Fanfa
JF-Expert Member
- Sep 25, 2009
- 2,388
- 3,710
Lini vocha anasaini Kinana ili muanze kuzunguka nchi nzima kama UKAWA. Je mna watu wa kuvuta watu au ni Kinana, Mwigulu na swahiba wangu Kikwete. Ila fisi wenu hawana mvuto kwetu sasa hivi tumeshawazoea, kutupakia kwenye malori hatutaki tena ajali zimezidi.
Washauri wasije wakarogwa wakaaenda na agenda ya katiba pendekezwa kwa wananchi, WATAJIMALIZA kabla ya uchaguzi
.
Washauri wasije wakarogwa wakaaenda na agenda ya katiba pendekezwa kwa wananchi, WATAJIMALIZA kabla ya uchaguzi
.
Hatulali.Hatuli,tukashiba. Hatuwazi tukang'amua. Hatupigi tena stori maofisini na kupumzika kidogo. Acheni sifa za kijinga. Mnataka tuwe tunatumwatumwa kila wakati au? Mnataka nyaraka-kemea ziendelee kutamalaki chamani mwetu? Acheni hizo. Ndiyo nini kugawana mikoa mbalimbali ya Tanzania na kushambulia kama nyuki? Mnalenga nini? Sifa zitawaua nyinyi UKAWA.
Kwa taarifa yenu, nasi tunasubiri 'mambo fulani' yaidhinishwe ili tuje kuwajibu mapigo yenu na tuvijibu vihoja vyenu kwa hoja za haja. Tutafanya mikutano ya mfano na si ya ngano. Tutafunika na kuwashika. Hakakuwa na ACT wala UKAWA.CCM ikianza kuunguruma,wote mtajificha. Sifa zenu zitawaponza!
Endeleeni tu kutuchokoza. Kama mbwai,itakuwa mbwai kweli!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam