UKAWA mnchezea shilingi kwenye tundu la choo

Tunko

Senior Member
Dec 24, 2013
181
41
Wanajamvi,

Kwa jinsi nilivyofuatilia hotuba ya RAIS wetu mpendwa JK ni wazi kuwa katiba iliopendekezwa inaweza kupatikana kabla hata ya uchaguzi.

Ina maana kuanzia leo tunahesabu siku 84 tupate katiba mpya na hilo nahisi litakuwa hivo kwa sababu wasipofanya hivo itabidi muswada upelekwe bungeni ili kurekebisha masharti yanayosema ipatikane siku 84 baada ya Rais kuipokea.

Hongera Rais na sisi wazalendo tunataka katiba ipatikane mapema.UKAWA imekula kwenu endeleeni kuandamana wakati sisi tunaipigia kura katiba.
 
Hapana ,Katiba haivuki itakwama tu kama ulimsoma Kikwete ,tunaweza kusema alijikaza sana sana kuitetea na kuisifu kuwa ni nzuri ,kama uliangalia Star TV ,huko mitaani ni HAPANA ,kuna wengine ndio wanapasua wazi kabisa kuwa maoni yao yametiwa kapuni ,HAPANA Tanganyika HAPANA Katiba ,huna la kuwambia Katiba nzuri kwa mapepari wa CCM na si kwa mwananchi wa kawaida ,wamejaribu kuipaka mafuta na kuivisha kilemba cha ukoka ,sijui wafugaji,wakulima,baraza la vijana ,walemavu,wanawake na samli kibao ,ila kuna maalumu mambo hayo ndio muhimu na wewe huwezi kuyaona maana utavamia kusoma hizo samli na kuondoka na mng'aro mwili mzima.
 
Kwani katiba ni mashindano nyie wapuuzi wa CCM....UKAWA hawataumia kwa lolote...wanaoumia ni wananchi watakaoteseka na katiba mbovu kwa miaka mingi ijayo...including wewe na wajukuu wako na watoto wa wajukuu wako
 
Hapana ,Katiba haivuki itakwama tu kama ulimsoma Kikwete ,tunaweza kusema alijikaza sana sana kuitetea na kuisifu kuwa ni nzuri ,kama uliangalia Star TV ,huko mitaani ni HAPANA ,kuna wengine ndio wanapasua wazi kabisa kuwa maoni yao yametiwa kapuni ,HAPANA Tanganyika HAPANA Katiba ,huna la kuwambia Katiba nzuri kwa mapepari wa CCM na si kwa mwananchi wa kawaida ,wamejaribu kuipaka mafuta na kuivisha kilemba cha ukoka ,sijui wafugaji,wakulima,baraza la vijana ,walemavu,wanawake na samli kibao ,ila kuna maalumu mambo hayo ndio muhimu na wewe huwezi kuyaona maana utavamia kusoma hizo samli na kuondoka na mng'aro mwili mzima.

Katiba hii itapita kwa kishindo hilo halina wasiwasi
 
Baelezee...longa...wape vidonge vyao....KWELI KABISA WAMECHEZEA SHILINGI KWENYE TUNDU LA CHOO...sasa wanaweweseka na sisi tunaomba sana Mungu abariki ndani ya siku 84 tupige kura ya maoni....USHAURI KWAO wanaojiita UKAWA....Kodisheni Chopa kumi zungukeni miji yote, mtaa kwa mtaa, kata kwa kata, wilaya kwa wilaya....(@quotes za Slaa) muwashawishi wapiga kura wapige hapana lakini sisi tunazunguka hivyohivyo na kuwaelewesha jinsi katiba ilivyozingatia mahitaji yao kuliko madaraka mliyokuwa mkiyalilia...na watatupa kura ya ndiyo na KATIBA BORA ITAWEZEKANA....
Wanajamvi kwa jinsi nilivyofuatilia hotuba ya RAIS wetu mpendwa JK ni wazi kuwa katiba iliopendekezwa inaweza kupatikana kabla hata ya uchaguzi inaama kwanzia Leo tunahesabu siku 84 tupate katiba mpya na hilo nahisi litakuwa hivo kwa sababu wasipo fanya hivo itabidi mswada upelekwe bungeni ili kurekebisha masharti yanayosema ipatikane siku 84 baada ya Rais kuipokea.Hongera Rais na sisi wazalendo tunataka katiba ipatikane mapema.UKAWA imekula kwenu endeleeni kuandamana wakati sisi tunaipigia kura katiba
 
Katiba hii itapita kwa kishindo hilo halina wasiwasi

Ukiniambia itapitishwa nitakubaliana nawe ila kusema itapita,hilo haliwezekani kama ilivyokuwa haikupita kwenye theluthu basi ndio hivyohivyo ,na joto la kutopita ni pale Mh.Kikwete aliposema subira huvuta kheri ,na bado halijawa tayari ,sijui umemsoma vizuri ,amejawa khofu. Ila inataka ujuwe kumsoma mtu anapozungumza ,la kama ni mpiga makofi utaondoka na pumba kibao !
 
bora umsaidiye huyo kilaza
 
Nakubaliana kwamba KATIBA inaweza kabisa KUPITISHWA, lakini haiwezi KUPITA ili mradi ccm watakuwa bado madarakani. Ona wanavyosutwa na kura mbili ambazo hawana hakika nazo kuzitolea maelezo, wanafyekafyeka tu utadhani mtu mwenye matege akitembea juu ya uzi.
 
Semeni yote lakini nawaza ni nani atakaye kuwa mlinzi na msimamizi wa Katiba hii kama siyo wale wote walioipigania kwa muda wote huo. Kwa maslahi ya wabinafsi wachache nusura tubadili maana ya Historia yetu. Walio wengi wako radhi kupigania Mazoea kuliko Sheria/Katiba, ndiyo maana ya haya yote ya kutaka tugawanyike gawanyike kama moja ya makabila ya nchi yetu, nadhani ni ili kila mtu awe mkubwa kwenye eneo lake. Mimi siamini katika hayo. Wabinafsi wachache hawapaswi kutubadilishia maana. Umoja wetu ndiyo nguzo yetu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hapana ,Katiba haivuki itakwama tu kama ulimsoma Kikwete ,tunaweza kusema alijikaza sana sana kuitetea na kuisifu kuwa ni nzuri ,kama uliangalia Star TV ,huko mitaani ni HAPANA ,kuna wengine ndio wanapasua wazi kabisa kuwa maoni yao yametiwa kapuni ,HAPANA Tanganyika HAPANA Katiba ,huna la kuwambia Katiba nzuri kwa mapepari wa CCM na si kwa mwananchi wa kawaida ,wamejaribu kuipaka mafuta na kuivisha kilemba cha ukoka ,sijui wafugaji,wakulima,baraza la vijana ,walemavu,wanawake na samli kibao ,ila kuna maalumu mambo hayo ndio muhimu na wewe huwezi kuyaona maana utavamia kusoma hizo samli na kuondoka na mng'aro mwili mzima.

Na bungeni ilisemwa kuwa haitopita. Itakwama Dar ila mikoani itapita bila wasi wasi.
 
Maharamia wote nawahakikishia lazima ikwame mm nimeishaanza kampeni nyumbani tayari sasa hivi niko kwenye ukoo nikimaliza nahamia kazini mtaani kisha namalizia kanisani
 
Back
Top Bottom