanachokitaka.
Lazima tuweze kutofautisha Siasa na Matamko ya kisiasa.
Nawakumbusha tu kuwa 65% ya washiriki wa Mkutano mkuu wa CCM ni Vijana.
Ivo Tunawakaribisha na tutawapatia Dawa Stahiki Nakuwatimizia Hitaji lenu kisawasawa kulingana na Uhitaji wenu.
Kumbukeni tu! CCM Tumejipanga, na CCM ni Ile Ile ya Mbelee kwa Mbeleee..
Hapa Kazi Tu!
By Peter Dafi
Mtetezi wa Wanyonge.